Ni masikitiko yangu makubwa kwa hali kama hii ambayo wanaofanyiwa ni watanzania, ila kwa vile wako upinzani. Hivi Tanzania ni nani, nijuavyo mimi Tanzania ni ya raia wote bila kujali awe wa chama chochote cha siasa. Tunakopelekwa na ccm siko, ccm wanatuandalia maafa ambayo haitasaulika katika historia ya Tanzania. Mpaka sasa ccm hawajakubali mabadiliko ccm inaona wale wote wanaojiunga na vyama ni adui yao na wanataka awe adui wa kila mtanzania. Wakati anaeonwa ni adui nae ni mtanzania. Ccm wanatuletea utengano katika Tanzania kwa tamaa yao ya madaraka. Najiuliza/nauliza hivi angekuwa wabunge wa ccm ndio wamecharazwa mapanga hao jamaa siwangekuwa ndani. Inawezekanaje Wanachama wa chadema zaidi ya 70 Arumeru juzi wamepigwa mabomu na kusekwa ndani kisa kuponda gari la kigogo wa ccm lakini waheshimiwa wabunge wa upinzani wamekatwa mapanga wakiwapo polisi lakini mpaka sasa hakuna aliekamatwa hata mmoja. hivi leo chadema wachukue nchi hawa watawala wanaofanya ivi si ndio watasababisha kulipizana kisasi.