Kwa nini JK ahangaike hivyo!? Mbona yeye ni President tayari! Tena kila kinachoendelea yeye anaweza kudai ni yeye ameanzisha na wabongo wakamwamini! Kwa ajishushe hivyo. Tena anamwaga hela nyingi pasi na kifano. Jana amekusanya Tshs 900! Ni za nini tena, kama mabango anayo hata mengine ameyaweka stoo au mahali fulani, kama ni kanga nchi nzima ina kanga na vibandiko vyake, hata nyingine wamewapa wazungu wavae, hazina watu wa kuvaa. Kama ni magari wanayo na mapikipiki na baiskeli na Helikopta tatu. Sasa hizi M 900 ni za nini? Kuhonga siyo, ole wao wasioijua sheria!
Ila huyo Mzee sijui nani Jaji Makame, kwa nini hamkemee huyu Bw Mdogo wake. Kwa umri wake sioni kwa nini anaona shida, cheo na mamlaka ya kumhoji anayo, umri anao sasa anaogopa nini! Yahya hawezi kumdhuru kwa sasa yuko hospitali. Wahi Mzee mwonye maana atasababisha kero na kero hujibiwa na kero. Tusicheze na amani tuliyo nayO. Tukemee walau