Polisi wavunja mkutano wa CHADEMA Dodoma

NGOWILE

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
454
258
Polisi mkoani DODOMA leo wamebatilisha kibali cha kufanya mkutano wa hadhara wa chama cha democrasia na maendeleo-CHADEMA.Mkutano huo ulikuwa ufanyike katika kata ya Chang'ombe eneo la standi kwa madhumuni ya kujenga na kukiimarisha chama katika kata hiyo.Mkutano huu ulikuwa ufanyike wiki iliyopita lakini ikashindikana kutokana na CCM kuwa na mkutano siku hiyo katika kiwanja hicho ndipo polisi waliwataka CHADEMA kuchagua siku nyingine ambapo CHADEMA walikubaliana na polisi kufanya mkutano huo siku ya leo.Kisheria polisi wanatakiwa kubatilisha kibali cha mkutano saa arobaini na nane kabla ya mkutano.Hakukuwa na sababu za msingi kutoka polisi.Licha ya mkutano kuvunjwa wakazi wa kata hii ya chang'ombe walikuwa na shauku kubwa ya kuwasikiliza viongozi wa CHADEMA kwani walimiminika kwa wingi kitu ambacho sio cha kawaida kwa mkoa wa DODOMA kwani ni ngome kubwa ya CCM.Kimsingi hii ni njia ya kukadhamiza democrasia kwa vyama vya upinzani kwa kukilinda chama Tawala CCM.Naomba kuwasilisha.source nipo DODOMA.
 
ni vyema awa vibaraka wa mafisadi wakorodheshwa ili siku na saa ya ukombozi itakapotimia wajibu mashitaka kwa kukwida demokrasia
 
Poleni sana hii naona inajitokeza sana Dodoma mara kwa mara kwa polisi kuzuia mikutano ya CDM, msivunjike moyo kazeni buti.
 
Hao polisi ndiyo wananyanyaswa na ccm lakini bado wanatumiwa na haohao. Wamekuwa kama misukule wasiotumia utashi binafsi na kusoma alama za nyakati. Cdm msikate tamaa, watabana weee wataachia tu!
 
Jeshi la polisi la Tanzania si rafiki tena wala salama wa maisha na mali za Watanzania.
 
Mbunge wa Dodoma mjini alifanya njama hizo kwani jmosi iliyopita alikuwa chang'ombe, anaogopa Chadema watamuumbua kwa kuweka vilaka vya udongo kwenye barabara za lami za hapa mjini.
 
Wanajisumbua tu!hawawezi kuzuia nguvu na fikra pevu za vijana wa sasa watakao mabadiliko!hata hao polisi wengi wao hawana mapenzi na magamba,ilo liko wazi,sema wanatii amri za wakuu wao!
 
Kamanda Ahsante kwa taarifa! Lakini ni vyema CCM wakajua kwamba hujuma wanazowafanyia CDM kupitia polisi zina mwisho wake ambao ni 2015, sisi wanamageuzi hatuta kubali hujuma kama hizi ziendelee huku zikizalilisha haki za wananchi, so hata kama 2015 polisi watajaribu kuibebeba CCM basi na sisi umma 2taamua kuibeba CDM na ambapo ktk hili polisi hawataweza kushinda umma kwani hata hiyo polisi imetokana na umma, DON GVUP CHADEMA"
 
Je sheria inasemaje ikiwa chama kimeingia hasara kwa kugharamia mkutano na ghafla ukavunjwa kinyume na masaa yaliyoandikwa? Je ipo fidia yeyote? Maana hii ni hasara, viongozi wametoka mbali then last minute una cancell mkutano...
 
Nashauri kwa mazingira kama haya ni bora kufanya mikutano ya ndani nayo inatoa matunda mazuri tu
 
Hofu za CCM hizo ila wajue kichapo kinawasubiri pale Arumeru na hii itakuwa hatua ya awali ya kuwanyanganya tonge mdomoni. Hawa polisi sijui watawaambia ni ni CDM 2015 na sijajua wataanzia wapi kujifanya wanamlinda rais kutoka CDM kwani inatakiwa safu nzima ya maaafisa yaani RPCs, OCDs wafutwe warudi nyumbani ianzishwe safu mpya ya watu committed
 
Nadhani wana-CHADEMA tuunge nguvu zetu na sisi tufanye operesheni ONDOA NA FAGIA CCM MKOA WA DODOMA...Nadhani itakuwa njema sana...kwanini Dodoma iwe ngome na pango la wanyang'anyi
 
Polisi mkoani DODOMA leo wamebatilisha kibali cha kufanya mkutano wa hadhara wa chama cha democrasia na maendeleo-CHADEMA.Mkutano huo ulikuwa ufanyike katika kata ya Chang'ombe eneo la standi kwa madhumuni ya kujenga na kukiimarisha chama katika kata hiyo.Mkutano huu ulikuwa ufanyike wiki iliyopita lakini ikashindikana kutokana na CCM kuwa na mkutano siku hiyo katika kiwanja hicho ndipo polisi waliwataka CHADEMA kuchagua siku nyingine ambapo CHADEMA walikubaliana na polisi kufanya mkutano huo siku ya leo.Kisheria polisi wanatakiwa kubatilisha kibali cha mkutano saa arobaini na nane kabla ya mkutano.Hakukuwa na sababu za msingi kutoka polisi.Licha ya mkutano kuvunjwa wakazi wa kata hii ya chang'ombe walikuwa na shauku kubwa ya kuwasikiliza viongozi wa CHADEMA kwani walimiminika kwa wingi kitu ambacho sio cha kawaida kwa mkoa wa DODOMA kwani ni ngome kubwa ya CCM.Kimsingi hii ni njia ya kukadhamiza democrasia kwa vyama vya upinzani kwa kukilinda chama Tawala CCM.Naomba kuwasilisha.source nipo DODOMA.
Mpaka lini..tena
 
Hao polisi ndiyo wananyanyaswa na ccm lakini bado wanatumiwa na haohao. Wamekuwa kama misukule wasiotumia utashi binafsi na kusoma alama za nyakati. Cdm msikate tamaa, watabana weee wataachia tu!

wananyanyaswa na ccm lakini wanafaidika kwa kupokea rushwa na kunyanyasa na kuua raia wasio na hatia,.they will pay heavy price, woe to them!!
 
CDM wasichoke. Wataalam wa PR wanajua kuwa hizi actions za Polisi zinaongezea umaarufu zaidi CDM kuliko kuuondoa. CDM waombe kibali tena na tena iwe ndiyo normal kwani hasira za wananchi dhidi ya polisi kuwanyika haki ya kuisikiliza CDM inakuwa Channeled to CCM.

Ila kama CDM wataacha kuomba kibali na kupublish kwa wananchi watasahaulika. Ni good move kwani inajenga chama kwa kutumia nguvu ndogo sana. Wananchi wakiwasikiliza CDM kila siku katika mikutano itafikia mahali watawaona hawana jipya na kuwachoka ila wanapozuiwa na polisi ni positive issue kwa CDM kwani wananchi watakuwa na shauku na mapenzi makubwa na CDM. Tusiwalalamikie sana polisi, tufurahi kwani wanaijenga CDM zaidi ya CCM kwa vitendo vyao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom