Polisi wazuia matembezi ya amani ya BAWACHA Dar es Salaam

Dr. Katabazi

Member
Joined
Sep 23, 2015
Posts
14
Reaction score
7
POLISI WAVURUGA MATEMBEZI YA AMANI...

Katika hali ya sintofahamu leo imetokea pale polisi walipovamia matembezi ya Amani yaliyokuwa yanaongozwa na Mama Regina Lowassa pamoja na Baraza la Wanawake la Chadema (BAWACHA) ingawa walikuwa na Vibali vyote...

Hali hiyo imetokea maeneo ya Mlimani City jijini dar -es -salaam ambapo matembezi hayo yalikuwa ndio yanaanzia..

Katika hali isiyoyakawaida polisi wamewakamata wakina mama wengine wakiwa na watoto wadogo,bila kujali na kuwapiga..katika hali hiyo wameamrisha matembezi hayo yasifanyike ingawa vibali vyote vilikwisha patikana..

Kama taifa tunakwenda wapi? baadhi ya watu waliokuwa pembeni walisikika wakisema wameamua kuzuia matembezi hayo kwa sababu chama cha mapinduzi kilikuwa na lengo kama hilo hivyo inawezekana wametoa shinikizo kwa polisi ili kuzuia makusudi waweze kufanikisha ya kwao..Kiukweli hakuna HAKI hapo..

Polisi Tanzania msikubali kutumika kisiasa..simamieni haki na mdumishe amani...

Na Mtanzanzania mwema
Ilikuwa ni katika mkutano wa matembezi ya amani maeneo ya mlimani city hapa dsm. Mama Lowasa alikuwa na kundi kubwa la wanawake zaidi ya 100 ambao walikiwa na mkutano mfupi na kisha matembezi ya amani. Polisi walivamia na kuzuia kila kitu na kuwakamata wanawake kadhaa na kuwaweka ndani. Muda huu mama Lowasa anashughulikia kuwatoa.

View attachment 297052
Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam wamezuia mkutano wa Mke wa mgombea urais kupitia CHADEMA,Mama Regina Lowassa pamoja na baraza la wanawake chadema (BAWACHA) Ambao ulipaswa kuanza na matembezi ya amani kuliombea taifa amani.

msemaji anasema mkutano huo ulikua halali na walipewa kibali cha kuufanya siku ya leo lakini ghafla leo asubuhi kamanda mkuu wa kanda ya dar es salaam ,Kamanda Kova alifikia mahali hapo akiwa na vijana wake na kutoa amri ya kuzuia mkutano huo pasipo kua na maelezo ya kutosha zaidi.hali iliopelekea kutoeleweka hivyo kuleta mabishano na baadhi ya wajumbe wa BAWACHA hivyo kuwakamata akiwemo mwenyekiti wa baraza hilo.

Matembezi hayo, yalipangwa Kuanzia mlimani city majira ya saa tatu asubuhi na kupita katika mitaa mbalimbali ya jiji la dar es salaam na kuhitimisha katika viwanja vya Tanganyika packers Kawe ikifatiwa na maombi rasmi ya kuliombea taifa letu.

Mgeni rasmi ni mke wa mgombea urais wa CHADEMA kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mama Regina Lowassa akifuatana na mwenyekiti baraza la wanawake taifa, Mh Halima Mdee pamoja na Viongozi mbalimbali.

Mada ilipangwa kutatolewa na Legal and human right center.
Bawacha-620x308.jpg

Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee akitoka kuwatoa wanawake wa Bawacha waliokuwa wanashikiliwa na polisi Mabatini, Kijitonyama​

JESHI la Polisi limevamia na kuvuruga maandamano ya amani ambayo yaliandaliwa na Baraza la wanawake Chadema (BAWACHA), licha ya kupewa taarifa siku tatu kabla juu ya kufanyika kwa mkutano huo. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Aidha, mkutano huo uliovurugwa ulitakiwa uanzie maeneo ya Mlimani city Mwenge hadi Uwanja wa Tanganyika Packers Kawe ambapo Mke wa Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Edward Lowassa alitakiwa kuongea na wanawake wote wa Dar es Salaam.

​

Akizungumzia tukio hilo la uvamizi, Katibu Mkuu wa Bawacha Grace Tendega amesema wamesikitishwa na tukio hilo kwani uongozi wa Chama hicho ulitoa taarifa mapema na kwamba walishaulipia uwanja huo.

Tendega anasema, lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuwasha mishumaa ya amani wakiongozwa na Mama Lowassa ambapo alipanga kuzungumza na kinamama juu ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu kwani yakitokea machafuko kinamama ndio waathirika wakuu.

‘Kisheria barua inatakiwa kujibiwa ndani ya masaa 24 lakini cha ajabu hatukujibiwa ndani ya siku tatu baada ya sisi kuanza maandamano ndo ametuletea barua ya kuzuia maandamano yetu licha ya kujitetea kuwa maandamano yetu yalikuwa ya amani'.

