Polisi wamshushia kipigo mwandishi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wamshushia kipigo mwandishi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 30, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  29th December 2010

  Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Tanzania Daima wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga, Ali Lityawi, juzi alipata kipigo kikali kutoka kwa askari wa jeshi la polisi wilayani hapa na kunyang’anywa kamera yake ya kazi kwa madai ya kupiga picha mahabusu aliyetoroka rumande.
  Tukio hilo lilitokea majira ya saa 12:45 jioni katika mtaa wa Lumelezi karibu na Hospitali ya Magai ambapo alikutana na askari hao wakiwa katika jitihada za kumkimbiza mahabusu huyo aliyewatoroka kituoni.
  Akizungumza na waandishi wa habari, Lityawi alisema kuwa baada ya mahabusu huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja kukamatwa na polisi kwa kushirikiana na wananchi waliokuwepo katika eneo hilo, alianza kupiga picha za tukio hilo.
  Alisema katika harakati za kupiga picha, alijitokeza askari mmoja na kuanza kumshambulia kwa kumpiga kisha kumnyang’anya kamera aliyokuwa nayo na katika jitihada za kuigombania, ilidondoka ndani ya mtaro wa maji.
  Lityawi alisema wakiwa katika purukshani hizo, alijitokeza askari mwingine na kumsaidia mwenzake kuendelea kumshambulia.
  Alisema katika jitihada za kugombania kamera, hiyo askari hao walifanikiwa kuichukua huku wakimkamata na kwenda naye kituoni ambapo walifika na kumweleza Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD), George Simba,, aliyeamuru kuwekwa mahabusu kwa muda kwa kosa la kuwapiga askari picha bila kibali maalum.
  “Aliniamuru kufuta picha hizo haraka kwenye kamera na baada ya kukataa na kutaka anionyeshe ni kifungu gani cha sheria kinachompa mamlaka ya kunizuia kufanya kazi zangu, aliamuru itolewe kadi ya kumbukumbu iliyohifadhi picha hizo na kunitaka niifuate kesho yake kituoni hapo,” alisema.
  Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Diwani Athumani, amelaani kitendo hicho kilichofanywa na askari wa jeshi lake na kumtaka OCD kuangalia jinsi ya kumtengenezea kamera yake mwandishi huyo na kumwomba msamaha.
  “Ni sera ya jeshi kusaidiana na waandishi wa habari na vyombo vyao kuwaelimisha wananchi utendaji kazi wa jeshi na kuwapa elimu inayohusiana na usalama wa raia na mali zao. Kama waliona kuwa picha anazopiga si nzuri kwao, wangemwomba asizitumie badala ya kumshambulia, kumharibia kamera yake, lakini pia kumweka mahabusu kwa muda,” alisema.
  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...