Polisi waua majambazi watatu Dar es Salaam

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
42,302
Likes
37,954
Points
280

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
42,302 37,954 280
POLISI jijini Dar es Salaam wamewaua majambazi watatu katika mapambano ya kurushiana risasi yaliyodumu takribani dakika 45.

Tukio hilo lilitokea juzi saa 3.30 usiku katika makutano ya barabara za Kawawa na Nyerere, baada ya majambazi hao kumvamia mfanyabiashara, Shiv Kumar (27) ambaye ni Meneja wa Kampuni ya NAS Hauliers.

Akizungumzia tukio hilo jana, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema majambazi hao waliokuwa wakitumia gari namba T 651 AWW walimvamia mfanyabiashara huyo mwenye asili ya Kiasia aliyekuwa akiendesha gari namba T 136 AQT aina ya Toyota Rav4 na kumzuia kwa mbele.

“Baada ya kumzuia, majambazi hao walitoka ndani ya gari lao na kutoa bastola na kumfyatulia risasi mfanyabiashara huyo iliyompata katika bega la kushoto na ubavuni, lengo likiwa ni kumpora fedha na gari hilo,” alisema Kova.

Alisema kutokana na msongamano wa magari na wingi wa watu sehemu ya tukio hilo, majambazi hao walishindwa kupora na badala yake walikimbia na gari lao kuelekea Magomeni/Kigogo kupitia Barabara ya Kawawa.

Kamanda Kova aliwataja majambazi hao kuwa ni Sudi Kazi (35) wa Manzese ambaye alikuwa dereva wa gari lao, na wengine waliotambulika kwa jina moja moja; Athuman mkazi wa Magomeni na Mwakibinga wa Kimara.

“Taarifa za tukio hilo zilifika Polisi na ufuatiliaji wa kukamata majambazi hao ulianza mara moja na ilipofika saa 4 usiku, polisi wa kitengo cha CTR waliokuwa doria eneo la Mabibo, wakitumia gari namba PT 1447 Toyota Land Cruiser, walilitilia shaka gari la majambazi hao na kulifuatilia,” alisema.

Kova alisema majambazi hao walipogundua kuwa wanafuatiliwa waliongeza mwendo kuelekea Barabara ya Morogoro huku polisi wakizidi kulifuatilia na walipokaribia Magomeni Kagera, majambazi waliwafyatulia risasi polisi.

“Polisi walijibu mapigo kwa kufyatua risasi na kupiga matairi ya gari la majambazi na kuserereka na kupinduka na kutumbukia mtaroni na majambazi hao kujaribu kutoroka huku wakiendelea kuwamiminia polisi risasi,” alisema.

Alieleza kuwa wakati wakiendelea kurusha risasi, askari walilizingira gari la majambazi na kuwadhibiti na kuwapa kipigo kikali ndipo walipogundua kuwa dereva wa gari hilo, Sudi, alikuwa amekatika mguu wa kulia kutokana na purukushani hizo.

Hata hivyo, majambazi wawili walitoka ndani ya gari wakiwa na bastola na kuwarushia risasi polisi ambapo askari mmoja, Koplo Hassan aliyekuwa akiendesha gari la Polisi alijeruhiwa mguu wa kulia na polisi wengine wakaendelea na mapambano na kuwazidi nguvu majambazi kwa kuwajeruhi.

Katika upekuzi uliofanyika, polisi walikamata silaha nne; bastola aina ya Glock namba HZM 326 Cal. 9 mm ikiwa na risasi nane, bastola aina ya Browning namba A. 279149 Cal. 7.65mm, Revolver namba CK73716 ikiwa na risasi mbili na bunduki aina ya Rifle MarkIV ikiwa na risasi tisa na kibao cha namba ya gari T 254 BBP ambazo zinaonesha kuwa namba halisi za gari hilo ambalo lilikuwa limebandikwa namba bandia T 651 AWW.

