Polisi wavamia nyumbani kwa Diamond usiku!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,295
33,079


Diamond Platnumz


IMELDA MTEMA NA GABRIEL NG’OSHA

DAR ES SALAAM: Polisi wenye silaha hivi karibuni wali ka nyumbani kwa msanii nyota, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anayeishi Mivumoni Madale na kusitisha shughuli za burudani zilizokuwa zikiendelea ndani, Risasi Mchanganyiko limedokezwa.

Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, shughuli iliyositishwa na polisi ilikuwa ni ile ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mama mzazi wa mkali huyo wa muziki, Sanura Kassim ‘Sandra’ iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Ilidaiwa kwamba msanii huyo amekuwa akifanya sherehe mara kwa mara katika nyumba yake hiyo, hali inayosababisha kero kwa baadhi ya majirani zake, ambao nao, wamekuwa wakilalamika mara kwa mara kwa viongozi wa serikali ya mtaa huo.



Nyumbani kwa Diamond Platnumz


Gazeti hili baada ya kuupata ubuyu huo, lilifunga safari hadi nyumbani kwa msanii huyo na ku kia ofisini kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mivumoni, Deodatus Kamugisha ambaye baada ya kuulizwa kuhusu kuwepo kwa tukio hilo la askari kuzima sherehe hiyo, alikiri kuwa ni kweli.

“Nimekuwa nikipata malalamiko ya mara kwa mara kuhusu sherehe za Diamond kuwa waalikwa wake ni vijana wa kihuni ambao wakija huwa wanavuta bangi hadharani, wanafunga barabara pamoja na kujisaidia haja ndogo hovyohovyo maeneo ya nje ya nyumba yake.



Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mivumoni, Deodatus Kamugisha.


“Juzi nilipigiwa simu usiku na majirani zaidi ya sita wakila lamika kuhusu sauti kubwa ya muziki wa kwenye sherehe ya Diamond, nilimuita lakini akakaidi, ikabidi niende Kituo cha Polisi cha Wazo na kuchukua polisi wakiwa na silaha na kwenda kufunga sherehe ile, sheria iko wazi kuhusu utaratibu wa kupiga muziki maeneo ya baa na majumbani,” alisema Kamugisha.

Baadhi ya majirani waliozungumza na gazeti hili, walisema kumekuwa na tabia ya Diamond kufanya sherehe mara kwa mara nyumbani hapo, huku muziki mkubwa ukipigwa, jambo ambalo kwao ni kero.

“Nachukizwa sana na kelele za Diamond, kwani watu tunashindwa kulala kwa sababu yeye anafanya sherehe mbona kuna kumbi na hoteli anaweza kwenda tu, mimi nyumba yangu ni kama kilomita mbili kutoka kwake, lakini nasikia muziki kwa kero, je walio ubavuni mwake si wanataabika sana!” alisema mzee mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Gazeti hili lilimtafuta Diamond kwa simu yake mkononi ili kuzungumzia ishu hiyo lakini iliita bila kupokelewa kwa muda wote. chanzo.Polisi wavamia nyumbani kwa Diamond usiku!
 

Attachments

  • Diamond-Platnumz.png
    Diamond-Platnumz.png
    88.5 KB · Views: 96
  • mwenyekiti WA SERIKALI YA  MTAA.jpg
    mwenyekiti WA SERIKALI YA MTAA.jpg
    19.9 KB · Views: 88
  • NYUMBA YA DIAMOND.png
    NYUMBA YA DIAMOND.png
    90.1 KB · Views: 345
Tena! Huyu diamond si alikua kapuku mwenzao? Maana kipindi cha kampeni nilimsikia akiimba "ccm mbele kwa mbelee".

Umekosa la kuandika unaleta ya siasa, na wewe yakitokea mtaani kwako kila mtu atakuwa sabbau anavutiwa na chama fulani....mmmmmmm

Na bado ataendelea kuimba chochote kile...yeye umuhimu pesa anaingiza...
 
Umekosa la kuandika unaleta ya siasa, na wewe yakitokea mtaani kwako kila mtu atakuwa sabbau anavutiwa na chama fulani....mmmmmmm

Na bado ataendelea kuimba chochote kile...yeye umuhimu pesa anaingiza...
Mbona povu tena jamani! Au nimegusa penyewe nini?
 
Kazoe makelele huyo,nakumbuka kuna kipindi miaka ya tisini kama sikosei,nilipendelea kwenda baa moja mtaa wa congo k'koo,ilikuwa ikisifika kwa utamu wa chips ja kuku ikiitwa congo bar,huyo mtoto alikuwa anaimba nje ya nyumba jirani ma baa hiyo,tulikuwa tukimpa soda,sasa juzi kuna rafiki yangu ndio akanikumbusha kuhusu yeye amekuwa maarufu huko.
 
Back
Top Bottom