Polisi wamsafisha Nassari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wamsafisha Nassari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Medical Dictionary, Oct 30, 2012.

 1. Medical Dictionary

  Medical Dictionary JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 1,053
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha, limemsafisha Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA), kuwa hakuhusika katika tukio la kufyatua risasi hewani kama ilivyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari jana. Badala yake, Kamanda wa Polisi Mkoa, Liberatus Sabas, alisema kuwa wanamhoji mjumbe wa mkutano Muu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Wilaya ya Arusha, Godfrey Mwalusamba, kuhusiana na tukio hilo. Kufuatia hatua hiyo, Nassari ametoa siku 14 kwa magazeti ya Uhuru na Habari Leo kukanusha taarifa walizoandika wakimhusisha na tukio hilo kwenye Kata ya Daraja Mbili siku ya Jumapili, vinginevyo atayashitaki Baraza la Habari nchini (MCT).

  Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Kamanda Sabas alisema kuwa Mwalusamba alifyatua risasi hewani kwa lengo la kumuokoa mwanamke mmoja ambaye jina lake hakulitaja, ambaye alikuwa akishambuliwa na kundi la vijana wakimtuhumu kuwa alikuwa akigawa fedha kwa wapiga kura. Alisema kuwa kwenye tukio hilo, Musa Khamisi, alijeruhiwa kwa kukatwa na panga ambapo jumla ya watu wanane walikamatwa na tayari walifikishwa mahakamani jana kujibu mashitaka ya kujeruhi na shambulio la aibu.

  Naye Nassari, aliwaambia waandishi wa habari kuwa amefikia uamuzi wa kuyataka magazeti hayo kukanusha habari hizo kwa uzito uleule waliotumia kuzitangaza baada ya kutafakari na kujiridhisha kuwa habari hizo ziliandikwa kwa hila, zikiwa na lengo la kumchafua.

  "Magazeti hayo yameandika kuwa nilifyatua risasi saa saba mchana Kata ya Daraja Mbili wakati muda huo nilikuwa Kata ya Bangata nikiwa wakala mkuu wa uchaguzi, siku hiyo nilipita Kata ya Daraja Mbili saa mbili asubuhi kwa ajili ya kushusha mawakala kisha nikaondoka," alisema. Alisema kuwa habari hiyo iliyoandikwa na gazeti la CCM na lile la Serikali iliandikwa kimkakati kwa lengo la kumchafua yeye binafsi na chama chake huku akiweka bayana kuwa huo ni mwendelezo wa hila anazofanyiwa tangu anyakue ushindi wa jimbo hilo.


  Source:tanzania daima
   
 2. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Washita hao, wafungiwe na wao waone utamu.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Magazeti ya Wajinga hayo!
  Ishu ni kwamba Magazeti yenyewe yakanushe habari hizo kwa heading kama walizotoa wakati wakifanya umbea!
  Hivi hawa Wahariri kweli ni professionals!
   
 4. s

  sawabho JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Hilo ndilo tatizo la kufanya kazi wakati mtu anawaza cheo siku sijazo. Wahariri professionals walipaswa kuhoji wahusika kwanza ili kuijiridhaisha pasipokuacha mashaka kabla ya kwenda mitamboni.
   
 5. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kwani hilo Baraza la habari (MCT) lipo wapi kuachia uongo na uchochezi unaofanywa na magazeti ya CCM na Serikali yake? