Polisi wasaka simu ya Lema

Benz Petrol

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
504
Reaction score
196
Wakati Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema (pichani), akitarajiwa kufikishwa mahakamani leo, kuna taarifa zinazoeleza kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo linatafuta simu ya mkononi ya mbunge huyo ili kufuta ujumbe mfupi wa maneno (sms) wa vitisho anaodaiwa kutumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Ijumaa iliyopita mke wa mbunge huyo, Neema Lema, alikwenda katika kituo kikuu cha polisi kumpelekea chai mumewe, lakini askari walimtaka awapatie simu ya Lema.

Habari zinaeleza kuwa askari polisi hawakumueleza Neema sababu za kuitaka simu ya mumewe, lakini aliwaeleza kuwa hajui iliko.

Chanzo chetu kinaeleza kuwa baada ya Neema kuwaeleza kuwa hakuwa nayo wala kujua iliko, askari mmoja wa kike alichukua mkoba wake na kuanza kuupekua kwa ajili ya kuitafuta simu ya mbunge.

Hata hivyo, askari huyo ambaye ni msaidizi wa mmoja wa maofisa waandamizi wa jeshi hilo mkoani Arusha, aliamua kumrejeshea Neema mkoba wake.

Lema akizungumza na waandishi wa habari Alhamisi iliyopita kabla ya kukamatwa siku hiyo usiku, alisema kuwa Mulongo alimtumia sms za vitisho zilizokuwa zinamtaka ajisalimishe katika kituo cha polisi na zingine zikimtishia maisha.

NIPASHE jana lilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, kuhusiana na sababu za Jeshi la Polisi mkoani humo kuitafuta simu ya mkononi ya Lema, alisema kuwa asingeweza kuzungumzia masuala ya Lema kwa kuwa alikuwa katika msafara wa Rais Jakaya Kikwete jijini Arusha.

"Nipo katika msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, siwezi kuzungumzia masuala yanayomuhusu Lema kwa sasa, niko ‘bize' labda unitafute baadaye tutazungumza," alisema Sabas.

Hata hivyo, alipotafutwa baadaye kabla gazeti hili kwenda mitamboni, simu yake iliita bila kupokelewa.

Aprili 24, mwaka huu wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) walifanya vurugu kubwa chuoni hapo baada ya kuuawa kwa mwenzao, Henry Kago (22), aliyechomwa kisu na watu wasiojulikana.

Kago alichomwa kisu Aprili 23 saa nne usiku akiwa njiani eneo la kanisa la Wasabato akitokea chuoni hapo kujisomea.

Baada ya taarifa za kifo hicho, wanafunzi wa chuo hicho walikusanyika na kuanza maandamano hadi kituo kikuu cha polisi wakilalamikia ulinzi duni.

Muda mfupi baadaye Lema alifika na kuwatuliza wanafunzi hao na kuzungumza nao kwa zaidi ya saa tatu wakati wakimsubiri Mulongo.

Hata hivyo, baada ya kufika chuoni hapo Mulongo alishindwa kuzungumza kutokana na kutokuwapo kwa vipaza sauti chuoni hapo, jambo lililopelekea wanafunzi hao kuanza kumzomea na kumrushia chupa za maji pamoja na mawe kabla ya uongozi wa chuo kubadili ukumbi wa mkutano.

Zomeazomea hiyo iliendelea na mkutano kuvunjika na polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kufika na kuanza kurusha mabomu ya machozi ili kuwatawanya wanafunzi hao.

Kufuatia kitendo hicho, Jeshi la Polisi Mkoani Arusha lilimtuhumu Lema kama kichocheo cha vurugu hizo na kuanza kumtafuta ili kumfungulia mashitaka ya uchochezi.

Alhamisi saa 9:30 usiku polisi wakiwa kwenye magari manne, mbwa, mabomu ya machozi na silaha nyinginezo za moto, walivamia nyumba ya mbunge huyo na kumtia mbaroni.

Operesheni ya kutiwa mbaroni Lema iliongozwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha (OCD), Gillel Muroto ambaye alifuatana na askari zaidi ya 25.

Kabla ya kumkamata, askari hao waliruka ukuta wa fensi ya nyumba ya mbunge huyo na kuvunja mlango na kumkamata kisha kumfunga pingu hadi kituo kikuu cha polisi huku akisindikizwa na umati wa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

CHANZO:
NIPASHE
 
Afadhari sasa hata wasiopenda kufikiri wataelewa kwanini Lema alikamatwa na kufunguliwa mashitaka, kumbe kesi imepikwa na mkuu wa mkoa, mtazamo wangu hapa ni huu, Mkuu wa mkoa anahisi kadharirishwa cause hafanyi kazi za wananchi badala yake muda mwingi anafanya kazi za chama, imekuaje Lema akafika mapema hapo chuoni while yeye mkuu wa mkoa ambaye OCD, RPC, RCO wanatii amri zake na bado hakufika chuoni on time, kitendo cha yeye kuanza kudai vipaaza sauti ili aongee na wanafunzi, swali, kwanini Lema aliweza kuongea nao without microphones na speakers halafu yeye ashindwe?

