VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Polisi wetu tunawapenda. Mnapotukera,tunawaponda. Mnapofanya jambo jema,tunawapongeza. Mnapoboronga,tunawaasa hata kisasa hasa kujitenga na siasa.
Wanasiasa wana mambo mengi. Wanasiasa,katika dunia yao ya siasa,wana marafiki na maadui. Wana bifu zao na furaha zao. Wanaishi tofauti na wengine. Wapo wanasiasa wa aina mbili: watawala na watawaliwa
Wanasiasa watawaliwa ni wepesi sana. Ni wanyonge. Hawana ubavu wa nguvu kupenyeza ushawishi au amri kwa vyombo vya usalama. Kwa sifa hizo,hawana tofauti sana na wananchi wa kawaida. Ulinzi wao mkuu ni public sympathy.
Wanasiasa watawala wana ushawishi na hata kupenyeza amri zao. Hutumia ukaribu wao na wakuu wa kiserikali na kichama kufanya yao kwa vyombo vya ulinzi kama polisi. Nawataja sana polisi kwakuwa wao ni wa karibu yetu zaidi
Pamoja na makandokando hayo yote,polisi wanapaswa kufanya kazi zao kwa uhuru,weledi,juhudi na maarifa. Wanafunzwa hivyo vyuoni mwao. Ili kufanya kadiri ya mafunzo na wanachotamani wananchi,polisi wanapaswa kujitenga na wanasiasa.
Kwa kinachoendelea katika kile kinachoitwa mapambano dhidi ya madawa ya kulevya,aibu tunaona sisi wananchi!
Mwafaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam