Polisi wavamia gari la kampuni ya Mafuta Tanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wavamia gari la kampuni ya Mafuta Tanga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Alnadaby, Feb 20, 2009.

 1. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Katika hali isiyokuwa ya kawaida RTO 9 Kamanda wa Usalama wa barabarani mkoani Tanga akifuatana na askari wake wanne walimvamia Meneja wa kampuni ya mafuta ya GBP wakampiga hadi akazimia.

  Meneja huyo kwa jina la Amour aliyekuwa akitoka kituo cha mafuta cha Airport eneo la Kange alisimishwa alipokuwa akielekea Makorora na kutolewa kwenye gari na kupigwa hadi akazimia.nadni ya gari kulikuwa kuna pesa za mauzo za kituo cha GBP Airport.

  Baada ya kutafutwa na Mwajiri wake bila kupatikana kwa kuwa simu zake zilikuwa tayari zipo mikononi mwa askari hao na zimezimwa,mwajiri alianza kazi ya kumtafuta Meneja wake na aliwasiliana na Mkubwa mmoja na kazi ikaanza mara moja.

  Mkubwa akawa anampigia simu RTO lakini RTO alikuwa hazipokei.

  Baada ya masaa kadhaa RTO na askari wake wakamfikisha meneja yule akiwa hoi kwa kupigwa hadi kituo cha Mabawa.

  Habari zaidi zitafuata.
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,798
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  ..continue plz
   
 3. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Malizia hiyo habari ili tuichangie mkuu........!
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Sasa mkiambiwa nchi inaendeshwa kienyeji mnapiga makelele .watasema walifikia mwizi.
   
 5. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Yale yale ya kesi ya mauaji ya wafanyabiashara 3 na taxi driver. Wataandika maelezo kuwa alikuwa mwizi. Naamini kipigo hicho hakitamwondoa uhai na ataweza kuweka ushahidi bayana. System zote za usalama wa raia na nchi Tz zinayumba kwa sasa. Shame!
   
 6. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kuna coe of conduct ya polisi kufanya kazi zao. Kama huo jamaa alikuwa anapinga kukamatwa, au kama alikuwa alikuwa anatumia nguvu dhidi ya polisi au kama alifanya lolote kinyume na hali ya kawaida(na ushahidi ukaonekana wazi), basi polisi walikuwa na haki ya kuchukua hatua zinazotakiwa kukabaliana na jamaa huyo.
  Lakini mkuu inabidi utoe habari kamili kuhusu mazingira ya tukio ili ijulikane sababu ya polisi kufanya hivyo.
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  nasikia huyo jamaa alikuwa na mre than 20mil za mauzo kwenmye land cruiser yake, na sasa hazionekani na hao trafiki wanasema hawakukuta fedha kwenye gari wakati wanamkamata.
  Wanachosema trafiki ni kuwa walimsimamisha jamaa hakusimama na wakaamua kufukuzana naye hadi mjini ndipo wakamkamata. hawajatoa maelezo kwa nini waliamua kumnyang'anya gari na kumpa kichapo.
   
 8. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #8
  Feb 21, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa taarrifa ilivyo sasa ni ya kusikitisha tu, kwani ASKARI WATANO ni wazi kuwa wangemudu kumtia huyo mtuhumiwa nugvuni bila kipigo. hata kama angeleta ubishi, kwa mafunzo ya kipolisi Askari watano ni wengi sana dhidi ya mtu mmoja.Tunasubiri habari kamili.
   
 9. Kocha

  Kocha JF-Expert Member

  #9
  Feb 21, 2009
  Joined: Mar 2, 2008
  Messages: 375
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Tatizo la polisi wengi wa tz ni kwamba hawana ufahamu wa sheria hata zile za msingi pia wengi ni wahuni kazi yao ni kubangikia watu makosa,mifano iko mingi sana
   
 10. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #10
  Feb 21, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Habari za kuaminika ni kuwa Kamanda na askari wake walikuwa wamelewa.Pili walipekua gari lake in and out na kumpiga hadi akazimia.

  Aliyebondwa ni mtu mpole na asingeweza kuwachokoza askari hao.Inaaminika walijua kuwa anatoka Petrol Station akiwa na fedha za mauzo.Walimzinga na kumpiga sana wakazunguka naye masaa kadhaa bila kumfikisha kituoni.

  Habari za ndani kabisa ni kuwa RTO anamwagukia Siro(RPC) amuondoe katika orodha ya watuhumiwa kwa kuwa ana umri wa kustaafu hivi karibuni.Lakini hii imeshafika kwa IGP na moto unaanza kuwawakia.

  Police brutality katika Tz ni jambo la kawaida.Wengi wanajiona kama wako above the law.
   
 11. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #11
  Feb 21, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna haja ya KUBORESHA Vyuo vya POLISI pamoja na ELIMU YA KAZI wanayofanya. Sijui kama itawezekana katika WIMBI HILI LA UFISADI ULIOKITHIRI>
   
 12. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #12
  Feb 21, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Malipo kiduchu kwa wasitaafu ndio chanzo cha ufisadi ndani ya jeshi la police Huyu RTO inaonekana hajajiandalia maisha vizuri na kaamua kutumia huo mwanya ili kupata cha kuanzia baada ya kusitaafu.
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Feb 21, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Na sasa atastaafu kwa moto
   
Loading...