Polisi wapiga mabomu Mbinga,watoto waongoza maandamano

Polisi wapiga mabomu Mbinga,watoto waongoza maandamano

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Joined
Sep 7, 2011
Posts
3,295
Reaction score
2,505
Ni muda mfupi uliopita polisi wamepiga mabomu ya machozi ya kutosha kusambaratisha maandamano mbinga mkoani Ruvuma.

Maandamano hayo yanalenga kupinga malori yanayobeba makaa ya mawe toka wilayani humo na wazazi wameamua kuwatanguliza watoto katika maandamano hayo jioni hii.

Hadi sasa Polisi imewakamata viongozi wanaodaiwa kuongoza maandamano hayo na kiongozi mkuu ametajwa kuwa ni John John Komba (Haijaelezwa uhusiano wake na Mbunge wa jimbo hilo Kapteni John Komba).

Aidha waandamanaji wameeleza kuwa hawataacha maandamano hayo hadi hapo kitakapoeleweka na makaa hayo yaachwe kusafirishwa kwa namna tyoyote toka wilayani kwao.

Pia wameeleza kuwa hawataki kumuona Mkuu wa wilaya hiyo wala mkuu wa Mkoa kwani wamepelekewa malalamiko mara kadhaa bila kuchukua hatua yoyote.

Star Tv wameeleza katika Breaking news.
 
Ina maana kuna watu wanatekeleza sera za chadema huko Mbinga?

Ssasa watoto wa nini kwenye maandamano
 
Ina maana kuna watu wanatekeleza sera za chadema huko Mbinga?

Ssasa watoto wa nini kwenye maandamano

Haki ya nani utakuwa na matatizo kichwani sio bure! Au lah utakuwa umetoroka kitanda Mirembe Hospital
 
shida ya polisi wetu hawajajua haki ya maandamano any way serikali sikivu iko wapi
 
Ina maana kuna watu wanatekeleza sera za chadema huko Mbinga?

Ssasa watoto wa nini kwenye maandamano

Inamaana kuwa ni CHADEMA tu ndio sera za kuona uchungu wanapoona rasilimali za taifa zinaondoka na hakuna impact yoyote kwa uchumi wa jamii inayozunguka? it is clear that CCM will never be agigatated hata kama nchi yote ikiuzwa kwa mabeberu.
 
Waandamane, wasiandamane Mkaa utatoka tuuu. Si mali ya Mbinga. Upate soko kwanza, watu wale kidogo ndio mifupa na mapanki yaletwe Mbinga. Yule jamaa yenu atakula nini kile kitumbo kisipungue.
Ati sera za CDM. Huko nako CDM wamefika? 2015 si mbali, msiogope mabomu, Mbinga komaeni mpaka 2015.
 
Hapana, wanapinga sera ya ccm ya kuwaibia wananch raslimali zao wanakwenda kufaidi wachache huku wananchi wakibaki maskini na hawana huduma mhimu za kijamii, chunguza vizuri utaelewa baadae
Na wana itekeleza kauli ya Wapigwe tu..........iliyotolewa na Pinda
 
Waandamane, wasiandamane Mkaa utatoka tuuu. Si mali ya Mbinga. Upate soko kwanza, watu wale kidogo ndio mifupa na mapanki yaletwe Mbinga. Yule jamaa yenu atakula nini kile kitumbo kisipungue.
Ati sera za CDM. Huko nako CDM wamefika? 2015 si mbali, msiogope mabomu, Mbinga komaeni mpaka 2015.

ukiona wananchi wa vijijini nao ia mali zao kwa kiwango hiki basi ujue ukombozi wa nchi hii toka makucha ya mkoloni mweusi umekaribia.
 
Mbinga wanaibiwa mchana kweupe, barabara za mbinga hasa vijijini ni vumbi tupu, wabunge na madiwani wa mbinga ni mizigo mitupu, makaa ya mawe yanachimbwa na kuondolewa kimyakimya, na inasadikika wakuu wa wilaya na mkoa ndo madalali wa kutorosha makaa ya mawe mbinga! Pia mwenyekiti wa ccm Mkoa wa ruvuma aitwaye Oddo mwisho ufisadi na yeye ni pete na kidole!wananchi wa mbinga wasiposimama kidete wataendelea kuvuna mabua!
 
Hapo CHADEMA imeingilia wapi?
Mlango wa KIA?

Maandamanao ni ya wananchi katika harakati za kudai Uhuru wa kiuchumi. Lakini kwa akili yako kubwa kama pua yako, unaamini kwa moyo wa dhati kwamba kila maandamano ni ya CHADEMA.
CHADEMA haikuvumbua maandanao Tanzania wala haina PATENT ya maandmano.

Maandamano ni moja kati ya njia halali KIKATIBA zinazotumwa na wananchi kutoa ujumbe vitendo kwa serikali ili kuibana ichukue hatua zinazostahili.

Enzi za Nyerere wanawake waliwahi kuandamana mpaka kwake wakiipinga uhaba wa nguo Tanzania.( Enzi hizo za RTC na maduka ya kaya naamini ulikuwa kindaDUCHU au hukuwepo kabisa)
Sasa sijui nao walikuwa wakifuata sera za CHADEMA?

CCM na waumini wake wanaamini kwamba wananchi wakiandamana mahali popote nchini Tanzania ni wafuasi wa CHADEMA.
Hii ni imani potofu na potevu

Hiyo kitu mimi naiita Myopic way of thinking; Yaani ni sawa na kuwa na uchi wa akili.
Ukiwa na uchi wa mnyama tutakufunika kikoi kusetili aibu yako, ukionyesha uchi wa akili yako tutaufunika na nini ili kusetiri aibu ya akii yako??

Ina maana kuna watu wanatekeleza sera za chadema huko Mbinga?

Ssasa watoto wa nini kwenye maandamano
 
Inamaana kuwa ni CHADEMA tu ndio sera za kuona uchungu wanapoona rasilimali za taifa zinaondoka na hakuna impact yoyote kwa uchumi wa jamii inayozunguka? it is clear that CCM will never be agigatated hata kama nchi yote ikiuzwa kwa mabeberu.
ARE YOU SICK IN YOUR OWN HEAD? OR yOU NEED MEDICS? what do you mean by mabeberu/
 
Ni muda mfupi uliopita polisi wamepiga mabomu ya machozi ya kutosha kusambaratisha maandamano mbinga mkoani Ruvuma. Maandamano hayo yanalenga kupinga malori yanayobeba makaa ya mawe toka wilayani humo na wazazi wameamua kuwatanguliza watoto katika maandamano hayo jioni hii. Hadi sasa Polisi imewakamata viongozi wanaodaiwa kuongoza maandamano hayo na kiongozi mkuu ametajwa kuwa ni John John Komba (Haijaelezwa uhusiano wake na Mbunge wa jimbo hilo Kapteni John Komba). Aidha waandamanaji wameeleza kuwa hawataacha maandamano hayo hadi hapo kitakapoeleweka na makaa hayo yaachwe kusafirishwa kwa namna tyoyote toka wilayani kwao. Pia wameeleza kuwa hawataki kumuona Mkuu wa wilaya hiyo wala mkuu wa Mkoa kwani wamepelekewa malalamiko mara kadhaa bila kuchukua hatua yoyote. Star Tv wameeleza katika Breaking news.

kama hadi Mbinga wameandamana basi ukombozi wa nchi hii umekaribia
 
Mbinga wanaibiwa mchana kweupe, barabara za mbinga hasa vijijini ni vumbi tupu, wabunge na madiwani wa mbinga ni mizigo mitupu, makaa ya mawe yanachimbwa na kuondolewa kimyakimya, na inasadikika wakuu wa wilaya na mkoa ndo madalali wa kutorosha makaa ya mawe mbinga! Pia mwenyekiti wa ccm Mkoa wa ruvuma aitwaye Oddo mwisho ufisadi na yeye ni pete na kidole!wananchi wa mbinga wasiposimama kidete wataendelea kuvuna mabua!
Viongozi wanapokuwa madalali wa ufisadi na wizi, wananchi wakimbilie wapi jamani?? Nchi hii inatia hasira sana
 
Duh! Hivi ni kwanini mtu anapokuwa mwana CCM anakuwa kama taahira? Jamani naomba kueleweshwa!!!

simjuia Chris Lukosi, lakini kwa maandishi yake ninavyoyaona naamini zamani alikuwa mpinzani (whether chadema au chama kingine) kisha akafukuzwa na ndio maana amebaki na hasira kichwani na wala hafikirii kabla ya kuandika. Hii ni kwasababu maandishi yake hayatofautiani kabisa na Juliana Shonza, Mtela pamoja na Tuntemeke. Hawa wote walikuwa wapinzani kabla ya njaa zao kuwapeleka CCM. Likewise kwa huyu bwana Chris
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom