Polisi yatoa tahadhari dhidi ya Al-Shabab

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
JESHI la Polisi Kanda ya Zanzibar limeiomba Jumuiya ya Maendeleo ya Wavuvi ya Watu wa Kojani (KOFDO) kutoa ushirikiano wa kiulinzi katika maeneo ya baharini ili kuweza kukabiliana na tishio linaloweza kufanywa na Kundi la Al-Shabab. Wito huo umetolewa leo kupitia mkuu wa kituo cha Polisi Bububu Inspekta Mwatum Omar Hassan, alipokuwa akizungumza na jumuiya hiyo katika Ukumbi wa CCM Mtoni Mjini Zanzibar.

Alisema kwa vile kundi la Alshabbab linafanya hujuma zake kupitia maeneo ya baharini,Wakojani wanaweza kusaidia sana kuepusha hujuma hizo kwa vile shughuli zao za kila siku huzifanyia baharini. Inspecta Mwatum amewataka Wanajumuiya wa KOFDO kufanya kazi ya ulinzi shirikishi katika eneo la Baharini kwa kutoa taarifa kwa jeshi hilo pale ambapo wataviona vyombo vigeni vya baharini na kuvitilia shaka.

“Kama mtaona chombo kigeni kwenu baharini chenye watu wenye wasifu wa Kisomali au Kiethiopia basi mtusaidie kuleta taarifa katika Jeshi letu, maharamia hawana wema kazi yao ni hujuma tu,” Alisema Ispecta Mwatum Aidha Inspeta Mwatum aliwataka wanajumuiya hiyo kuwafichua wale wote wanaoendesha biashara za magendo na madawa ya kulevya katika maeneo ya mwambao na kuwahakikishia ushirikiano kutoka kwa jeshi hilo.

Ameeleza kuwa taarifa ambazo wanajumuiya hiyo watazitoa kwa Jeshi la Polisi zitakuwa siri na kuahidi kuzifanyia kazi ipasavyo ili kuweza kuepukana na madhara ambayo yanatokana na magendo.

Kwa upande wao wanajumuiya hiyo wamelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuonesha ushirikiano wao kwa Jumuiya hiyo na kuahidi kufanya kazi kwa pamoja na Jeshi hilo. Aidha wamelitaka Jeshi hilo kufanya kazi ya ziada ya kuwakutanisha wao na Idara ya Uvuvi Zanzibar ambayo imekosa mashirikiano ya dhati na Jumuiya hiyo.

Wamesema kama ambavyo Jeshi hilo limeonesha njia kwa ajili ya kufanya kazi kwa pamoja na Jumuiya hiyo, ndivyo ambavyo wangependa pia kufanya kazi na Idara ya Uvuvi na Mazingira.

Jumuiya ya KOFDO ni jumuiya ambayo wanachama wake ni wavuvi ambao hufanya kazi za kivuvi mchana na usiku katika Bahari ya Hindi ambapo Makao Makuu yake yapo Mtoni Mjini Zanzibar. mwisho

chanzo. Polisi yatoa tahadhari dhidi ya Al-Shabab
 
Back
Top Bottom