Amesema, barua waliyoipokea leo kutoka Makao makuu ya Polisi iliwakataza kufanya maandamano wala mkutano wowote kwa kile alichodai kuwa njia walizokuwa wamepanga kupita wangesababisha vurugu na uvunjifu wa amani.

Weka picha za waliopigwa, acheni uzushi usio na maana. Jitu kubwa umekalisha makengere yako na kuanza kuandika upumbavu nanga ww
 
POLISI WAVURUGA MATEMBEZI YA AMANI...

Katika hali ya sintofahamu leo imetokea pale polisi walipovamia matembezi ya Amani yaliyokuwa yanaongozwa na Mama Regina Lowassa pamoja na Baraza la Wanawake la Chadema (BAWACHA) ingawa walikuwa na Vibali vyote...

Hali hiyo imetokea maeneo ya Mlimani City jijini dar -es -salaam ambapo matembezi hayo yalikuwa ndio yanaanzia..

Katika hali isiyoyakawaida polisi wamewakamata wakina mama wengine wakiwa na watoto wadogo,bila kujali na kuwapiga..katika hali hiyo wameamrisha matembezi hayo yasifanyike ingawa vibali vyote vilikwisha patikana..

Kama taifa tunakwenda wapi? baadhi ya watu waliokuwa pembeni walisikika wakisema wameamua kuzuia matembezi hayo kwa sababu chama cha mapinduzi (CCM)kilikuwa na lengo kama hilo hivyo inawezekana wametoa shinikizo kwa polisi ili kuzuia makusudi waweze kufanikisha ya kwao Hivyo moja kwa moja CCM watakuwa wametoa shinikizo hilo...Kiukweli hakuna HAKI hapo..

Wakina mama wamedhalikishwa,walemavu pia wamenyanyaswa..Hivi kweli wakina Mama wanaweza kuvuruga Amani kwa matembezi tena yenye lengo la Kuombea nchi amani

Polisi Tanzania msikubali kutumika kisiasa..simamieni haki na mdumishe amani...

Na Mtanzanzania mwema
 
Mwisho wao 25/10/2015. Na lazima kila mtu atajibu kwa nafasi yake. Hakuna cha nilitumwa na sijui Prof. wa Kichina sijui nani vile!!!
 
Ilikuwa ni katika mkutano wa matembezi ya amani maeneo ya mlimani city hapa dsm. Mama Lowasa alikuwa na kundi kubwa la wanawake zaidi ya 100 ambao walikiwa na mkutano mfupi na kisha matembezi ya amani. Polisi walivamia na kuzuia kila kitu na kuwakamata wanawake kadhaa na kuwaweka ndani. Muda huu mama Lowasa anashughulikia kuwatoa.
 
Ilikuwa ni katika mkutano wa matembezi ya amani maeneo ya mlimani city hapa dsm. Mama Lowasa alikuwa na kundi kubwa la wanawake zaidi ya 100 ambao walikiwa na mkutano mfupi na kisha matembezi ya amani. Polisi walivamia na kuzuia kila kitu na kuwakamata wanawake kadhaa na kuwaweka ndani. Muda huu mama Lowasa anashughulikia kuwatoa.

kisa cha kuwakamata ni nini sasa..??!
 
Asanteni mapolisi kwa kuwapa promo ukawa bila kujua this time Ohh job you have haaa
 
POLISI WAVURUGA MATEMBEZI YA AMANI...

Katika hali ya sintofahamu leo imetokea pale polisi walipovamia matembezi ya Amani yaliyokuwa yanaongozwa na Mama Regina Lowassa pamoja na Baraza la Wanawake la Chadema (BAWACHA) ingawa walikuwa na Vibali vyote...

Hali hiyo imetokea maeneo ya Mlimani City jijini dar -es -salaam ambapo matembezi hayo yalikuwa ndio yanaanzia..

Katika hali isiyoyakawaida polisi wamewakamata wakina mama wengine wakiwa na watoto wadogo,bila kujali na kuwapiga..katika hali hiyo wameamrisha matembezi hayo yasifanyike ingawa vibali vyote vilikwisha patikana..

Kama taifa tunakwenda wapi? baadhi ya watu waliokuwa pembeni walisikika wakisema wameamua kuzuia matembezi hayo kwa sababu chama cha mapinduzi (CCM)kilikuwa na lengo kama hilo hivyo inawezekana wametoa shinikizo kwa polisi ili kuzuia makusudi waweze kufanikisha ya kwao Hivyo moja kwa moja CCM watakuwa wametoa shinikizo hilo...Kiukweli hakuna HAKI hapo..

Wakina mama wamedhalikishwa,walemavu pia wamenyanyaswa..Hivi kweli wakina Mama wanaweza kuvuruga Amani kwa matembezi tena yenye lengo la Kuombea nchi amani

Polisi Tanzania msikubali kutumika kisiasa..simamieni haki na mdumishe amani...

Na Mtanzanzania mwema

Kama wana bibali vyote, kisa cha kuwazuia ni nini?
 
Back
Top Bottom