Bawabu wa pili
Senior Member
- Nov 14, 2025
- 147
- 432
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa tahadhari kali kwa wananchi wenye tabia ya kupiga baruti au fataki bila vibali vya kisheria, likisisitiza kuwa hatua za haraka za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kuvunja sheria na kusababisha hofu au usumbufu kwa jamii, hasa katika kipindi cha kuelekea sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya.
Kupitia taarifa yake kwa umma iliyotolewa Desemba 22, 2025, jeshi hilo kupitia Kamanda wake mkuu wa Kanda Jumanne Muliro limeeleza kuwa linaendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kuzuia na kudhibiti vitendo vya kihalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama pamoja na wananchi. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hali ya usalama kwa ujumla ni shwari na wananchi wanaendelea na shughuli zao za kila siku kama kawaida.
Katika kuimarisha usalama kuelekea sikukuu, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeeleza kuwa litaendelea kushirikiana kwa karibu na wananchi pamoja na nyumba za ibada ili kuhakikisha usalama unaimarika kabla, wakati na baada ya ibada na mikusanyiko mbalimbali ya kidini.
Aidha, wazazi na walezi wametakiwa kuwa na uangalizi wa karibu kwa watoto wao wakati wa matembezi na mikusanyiko, huku wananchi kwa ujumla wakihimizwa kutoacha makazi yao bila uangalizi katika kipindi cha sikukuu.