Elias Msuya
Senior Member
- Dec 23, 2011
- 173
- 671
Wakati kesi za Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu zikiendelea leo katika Mahakama ya Haki Mkazi Kisutu Dar es Salaam, askari wa Jeshi la Polisi wakiwa kwenye magari manne wamezingira nyumbani kwake kinachoelezwa kuwa wanataka kufanya upekuzi.
Lissu aliyekamatwa Aprili 12, 2025 wilayani Mbinga Mkoa wa Ruvuma, alipendishwa kizimbani katika Mahakama ya Gakimu MKazi Kisutu Dar es Salaam, akikabiliwa na mashitaka ya Uhaini na Kuchapisha taarifa za uongo.
Akizungumza na JamiiForums leo Aprili 28, 2025 saa 4:04 asubuhi, Mkurugenzi wa Uenezi na Mawasiliano wa Chadema, Brenda Rupia amesema polisi hao wanataka kufanya upekuzi nyumbani kwa Lissu.
“Bado wapo hapo, hawasemi wanataka nini zaidi, maana kama angekuwepo Mwenyekiti (Lissu), tungesema ni house arrest (kukamatiwa nyumbani). “Tumewaomba vibali vya upekuzi, hawana,” amesema.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alipoulizwa sababu ya askari hao kufika mahali hapo, amesema ni ulinzi wa kawaida.
“Sisi tumeweka ulinzi wa kawaida, sasa hao wanaosema tunafanya upekuzi waulize askari wameonyesha searching order au searching warrant? Maana kabla hujauliza kibali cha Mahakama kwa nini usiulize kibali cha polisi?” amehoji Muliro.
Ameongeza, “Waulize wenye nyumba sio viongozi wa Chadema. Inawezekana wameona watu wanapitapita wakawaita polisi. Sisi tunafanya ulinzi kwa watu wote, sio chama iwe ni Chadema, ACT Wazalendo au chama chochote.”
Akizungumzia ujio wa polisi hao, msaidizi wa Lissu, David Djumbe amesema awali walifika alfajiri wakiwa na magari manne na kuanza kugonga geti, lakini hawakufunguliwa.
“Baadaye walikwenda kwa mjumbe wa shina ambaye aliwapigia simu wanafamilia akisema polisi hao wamekuja hapo kufanya upeukuzi, ndipo akaambiwa mwenye nyumba (Lissu) hayupo hawawezi kuwafungulia,” amesema.
Djumbe amesema ndugu waliopo nyumbani hapo wameshindwa kutoka kwenda kwenye shughuli zao kwa kuwa nyumba imezingirwa.