Polisi Watakiwa kuwasilisha Mikataba ya ujenzi eneo la Kunduchi, Mikocheni na Oysterbay jijini Dar

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
Screenshot from 2016-06-05 13:27:54.png

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira ameliagiza Jeshi la Polisi kuwasilisha Mkataba wa Miradi ya ujenzi wa nyumba za kuishi askari eneo la Kunduchi, Mikocheni pamoja na Kituo cha polisi cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, mradi unaohusisha pia majengo mbalimbali ya Mwekezaji ambaye Jeshi la Polisi limeingia nae Mkataba.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Jenerali Rwegasira amesema mradi huo ni mkubwa sana na wa muda mrefu na hivyo ameliagiza jeshi hilo kuuwasilisha Mkataba huo ambao utekelezaji wake unaendelea ili aweze kuufahamu vizuri mkataba huo unaolihusisha Jeshi la Polisi na Mwekezaji wa Kampuni ya Mara World Tanzania limited.

Jenerali Rwegasira ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki muda mfupi baada ya kukagua miradi hiyo katika maeneo ya Kunduchi na Mikocheni ambako zinajengwa nyumba za kuishi askari wa jeshi la Polisi na kwamba ujenzi wake bado unaendelea.

Jenerali Rwegasira ametembelea pia mradi wa ujenzi wa Kituo cha Polisi eneo la Polisi Oysterbay ili kuona maendeleo ya ujenzi huo sambamba na kufahamu hatua iliyofikiwa hadi sasa katika maeneo hayo ya jeshi la polisi.

Aidha mwekezaji huyo ambaye ni Kampuni ya Mara World Tanzania limited katika eneo la Polisi Oysterbay atajenga kituo cha polisi cha kisasa, ofisi za kukodisha, hospitali, maduka makubwa na hoteli.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.

5 Juni, 2016.

My Take:
Sasa Kimenuka rasmi.
 
haya tusubiri wateteaji waje maana wao kila kitu wanapinga ila katibu mkuu aache siasa za promo hiyo kitu haikuhitaji press release
 
huku tunakoenda hata siri za kijeshi zitarushwa ili waonekane tu kwenye TV
IMPULSIVE MEN !
 
Tunaomba awe amedhamiria sio kutafuta umaarufu wa kisiasa.
 
View attachment 353806

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira ameliagiza Jeshi la Polisi kuwasilisha Mkataba wa Miradi ya ujenzi wa nyumba za kuishi askari eneo la Kunduchi, Mikocheni pamoja na Kituo cha polisi cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, mradi unaohusisha pia majengo mbalimbali ya Mwekezaji ambaye Jeshi la Polisi limeingia nae Mkataba.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Jenerali Rwegasira amesema mradi huo ni mkubwa sana na wa muda mrefu na hivyo ameliagiza jeshi hilo kuuwasilisha Mkataba huo ambao utekelezaji wake unaendelea ili aweze kuufahamu vizuri mkataba huo unaolihusisha Jeshi la Polisi na Mwekezaji wa Kampuni ya Mara World Tanzania limited.

Jenerali Rwegasira ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki muda mfupi baada ya kukagua miradi hiyo katika maeneo ya Kunduchi na Mikocheni ambako zinajengwa nyumba za kuishi askari wa jeshi la Polisi na kwamba ujenzi wake bado unaendelea.

Jenerali Rwegasira ametembelea pia mradi wa ujenzi wa Kituo cha Polisi eneo la Polisi Oysterbay ili kuona maendeleo ya ujenzi huo sambamba na kufahamu hatua iliyofikiwa hadi sasa katika maeneo hayo ya jeshi la polisi.

Aidha mwekezaji huyo ambaye ni Kampuni ya Mara World Tanzania limited katika eneo la Polisi Oysterbay atajenga kituo cha polisi cha kisasa, ofisi za kukodisha, hospitali, maduka makubwa na hoteli.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.

5 Juni, 2016.

My Take:
Sasa Kimenuka rasmi.
Nimeona mjenzi WA pale mikocheni Ni kampuni ya rostam Aziz nikajua tiyari tumeliwa na huenda hiyo mwekezaji ndiye mjenzi
 
Sitaki kuamini kama Polisi iliingia mikataba hii na wawekezaji bila wizara kuwa na taarifa na bila kuwa na nakala za mikataba.Kwa hali sitaacha kushangaa

Inawezekana Mkuu.
Mimi nimeishaishuhudia hii ikifanyika kwenye taasisi moja. Na Baada ya ufisadi kugundulika Wizara husika ikawa haijui kitu chochote. Labda sema kwa vile mradi ni mkubwa sana, siyo rahisi kutoihusisha wizara. Lakini amini kabisa kuna mambo mengi yanayofanywa na viongozi wa taasisi za serikali bila Wizara kujua.
 
Sitaki kuamini kama Polisi iliingia mikataba hii na wawekezaji bila wizara kuwa na taarifa na bila kuwa na nakala za mikataba.Kwa hali sitaacha kushangaa

Hiyo ni ajabu kwa kweli, ina maana Wizarani hakuna hiyo mikataba, mpaka haiombe Jeshi la Polisi? Lakini kingine cha kujiuliza hii inapaswa kuwa taarifa kwa Umma au ndio wanataka kuosha nyeusi kuwa nyeupe?
 
Back
Top Bottom