Kuwa na vipaaza sauti mahali it means kuna maandalizi, hapa mtu kapigwa kisu kafa, hii ni emergence, nani anapata muda wa kutafuta hayo mavyombo? Poor thinking capacity kabisa, bado nafikiria, hivi hawa wakuu wa mikoa, kigezo gani hua kinatumika kuwachagua?
 
Wanaitafuta simu ya nini tena wakati mwenzao (Mulongo) ameshakanusha kuwa hajawahi kumtumia msg hiyo Mh. Lema? Wakitaka wakamchukue maelezo Mulongo wamsikie kwanza, manake keshatoka public kukanusha kuwa msg siyo yake. Au ndo keshajua kuwa atasutwa kwa kusema uongo mbele ya umma? Unajua ukitaka kudanganya lazima uwe very smart.
 
Jamani,

Kama ni kweli tuelimishane wote kuhusu mambo haya kama simu. Polisi wa Tanzania na wakuu wao ni wajinga kupindukia.

Meseji inapokuja kwenye simu inaweza kukaa kwenye handset au kwenye SIMCARD. Na wakati mwingine inaweza kuwekwa kopi kote kwenye Handset na SIM card kutegemea na simu yako.

Zipo zingine ni zaidi ya hapo. Meseji au chochote kinaweza kukaa kwenye Memory card.

Hivyo, unaweza kuamua kuwapa handset hao polisi wajinga na wakaifuta meseji wakaamini kabisa wamakukosesha ushahidi, lakini wakashangaa kuwa nao siku utakapohitajika.

Zaidi ni kwamba zipo simu ambazo unaweza ku-backup content zako kwenye computer yako (zako) na kukaonekana kama hakuna chochote kwenye handset.

Ukifanya hivi utakuwa umewapiga changa la macho, lakini ili kuwahadaa mkikamatwa na polisi hakikisha umefanya backup ya content ikiwemo phonebook, SMS na MMS zote kwenye simu yako.

Wabunge naamini wana simu zenye features za namna hii. Ukishfanya backup yaani kwenye laptop yako iliyo offline, nenda uka-upload contents hizo kweny online memories kama vile email yako ya gmail na zingine nyingi tu.

Hivyo, polisi au wenzao watakapopekua nyumba yako, watachukua kila kitu hadi laptop lakini utakuwa umewakomsesha kwani watakuwa wamechukua makasha tu yaani hardware lakini software content ume-save wasikoweza kufika.
 
Hizi ni akili za akina malungo refer naibu wa elimu....
polisi wanatumika na vilaza iwe wanajijua ama la..
 
hawa watu majina yao yanayoanzia na M na kuishia na O wana shida kweli::::2013 ni mwaka wao
 
Hayo ni mambo ya shule sasa polisi wenyewe darasa la saba
 
Wanaisaka simu na lema wamespend nae wikiendi yote? Policcm bwana akili zao huwa wanashikiwa. Waende na mabomu ya kutupa na mkono, vifaru, mbwa na farasi wakaipekue nyumba yake upya. Ama vile waliazima?
 
Sasa si wacheki na TCRA waifute juu kwa juu!
Maana wao wana mkono mpana
 
Wanahofu baada ya kusikia CHADEMA watamshataki Mulongo.
 
Mwenzao Mulongo alishakanusha kuwa hajamtumia Mh. Lema sms hiyo, wao wanaitafuta ya nini? Unajua ukishakuwa mwongo you have to be vey smart!
 
S wakaufute huo ujumbe kwa 'service provider' ili Lema aonekane 'kajitungia meseji'?!
 
uongo ni mwingine ni wa kipuuzi sana kuachiwa hapa, huo ujumbe umewekwa kila mahali sasa hao wanaotaka kuufuta ni wajinga kiasi gani.
 
uongo ni mwingine ni wa kipuuzi sana kuachiwa hapa, huo ujumbe umewekwa kila mahali sasa hao wanaotaka kuufuta ni wajinga kiasi gani.

unamanisha NIPASHE ni waongo au nani?
 
Ile sura ya Mkuu wa Mkoa ni kichefuchefu tosha. Sasa anawasingizia watoto wa watu kuwa ni kichefuchefu
 
Kiongozi mkuu wa shughuri za serikali mkoani, Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya mkoa, mwakilishi wa Rais mkoani, Rais wa mkoa, anapogeuka na kufanya kazi kihuni namana ya Magesa Mulongo, wavuta/wala unga/bangi wafanye nini sasa.

Anaendekeza siasa na jazba, meseji atume yeye mwenyewe then anaanza kutafuta simu kupitia mapolisi uchwara wazee wa ndio mkuu/mzee, poleni.

Polisi wetu watakuwa huru na kuondokana na utumwa walionao siku ccm wakiondoka madarakani.
Poleni polisi wa Tanzania, ile acheni nidhamu ya uonga, nidhamu ya kutii amri ambazo sio halali, nawapa pole wanaotafuta kazi ya upolisi wakati huu ambao ccm bado iko madarakani.
 
First they ignore you, then they laugh at you, then they fight you, then you win. - Mahatma Gandhi
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…