Polisi wanne wafukuzwa, washtakiwa kwa rushwa

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Tabora leo imewapandisha mahakamani polisi watatu kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Sh3 milioni kutoka kwa mmoja wa wafugaji wa kijiji cha Mkirigi wilayani Kaliua.

Hatua ya kufikishwa mahakamani kwa polisi hao kunakuja wiki chache baada ya gazeti la Mwananchi kuripoti tukio hilo ambapo Takukuru pamoja na uongozi wa polisi mkoa wa Tabora uliamua kufanya uchunguzi na kuthibitisha habari zilizoandikwa na Mwananchi.

Waliofikishwa mahakamani leo baada ya kufukuzwa jeshini kuanzia jana ni pamoja John Okinda, Kabila Pius na Patrick Robert, huku mtuhumiwa mmoja, Elisha David akifanikiwa kutoroka muda mfupi kabla ya kukabidhiwa mikononi mwa Takukuru.

Mbele ya hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Urambo, Hassan Momba inadaiwa na wakili wa Takukuru, Edsoni Mapalala kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo Machi 7, mwaka huu.

Wakili Mapalala ameiambia mahakama kuwa siku hiyo katika Kijiji cha Mkirigi kata ya Ilege wilayani Kaliua, washtakiwa wakiwa ni waajiriwa wa Jeshi la polisi waliomba rushwa ya Sh3 milioni kutoka kwa Dotto Ng'andulanye ili wasimchukulie hatua za kisheria baada ya kumtuhumu kumkuta ameotesha mche mmoja wa bangi shambani kwake.

Katika shtaka la pili washtakiwa walidaiwa kupokea rushwa ya Sh3 milioni kutoka kwa Ng'andulanye kama kishawishi cha kutomchukulia hatua za kisheria kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.


Watuhumiwa wote wamekana mashitaka dhidi yao na shauri hilo kuahirishwa hadi Aprili 27, mwaka huu itakapoanza kusikilizwa baada ya upande wa mashtaka kuieleza mahakama kuwa upelelezi umekamilika.

Upande wa mashtaka haukuwa na pingamizi kuhusu dhamana ambapo mahakama ilimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika, mmoja akiwa mtumishi wa Serikali watakaosaini hati ya dhamana ya Sh2 milioni kila mmoja.


Chanzo: Mwananchi
 
duh! enzi zile wasingefuatiliwa kwa taarifa za magazetini hata kama ni za kweli! asante Magu kwa uzalendo na uchungu wa nchi kwa maana taratibu tunaweza kuchukuliana hatua wenyewe


Wangepewa vyeo au kuhamishwa..
 
duh! enzi zile wasingefuatiliwa kwa taarifa za magazetini hata kama ni za kweli! asante Magu kwa uzalendo na uchungu wa nchi kwa maana taratibu tunaweza kuchukuliana hatua wenyewe
Ni hatua nzuri sana aisee, nchi inaanza kurudi kwenye misingi
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Taraaaatibu nchi inaanza kunyoka, walizidi hawa polisi kwa kubwia rushwa.
 
  • Thanks
Reactions: dtj
hao hawapo katika level ya kuhojiwa kwanza na tume ya maadili bongo visa haviishi mtu anaiba eti mpaka ahojiwe na watu wa maadili kazi ya police au takukuru ni nini sasa...
 
Mwizi anamuhoji mwizi!mchafu kwa mchafu basi shida tu.....hakuna wakumsikiliza mwenzake
 
Back
Top Bottom