Pombe imechachuka

Kama alivyokula matapish mbowe kwakumlamba miguu lowasa

HIyo unayotaka kuleta wewe ni THREAD nyingine anzisha ili tuijadili, usichanganye na hii.

kwa hiyo unakubali kuwa SIFUNI MCHOME amekula matapishi yake?????

kwa nini Rais Magufuli anakaa na watu ambao wanayumba kama upepo hawana hata mwelekeo????

Je, hajui kuwa hawa watamuharibia sifa yake ambayo kwa muda mfupi hadi nchi za nje amefahamika???

Kwa nini anakumbatia viongozi ambao ndio waliotufanya tuwe katika hali ya sasa yaani wale wa awamu ya nne???

Je, au ndio makubaliano ya kikao cha juzi?????


TUMEKUBALI CCM NI ILEILe!!!!!!!!!! HAKUNA MABADILIKO NDANI YA SERIKALI HII ISIPOKUWA MAKINI
 
Kweli mkuu ccm ni ile ile. Na mawaziri ni wale wale....Muhongo, Mbarawa, Mwakyembe, Makamba, Nchemba, Lukuvi, etal

Rais Magufuli amekaa muda mrefu kabla ya kutangaza baraza la mawaziri ni zaidi ya mwezi. Tulitegemea kuwa kuna MABADILIKO kumbe ametuletea awalewale akina MWAKYEMBE ambao walisifika kwa TUHUMA YA UFISADI SHIRIKA LA RELI KATIKA UNUNUZI WA MABEHEWA. TENA AMEMPA WIZARA YA SHERIA ILI IWE KAMA HUYU HAPA CHINI:-


kwa hiyo tusitegemee kama ile shutuma ya Shirika la Reli itafanyiwa kazi katika Awamu hii. Lazima ataifukia kama jamaa alivyofanya kuhusu Katiba Mpya.
 
Watanzania kwa wivu kwani Waziri aliyekuwepo awamu iliyopita kuna dhambi gani akiteuliwa tena hapa cha muhimu mawaziri wanatekeleza mambo ambayo Rais wa sasa anaagiza. Sasa watu wanataka sura mpya sijui zitoke sayari gani!!!


ina maana katika Wabunge wote wa CCM walikuwepo UWAZIRI awamu iliyopita????

Kuna wengiun ambao walikuwa ni wabunge na wamerudi bungeni mfano. Dr. Ndungulile wa kigamboni,Mbune wa Ilala, na wengine wengi tu!!!!!!

pia Rais amepewa nafasi ya kuteua Wabunge 10, pia kuna wabunge viti maalum!!!!

Yaani bado tu idadi ya hao MAWAZIRI 34 aliohitaji wasingepatikana katika hawa wote???

Au ndio kupeana fadhila / shukrani kwa kupiga debe vizuri katika kampeni bila ya kuangalia utendaji wa kazi???

AMA KWELI CCM NI ILE ILE HAKUNA MABADILIKO AMBAYO WALIKUWA WANAIMBA KATIKA KAMPENI!!!!!!!!​
 

Mkuu naona jamaa hujamuelewa vizuri. Anachokosoa nikwamba tangu uhuru serikali nimoja tu ya Ccm na Tanu. Watumishi wa serikali hii hii ndio waliotoa vibali kwa raia wakajenga maeneo yasiyo ruhusiwa. Sasa iweje hukumu iwashukie wananchi tu bila wahusika upande wa serikali kuchukuliwa hatua?
 

Hill jina unalotumia tu tayari unaonesha fikra zako zimekaaje ..sema unataka wapi leo ukakeshe kigodoro?
 

Mjiandae kufungua viwanda vya juisi tu ila si udarari wa gesi yetu
 

Ukimwona anayelia kuliko wote huyo huyo ndo mchawi wako ..unaonekana ulikuwa unahusika sana na sahivi tumefunga Magufuli, katambike mizambwa yako
 
siku moja baada ya sifuni mchome kuteuliwa katibu wizara ya elimu kuna mdau wa jf aliandika hivi nanukuu , " NAPINGA SIFUNI MCHOME KUTEULIWA KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU " mwisho wa kunukuu , uzi upo humuhumu jf , na baada ya muda mfupi ikaletwa divisheni 5 .
 

majority ya zilixzobomolewa hazikua na vibali... pia upande wa serikali, watu wanatimuliwa
 
Hill jina unalotumia tu tayari unaonesha fikra zako zimekaaje ..sema unataka wapi leo ukakeshe kigodoro?

Mkuu niko vizuri kiakili. Nimeandika ili kuelezea dukuduku langu kwa kile ninachokiona kwa huyu rais mpya.
 
Ni kweli usemayo mkuu. Huyu mtu hatokuwa na jipya. Anaendeshwa na mfumo ccm. Na ccm ni ile ile..

Tatizo lenu kubwa mnakosa uvumilivu, lakini pia mmezoea majungu.

Magufuli ndiyo kwanza ameanza kufanya kazi yake tulieni tumpe muda na ushirikiano sio kila kitu ni kuponda tu!

Eti huyu mtu hatokuwa na jipya... Kumbe mwenye jipya ni nani...Mbowe, Mbatia au Lowassa?

Tunajua wachache hampendi kuona Magufuli hakifanikiwa, lakini wengi tunamuombea kwa Mungu!

Near Tegeta Machinjioni.
 


NUKUU KATIKA MAANDIKO YA VITABU VYA DINI:-

"Huwezi kuweka Divai mpya katika chombo cha zamani" Mwenye masikio na asikie.
 
Ukimwona anayelia kuliko wote huyo huyo ndo mchawi wako ..unaonekana ulikuwa unahusika sana na sahivi tumefunga Magufuli, katambike mizambwa yako

KWa hiyo umekubali kuwa mfumo wa CCM umeshindwa kuongoza Miaka 54 toka tupate UHURU????

Je, Ni mabadiliko gani yanayoweza kuletwa leo hii na ikiwa mfumo bado upo.

Ukitaka kuumaliza mti yakubidi Ukate mizizi kwanza ndipo mti utakauka.
 
hiv inamana mtu ukiwa bavicha ndo unatokwa na akili kiasi hiki?yaani sioni points zaidi ya mipasho na wivu wakike,rudini kwenu mtuachie nchi yetu mb.wa nyie


hivi ukiwa ccm bila kuitukana bavicha hupandishwi cheo...ni wapi imeandikwa mtoa mada ni bavicha...mipasho anayo mwenyekiti wa ccm taifa ndo kafundisha kina nape na makonda
 

Hao uliowataja ndiyo wenye jipya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…