Polisi wanane mbaroni kwa kuua raia kinyama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wanane mbaroni kwa kuua raia kinyama

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mwandiga, Dec 6, 2011.

 1. mwandiga

  mwandiga JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  · Wadaiwa kumtesa, kumpiga, kumdhalilisha hadharani
  · Wadaiwa kumpasua bandama kwa kitako cha bunduki
  · Mdogo wake naye yuko hoi mahabusu kwa kipigo
  Jeshi la polisi mkoani kigoma linawashikilia askai wanane wa kituo chake cha wilaya ya kasulu kwa tuhuma za kkmtesa, kumpakipigo na kumuua raia festo andrea,kwa tuhuma za ujambazi wa ktumia silaha…………..
  Kamanda wa polisi mkoa wakigoma Frasser Kashai alithibitisha kutokea kwa tukio hilo(Agosti 08.2011 …….. .
  Alisema “ askari wote wanane tunawashikilia na tunafanya uchunguzi juu wao waliohusika….” Hata hivyo alikataa kutaja majina ya askari hao kwa maelezo kuwa tuhuma hizo zinachunguzwa na kushughulikwa na uongozi wa juu wa jeshi la polisi.
  Source: Nipashe la tarehe 03/12/2011
  Mimi ni najishughulisha na kilimo cha tumbaku na mahindi mkoa wa kigoma. Kwa hii habari kuna uongo mkubwa sana umeandikwa ambao umenipa machungu sana hadi kufikia kuandika haya. Ukweli ni kwamba huyu bwana kweli aliuawa kinyama na hao askari wanane. Hili swala likamfikia mbunge bwana moses machali na akaliongelea kwenye mkutano wa hadhara kulaani kitendo hicho, hawa askari wote wakawekwa lokapu ya polisi lakini muda wote huowalikuwa nje wanashinda kwenye baa ya polisi wakinywa bia na baadhi yao kwenda mjini kuzunguka na pikipiki na magari yao. Haya yote yalikuwa yanafanyika ocd akiona, na kulikuwa na timu ya polisi kutoka kigoma kwa ajili ya uchunguzi. Mwezu wa kumi na moja wote wakaachiwa huru na wapo mtaani tena wanatamba sana kuwa mambo yameisha kipolisi hivyo hawana hatia. Mbunge amesma hajui kama wapo nje lakini kwa mji wa kasulu ni mdogo wote wanaonekana muda wote, majina yao yapo na mengine yametajwa gazetini,
  Ni kitendo ambacho kimeuma watu wengi sana hapa kigoma lakini cha ajabu wauaji wote 8 wapo nje na sio kama frasser Kashai anavyosema wapo ndani nina ushahidi na hilo na hata mkitaka picha nitaweka kuwaonyesha. OCD simjui jina nae anaona hili jambo, DC nae ni walewale hana tofauti nao kwani alisema wakulima wapigwe risasi wafe nae haoengei lolote kwa watuhumiwa wa mauaji wapo nje. Lingine hao wote wanamiliki bunduki wamezificha ili kuwabambikia watu kesi. Huu ni ukanda wa vita hivyo silaha ni nyingi vijiji vya mipakani.
  Tukemee huu uongo na tusaidie haki itendeke maana hapa nimesikia watahamishwa vituo ili wasionekane kigoma. Sheria inasemaje kuhusu watuhumiwa wa mauaji? Wenye uelewa na sheria tafadhali mtujuze. Wanastahili kuwa mitaaani?
  Nitafutatilia kisha nitawajuza kijiwe wanachoshinda ili kwa mfuatiliaji ahakikishe mwenyewe. Pia chanzo cha mgogoro nitawaambia maana kuna wakulima wenzangu wapo rungwe mpya wanajua kisa hiki, nitawatafuta. Hawa ni polisi wanakula kodi zetu kama mishahara.
  Kwa nini OCD, OC CID, RPC na RCO na huyu kashai waiwajibishwe????? Najau waziri atasoma hapa, chukua hatua.
  Na huyu mwandishi aliyeandika hii habari ameshindwa kwenda Kasulu kuhakikisha maneno ya Frasser? Angewakuta tu mtaani na angeuelezea umma ukweli
   
 2. s

  semako Senior Member

  #2
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona Ditopile aliua tena mbele ya watu kwani alipelekwa wapi?
   
 3. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,429
  Likes Received: 3,792
  Trophy Points: 280
  Na wale waliomuuwa Kombe nao si wako huru..!! Kwa hiyo hata hao nao yatakuwa ni yale yale tuu........ KAMA KADAWIA
   
 4. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  mkuu waandishi wetu hawawezi kuchimbua haya.kama unao ushahidi wa kutosha M pm Invisible mtaalam wa mambo ya uchunguzi ripoti ishushwe hapa!
   
 5. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Pm kwa Pasco pia upate ushauri ili hawa wataalamu wailipue watu wakimbizane.asante kwa ripoti ili sheria ifate mkondo.
   
 6. Inno laka

  Inno laka JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 1,592
  Likes Received: 449
  Trophy Points: 180
  Sheria ndio itakayoamua na sio ww unayekulupuka,,,unaonge wameua umewachek walipokuwa wanaua ucongee k2 usichokijua
   
Loading...