Songambele
JF-Expert Member
- Nov 20, 2007
- 4,710
- 2,587
Mpira umekwisha Ndanda 1 - Maji Maji 0, hivi punde katika uwanja wa Nangwanda Sijaona (Umoja) Mjini Mtwara lakini uwezi amini macho yako Polisi wametengeneza vurugu baada ya kumkamata na kumtupia ndani ya defenda shabiki wa ndanda na kumshushia kipigo ambacho hakikuwa cha lazima. Na kwakuwa wananchi wamekirika kunyanyaswa na Polisi wenyewe wanawaita watu kutoka kaskazini wanawaonea nyumbani kwao bila sababu. Wananchi wamejikusanya na kusubiri nje ya uwanja kwanza gari la timu ya Maji Maji limetoka, likifuatiwa na la ndanda kwa Amani kabisa.
Timu zilipotoka na waamuzi wananchi wakawa wanasubiri na polisi nao watoke ili kiputwe nje ya Uwanja, Raia walianza kurusha mawe na polisi wakajibu kwa mabomu na yanaendelea kulindima katika maeneo yanayozunguka uwanja wa Nangwanda mida hii machozi na watu wananawa maji.
Binafsi nilikuwa uwanjani na kiukweli Polisi wanaanzisha vita bila sababu na wananchi kama kuna ambao mnaweza ongea na wakuu wao waambie uwanjani, shamra shamra hazikosi na uwanja umezungukwa na Bar na Grocery za kutosha manake walevi pia ni sehemu ya mashabiki. Vurugu zimetoka nje ya Uwanja na Raia wasio na Hatia imewagusa na wananchi wanasema wametoneshwa jambo lao la Gesi na wanajipanga hawawezi kukubari kushindwa kiraisi na wanataka shabiki mwenzao aachiwe na Polisi waliomshushia kipigo wachukuliwe hatua.
Wengine watatoa updates kama kuna madhara tutajurishana lakini polisi wameongeza vikosi.