Polisi yahadharisha wapenda ngono | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi yahadharisha wapenda ngono

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Fidel80, Jun 16, 2012.

 1. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  MKUU wa Intelijensia za Jinai katika Jeshi la Polisi nchini, Hussein Laisseri ametaka jamii kuwa makini na ‘dada poa’ ambao hutumia udhaifu wa wanaume kuwalisha mihadarati na kuwaibia. Kauli hiyo ameitoa wakati akijibu hoja za gazeti hili kuhusu kuzagaa kwa maelezo kwamba wasichana hao hupora watu kwa staili ya kujipaka dawa hizo katika sehemu za miili yao zinazohusishwa na ngono. Alisema ingawa walioathirika huwa hawataki kusema, utafiti unaonesha kwamba matukio hayo yanaongezeka ingawa wanaofanyiwa huona haya kuzungumza. Laisseri, ambaye pia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SAC), alimweleza mwandishi wa habari hizi, kuwa mazingira ya aina hiyo ya uhalifu pekee, yanatosha kumfanya mtendwa asiseme ukweli wa kilichomkuta na kuifanya ofisi yake ikose rekodi ya matukio hayo kama inavyopasa kuwa. “Si unaona kwamba ni matukio ya aibu? Sasa unatarajia kuna mtu atasimama na kusema alikuwa na mama au dada poa, halafu akaleweshwa na kuibiwa kwa njia hiyo?“ Alihoji. “Kila anayewasilisha madai ya kuibiwa fedha nyingi katika mazingira yasiyoeleweka, hueleza kuwa waliofanya hivyo ni wahalifu anaohisi kuwa ni majambazi au wezi wa ‘kuwinda’, hatuwezi kulazimisha mtu aseme kuwa alitendwa na ‘mtu wake’, hata kama ilikuwa hivyo, hadi ushahidi uthibitishe na si hisia,” alisema Laisseri. Aliwataka wanaokumbwa na kadhia hizo, wasifanye siri, bali walieleze Jeshi la Polisi ili wasaidiwe. Kwa mujibu wa utafiti, wengi wa wanaofanya wizi wa kutumia mihadarati, si wasimamao kando ya barabara, bali ni wenye vijiwe maalumu katika hoteli kubwa hasa kwenye huduma za kasino. “Dili zao si za fedha ndogo na wala hawalengi watu wa kipato cha kudunduliza. Hawaangalii sura wala mavazi ya wanayemlenga. Zaidi, wanapima ‘fungu’ la fedha wanazoweza kuiba na kuendeleza maisha yao,” alisema mmoja wa waliopata kukutwa na tukio la aina hiyo, ambaye hata hivyo alidai fedha zake hazikuibwa zote kwa kuwa alikabidhi sehemu kubwa kwa msimamizi wa kaunta katika hoteli aliyokwenda ‘kujirusha’ Dar es Salaam. Alidai kwamba aliingia chumbani na dola 1,000 za Marekani na baada ya kushituka usingizini ikiwa ni mchana wa siku ya pili, hakuzikuta wala kumwona binti aliyekuwa naye. “Ninachojua alivaa wigi refu na nguo za heshima. Anazungumza Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa na Kinyaturu. Alinibembeleza … nikafanya hivyo na sijui kulitokea nini kwani nilipoamka siku ya pili, sikumwona wala fedha zangu, lakini sikumweleza yeyote niliishia kulipa fedha ya chumba ya siku mbili,” alisema. Lakini, baadhi ya wafanyakazi wa kasino za Dar es Salaam walidai kwa nyakati tofauti kuwa wizi wa aina hiyo kwao si kitu kipya, kwa sababu ndio unaotumiwa na machangudoa wanaofahamika kwenye hoteli zao kila wakati. “Hivi unafikiri wanawake wote unaowaona kwenye kasino ni wafanyakazi au wacheza kamari kweli? Nenda kaunta utajionea mambo, kwa sababu wanakuja na Sh 3,000 tu za kadi za kuchezea kamari, halafu ‘wanatega mingo' (wanasubiri wateja) kwenye mashine za katikati, huku wakijinadi kwa kuzungusha macho na kubadili mitindo ya kusimama. “Wanawaliza sana Wazungu, wafanyabiashara wakubwa, mawaziri na watu wengine wenye umaarufu, wanaokuja kunywa bia na mvinyo kwenye kaunta za hoteli zetu. Na si unajua tena masharti ya humu? Yaliyotokea ndani ni ya ndani, hivyo tunakaa kimya tu na kuwashangaa,” alisema mfanyakazi wa kasino iliyo katikati ya Jiji la Dar es Salaam. Mfanyakazi mwingine wa kasino hiyo alisema aliukuta wizi wa aina hiyo katika kasino za Kampala, Uganda, lakini baadaye akaona ukiigwa na machangudoa wachache nchini na kuchukulia kuwa jambo la kawaida. “Sasa unatarajia nini, mtu kaacha mkewe au mumewe nyumbani na kuja kusaka changudoa kwenye kasino, acha aleweshwe, tena sasa hivi wanakoleza chuchu tu na kujizolea fedha. “Wengine bila aibu wanatutuma tuwashawishie wanawake hao na sisi tunafikisha ujumbe, kwa sababu tunaamini bila wao (machangudoa) biashara haichangamki na ukifuatilia kwa undani, utagundua kuwa hiyo ndiyo sababu inayofanya wasifukuzwe na uongozi wa kasino wanayoingia, licha ya kujulikana kuwa ni wezi,” alisema mfanyakazi huyo. Mikoa inayotajwa kuongoza kwa matukio ya aina hiyo ingawa hayajaripotiwa ni Mbeya hasa wilayani Kyela na Chunya, Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Mwanza, Singida na Arusha. Chanzo:Polisi yahadharisha wapenda ngono
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kwa wale wanao penda kunyonya chakula cha watoto kuweni makini dada zetu wanapakaza powder kwenye chuchu.
   