Kamanda alisema kutokana na hali za majambazi hao kuwa mbaya walipelekwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya matibabu, lakini walifikishwa hapo wakiwa wamekufa na miili yao kuhifadhiwa katika hospitali hiyo.

Koplo Hassan akitibiwa katika hospitali ya Polisi Baracks na baadaye kuruhusiwa na hali yake inaendelea vizuri.

Shiv alitibiwa katika Hospitali ya Aga Khan, alifanyiwa upasuaji mkubwa na kutolewa risasi mwilini na hali yake pia inaendelea vizuri.

“Msako mkali uliendelea usiku kucha kwa lengo la kuwapata washiriki wote wa kundi hilo la majambazi na kuwakamata wengine wawili ambao ni Obed Mwakasenga ‘Mwenyekiti’ (35) na Ally Rajab (27) na tunawahoji,” alisema Kova.

Katika hatua nyingine, Kova aliwapongeza askari sita akiwamo mwanamke ambaye alipambana na majambazi hao uso kwa uso.

Askari hao ni Koplo Hassan, Koplo Lucas, Konstebo Anold, Konstebo Ivan, Konstebo Musa na Konstebo Mwachumu na aliwapa kifuta jasho cha Sh 300,000.
 
source: habari leo
 
PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Messages
16,232
Likes
331
Points
180

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2009
16,232 331 180
KAZI NZURI SANA...lAKINI HII ISHU YA KUKIMBILIA KUTANGAZA KWENYE MEDIA KILA HATUA YA TUKIO LA KIPOLISI NAONA INASHUSHA EFFICIENCY YA KUWAKAMATA HAWA WALIOBAKI.
 
Jayfour_King

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2009
Messages
1,141
Likes
12
Points
0

Jayfour_King

JF-Expert Member
Joined Nov 15, 2009
1,141 12 0
"Taarifa za tukio hilo zilifika Polisi na ufuatiliaji wa kukamata majambazi hao ulianza mara moja na ilipofika saa 4 usiku, polisi wa kitengo cha CTR waliokuwa doria eneo la Mabibo, wakitumia gari namba PT 1447 Toyota Land Cruiser, walilitilia shaka gari la majambazi hao na kulifuatilia," alisema.

Taarifa haionyeshi kwamba tukio lilianza saa ngapi, ki habari huu ni utata. Huwezi kueleza muda katikati ya tukio bila kutaja mwanzo wa tukio kiufundi haileti maana, ila kazi nzuri hongera Kova na vijana wako.
 
Tiba

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2008
Messages
4,520
Likes
114
Points
160

Tiba

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2008
4,520 114 160
“Taarifa za tukio hilo zilifika Polisi na ufuatiliaji wa kukamata majambazi hao ulianza mara moja na ilipofika saa 4 usiku, polisi wa kitengo cha CTR waliokuwa doria eneo la Mabibo, wakitumia gari namba PT 1447 Toyota Land Cruiser, walilitilia shaka gari la majambazi hao na kulifuatilia,” alisema.

Taarifa haionyeshi kwamba tukio lilianza saa ngapi, ki habari huu ni utata. Huwezi kueleza muda katikati ya tukio bila kutaja mwanzo wa tukio kiufundi haileti maana, ila kazi nzuri hongera Kova na vijana wako.
Mkuu King,

Nafikiri kila kitu kiko wazi. Imeelezwa kuwa tukio la kumpiga risasi meneja wa NAS lilitokea saa 3.30 na polisi walianza kufuatilia saa 4.00. Sioni utata wa habari huko wapi hapa!!!!

Tiba
 
Hassani

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2009
Messages
277
Likes
45
Points
45

Hassani

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2009
277 45 45
Nadhani mwandishi kakosea sio CTR ni CRT(crisis responsible team).Kinachoongozwa na Venance toss kitaifa
 
Forum statistics

Threads 1,189,736
Members 450,798
Posts 27,645,707