Polisi wavamia eneo la Kimbangulile muda huu..

Friday Malafyale

JF-Expert Member
Jan 18, 2017
1,808
2,911
Muda huu Polisi Wakiwa na Difenda mbili za Polisi wamevamia eneo hili wakiwa na silaha za moto.

Hali ilikuwaje?


Nilikuwa napita mitaa hii kwenda maeneo ya Rangi tatu basi zikatokea hizo difenda moja ikapaki juu msikitini nyingine ikashuka chini ikiwa na Askari wawili wenye mashine na mwanamke mmoja alovaa Dera hivii kukiwa na raia alopigwa pingu kwa nyuma akiwa na askari.

Ghafla wakashuka wakaingia kwenye nyumba moja ambayo iko karibu na mashine hizi za kusaga na kukoboa.

Na mlangoni kulikuwa na fuso kukiwa na vijana wakipakiza mifuko ya Nilon ikidhaniwa ni unga ama mchele kama sikosei, basi wakaingia ndani kwa nguvu huku wakifoka sana.

Wakakaa kama nusu saa nzima ndani baadae wakaamua kutoka ila picha za gari ya polisi nilipiga kiwizi sana kitu ambacho ni ngumu kugundulika.

Basi nikasikia wadada wa hapa wakisemezana kwamba ningekuwa mimi ningemchamba mbona wanamchongea mwenzao mbona wana wivu sana jamani?

Nikawa nasikiliza tuu kama sina mpango vile, ila kwa ninavyohisi ni kama mali ya ukwepaji kodi ama magendo japo sina hakika.

Mwisho askari wengine wakapanda Fuso na wengine wakaondoka wakiwa kwenye difenda zao.

1d6fba3db71f71952c870bffc4fa473d.jpg


c30caaf497714c36d4ad77a200fee8b3.jpg


Mwafwaaa
 
mazoea yetu hayana makosa,
hii inaitwa ''comon mistake''
yani gari zoote za polisi zitaitwa defender


Kama ilivyokuwa wakati wa maombolezo ya Mwl Nyerere, kila TV set zote na TV stations zilikuwa zinaitwa ITV
 
Nilijua ndo wameenda kumkamata mwenyekiti wa Yebo FC,na hilo fuso limebeba bwimbwi anahamishia jangwani chimbo!..
 
Back
Top Bottom