 3. Erotica

  Erotica JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 2,514
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wanaona aibu sabb inakuwa imeenda tofauti na malengo yao.

  The difference btn sex for mone and sex for free is that sex for mone costs less.
   
 4. Erotica

  Erotica JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 2,514
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kama lengo ni kulevya, atakulevya tu. na wanaume waacha ulumbukeni na ushamba.

  mwanamke cd unatumia ulimi? iwe mdomoni or wereva? kabla ya kuparamia fuatilien do's & dont's
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mi mbona mchumba angu aliniwekea kwenye uvinza, nilipo zama uvinza na kwenye tope nikalewa jumla hii nayo utasemaje?
   
 6. Erotica

  Erotica JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 2,514
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  samtimes SEX ni wazimu. kama ni mchumba yako yeye ndie anakuelewa,

  mebbe unfamfanyaga sana siku hio alitaka apumzike, na kukataa hawezi :-*
   
 7. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Haya kwa wale waliopitiliza ktk ufunguaji wa zipu nnadhani ujumbe umefika kwenu.
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  usicheze na midadi ikikupanda unakuwa mwendawazimu, mapenzi ni uchafu, ukichaa, wendawazimu yaani ukisisimuka ni balaa i see aliniweza siku hiyo nikaishia kuchezea mouse tu.
   
 9. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #9
  Jun 16, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mkuu hata mheshimiwa mmoja anapendaga hii chakula ya watoto, yakamkuta ya kumkuta huko 'jiji kasoro bahari'
   
 10. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #10
  Jun 16, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  well said, tatizo wengi huchukua cds baada ya kuwa bwii na hapo reasoning inakuwa poor,na cds wana take advantage, all in all dunia uwanja wa fujo na tutalizwa sana kama hatubadili tabia
   
 11. Erotica

  Erotica JF-Expert Member

  #11
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 2,514
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  teh teh teh. ww Fid unaonekana unakamia sana. na hupokei jibu la no. akaona bora

  akuwekee huko huko tena i bet yeye ali koj*** ndio faham zikakupotea. teh teh teh.

  hapo una haki ya kufungua kesi mahakamani.
   
 12. Erotica

  Erotica JF-Expert Member

  #12
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 2,514
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  kufanya hakukwepeki. ma cd wacha waendelee kutembelewa afta al ndio kula yao hio.

  ishu ni kufanya na cd kama vile ni galfie or wifey. wengine hata wanaowachukua kwenda

  kunywa kwanza pombe ndio wakadu. yupo kwa ajili ya biashara mnapotezeana tu mda hapo.

  kutaneni elewaneni pangeni bei fanyeni. kila mtu ashike zake, akatafute mteje mwengine ww kanye pombe zako.
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Jun 16, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hahahaha kweli mkuu ndo maana Polisi wametahadhalisha watu wanao tembelea maeneo hayo wajihadhari na mipododo
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Jun 16, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  hahaha CD ukiona anakubali umpapase paja au utomase tomase saratani stuka huyo yupo kikazi zaidi. CD ambaye yupo kwa ajiri ya kutoa ngono hapendi kupoteza muda ukifika unapata huduma yako fasta unachapa mwendo maana pale sio kwa mkeo
   
 15. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #15
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Haya wale wanaume wakware waje kusoma hii maneno fasta..............
  Mie simo kabisa..............
   
 16. Erotica

  Erotica JF-Expert Member

  #16
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 2,514
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Usinifanye nitoe siri.............:tape2::shut-mouth: rekebisha huo usemi wako.
   
 17. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #17
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Haya haya wale wapenda short time kazi kwenu, ila hii hapa A t huwa inawakutaga sana watu wanaoendaga pale shoprite(mrina)
   
 18. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #18
  Jun 16, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Tatizo la kuchanganya biashara na starehe wapi na wapi ila lazima watu
  wajifunze kwa
  hiyo kama hujaibiwa jifunze halafu utajua
   
 19. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #19
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Erotica soma PM yangu fasta, kabla hujafunguka hapa.........................
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Erotica

  Erotica JF-Expert Member

  #20
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 2,514
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0


  teh teh teh. babu sirudii tena. nimekoma!
   
Loading...