Polisi Yahusishwa Mauaji ya Raia Ukerewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi Yahusishwa Mauaji ya Raia Ukerewe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Regia Mtema, Jan 20, 2010.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  Jan 20, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Polisi yahusishwa mauaji ya raia Ukerewe [​IMG] Frederick Katulanda, Ukerewe

  WAKATI Jeshi la Polisi likitangaza kuendelea na msako wa majambazi wanaotuhumiwa kuvamia Kisiwa cha Izinga na kusababisha vifo vya watu 14, imebainika kuwa watuhumiwa wawili kati ya waliohusika na mauaji hayo walikuwa ni maofisa wa Jeshi la Polisi wilayani Ukerewe.

  Kwa mujibu wa taarifa za siri kutoka kwa majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya na baadhi wa wauguzi wa hospitali hiyo, majina ya maafisa hao yamebainika ambapo pia moja kati ya silaha zilizotumika zilikuwa ni mali ya Jeshi la Polisi.

  Taarifa hizo zimebainisha kuwa silaha hiyo ya polisi ndiyo iliyosababisha kuuawa kwa idadi hiyo kubwa ya wananchi kwa kile kilichoelezwa kuwa harakati za polisi hao kujiokoa wasibainike baada ya kuzidiwa nguvu na wananchi.

  Wakizungumza kwa siri kwa hofu ya kuhofia kuuawa, baadhi ya majeruhi hao wameeleza kuwa wameshindwa kutoa maelezo hayo kutokana na ofisa mmoja wa Jeshi la Polisi kuwaonya baadhi ya majeruhi hao wasibainishe jambo hilo na hivyo kushindwa kulielezea.

  "Mauaji haya ya wananchi wengi yametokea baada ya wananchi kuwazidi nguvu majambazi hao, lakini baada ya kuona wamezidiwa mmoja wa majambazi hao ambaye sauti yake na hata sura yake imetambulika kuwa ni askari polisi alimwambia mmoja wao aliyekuwa katika mtumbwi amejificha kuwapiga risasi wanannchi ili kuokoa silaha naye kuanza kuachia risasi na kuua watu saba papo hapo," kilieleza chanzo chetu.

  Alisema kabla ya kuanza kwa upigaji wa risasi, awali majambazi hao walikuwa wakifyatua risasi za rashasha za aina ya blancoo ambazo ameeleza kuwa mara nyingi zimekuwa zikimilikiwa na Jeshi la Polisi jambo ambalo wananchi waliligundua na mmoja wao kueleza kuwa hawana silaha na wananchi wengi kukimbilia kuukamata mtumbwi huo ili kuwatia mbaroni majambazi.

  "Katika tukio hili baadhi ya majambazi waliohusika ni pamoja na maaskari wawili ya Jeshi la Polisi ambao majina yao na wao tumewatambua ambao mmoja wao toka wavamiaji hao walifika kisiwani humo alikuwa na silaha amelala na kujificha katika mtumbwi,"alisema mmoja wa majeruhi hao

  Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba baada ya kufanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali ya kisiwa hicho alisema kuwa maafisa upelelezi wanaendelea kukusanya ushahidi kuhusu tukio hilo na kwamba malalamiko yanayotolewa kuhusu askari wake ni sehemu ya tuhuma walizopokea na kukusanya kama sehemu ya vielelezo vya uchunguzi.

  "Katika upelelezi tunakusanya kwanza kila kitu, tunachoambiwa na wananchi au kuona au kupokea. Unaweza kufika mwisho wa uchunguzi ukakutana na matokeo tofauti na vielelzo ulivyokusanya katika uchunguzi, lakini hatutapuuza, kila tunachokipokea tutakifanyia kazi,"alisema

  Manumba ambaye alikagua pia nyumba mbili za kulala wageni zilizovamiwa na majambazi hao na kuangalia maeneo yote ya kisiwa kwa ujumla alisema mwelekeo wao wa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea vizuri.

  Hata hivyo, kwa nyakati tofauti baadhi ya majeruhi wa tukio hilo walieleza uwezekano wa askari hao kuhusika na tukio hilo ni mkubwa kutokana na kubainika kwa baadhi ya vielelezo vya kipolisi katika mmoja wa maiti za tukio hilo la aina yake.

  "Ni kweli kuna baadhi ya vielelezo ambavyo tumevikuta chumba cha maiti kwa maiti mmoja ambaye hajatambuliwa mpaka sasa, vina uhusiano na vifaa vya kipolisi na tumewakabidhi polisi,"alieleza mmoja wa wauguzi katika hospitali hiyo ya wilaya.

  Ilisemekana mmoja wa watuhumiwa ambaye aliuawa na wananchi ambaye alikuwa akimiliki nyumba ya kulala wageni ndiye aliyekuwa na mawasiliano na askari hao na siku chache kabla ya tukio alionekana mjini Nansio akiwa na askari hao wawili ambao mpaka sasa maelezo yao na jinsi ambavyo wametoweka kazini hayajabaainishwa wazi.

  Taarifa hizo zimethibitishwa na ofisa mmoja wa polisi wilayani hapa ambaye amedai kuwa askari hao wawili wametajwa kuhusika na jeshi hilo limeanzisha upelelezi wa siri dhidi yao .

  "Ni kweli kuna wenzetu wametajwa na mwenendo wao na jinsi ambavyo walitoweka kazini unatia mashaka, lakini tumesikia ofisi ya Afande IGP (Said Mwema), imeagiza uchunguzi wao,"alieleza.


  SOURCE:MWANANCHI NEWSPAPER


  Haya jamani hii ndio tz bwana.Kila kukicha mauaji halafu watu waliopewa dhamana nao wanahusika kwa namna moja ama nyingine.Hivi tatizo ni nini hasa?je viongozi wa juu waheshimiwi?wamepoteza dira?tatizo ni nini?tujadili
   
 2. Kionambele

  Kionambele JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni vizuri Afande Mwema akaliangalia hili kwa makini. Watu kama hawa siku wakijigundua wana kansa isiyopona ni rahisi kutumiwa kupiga risasi hata viongozi wetu. Kwa hiyo hakuna aliye salama pale jeshi la polisi na majeshi yetu mengine yanapogubikwa na tamaa za mali kiasi cha kuua ili kulinda hadhi isiyokuwepo.

  Mheshimiwa JK, ni bora ufanye kama Mwl Nyerere ambaye baada ya coup attempt miaka ile aliamua kuvunja Jeshi. Ikiwa mambo haya yanaendelea jeshini na wahalifu hawa katika ngazi zote wanafahamika ni bora wakafutwa mapema kwenye ramani ya Jeshi kabla siku moja pesa wanazopata kihalifu hazijaongezeka na kujiundia jeshi lao wenyewe.

  Hawa watu iko siku watapiga dili kubwa zaidi. Kwa mfano wanaweza kuamua kuvamia msafara wa Rais kwenye ziara zake za mkoani kwa ambush kubwa kiasi cha kufanikiwa kufanya uhaini.

  Tusidharau tu kufikiri hili ni suala la ukerewe, jamani damu imemwagika na ni hatari kwa 'future' ya nchi yetu.
   
 3. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,640
  Likes Received: 21,851
  Trophy Points: 280
  Kama kawaida yetu baada ya uchunguzi na mambo kupoa, tutasema ni majambazi kutoka nchi jirani. Na kwamba raia wetu wamezoea kuishi kwa amani na utulivu chini ya sera safi za chama tawala. Shit!
   
Loading...