Polisi yapewa siku 2 kumpata mwandishi aliyetekwa

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
Salmaaa.JPG

Mwandishi wa habari Bi. Salma Said,anaedaiwa kutekwa na watu siojulikana kwenye uwanja wa Mwalimu Julias Nyerere

Wakitoa tamko la pamoja, Katibu Mtendaji wa MCT Bw. Kajubi Mukajanga, Mkurugenzi wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu THRDC Bw. Onesmo Olengurumwa pamoja na mwenyekiti wa jukwaa la wahariri TEF Bw. Theophil Makunga wamesema kitendo hicho kinakwenda kinyume na misingi ya haki za binadamu.

Viongozi hao wamesema kuwa Licha ya kitendo hicho pia kuminya uhuru wa wanahabari na haki ya kupata habari, lakini pia kinajenga hofu kubwa miongoni mwa wanahabari na jamii kwa ujumla.

Aidha vyombo hivyo vimetaka vyombo vya usalama kuhakikisha vitisho vyote dhidi ya wanahabari na watetezi wa haki za binadamu visiwani Zanzibar vinakomeshwa na kuwaacha wawe huru kufanya kazi zao katika kipindi cha uchaguzi wa marudio.

Hivi karibuni Bi. Salma amekuwa akitoa taarifa mbalimbali za hali ya kisiasa visiwani Zanzibar kupitia Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani na mitandao ya kijamii ambapo alisema kuwa kuandika kwake habari hizo alikuwa akipata vitisho kutoka kwa watu wasiojulikana na hapo jana katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ilisemekana mwandishi huyo alitekwa na watu wasiojulikana.
 
Hakuna cha ccm uliwahi kuona wapi mtekwaji anaongea na simu? Huyu mdada atakuwa kajiteka mwenyewe kwa ujinga wake wa kisiasa.
...Kujiteka mwenyewe? Kama hiyo inawezekana nami kesho Jumapili ya Uchafuzi Zanzibar, ANAJITEKA pale KIA. Badala ya KUPIGA SIMU mie ntaandika ujumbe humu JF.....
 
Salmaaa.JPG

Mwandishi wa habari Bi. Salma Said,anaedaiwa kutekwa na watu siojulikana kwenye uwanja wa Mwalimu Julias Nyerere

Wakitoa tamko la pamoja, Katibu Mtendaji wa MCT Bw. Kajubi Mukajanga, Mkurugenzi wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu THRDC Bw. Onesmo Olengurumwa pamoja na mwenyekiti wa jukwaa la wahariri TEF Bw. Theophil Makunga wamesema kitendo hicho kinakwenda kinyume na misingi ya haki za binadamu.

Viongozi hao wamesema kuwa Licha ya kitendo hicho pia kuminya uhuru wa wanahabari na haki ya kupata habari, lakini pia kinajenga hofu kubwa miongoni mwa wanahabari na jamii kwa ujumla.

Aidha vyombo hivyo vimetaka vyombo vya usalama kuhakikisha vitisho vyote dhidi ya wanahabari na watetezi wa haki za binadamu visiwani Zanzibar vinakomeshwa na kuwaacha wawe huru kufanya kazi zao katika kipindi cha uchaguzi wa marudio.

Hivi karibuni Bi. Salma amekuwa akitoa taarifa mbalimbali za hali ya kisiasa visiwani Zanzibar kupitia Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani na mitandao ya kijamii ambapo alisema kuwa kuandika kwake habari hizo alikuwa akipata vitisho kutoka kwa watu wasiojulikana na hapo jana katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ilisemekana mwandishi huyo alitekwa na watu wasiojulikana.

Tags:
MCT Bw. Kajubi Mukajanga
Mkurugenzi wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu
THRDC
Bw. Onesmo Olengurumwa
mwenyekiti wa jukwaa la wahariri
TEF
Bw. Theophil Makunga
Salma Said
Uwanja wa ndege ya JKNIA kumbe mtu anaweza kutekwa enhee? Duh, basi abiria wanaosafiri kupitia uwanja huu go at your own risk....lol
 
Kama Ulimboka alivyojiteka, akajiumiza, akajipeleka hospitali na kama Mwangosi alivyojilipua mbele ya kamanda wa mkoa. Hii ni kweli na inawezekana kwa huyu dada kufanya hivyo. Fyokofyoko zao zitawafanya wakamatwe na washughulikiwe na Mungu yupo pamoja naye mkuu zidi kumuombea sababu yeye ni malaika mtarajiwa pamoja na waliomtangulia. Tutajijuuuuuuuu.
 
Back
Top Bottom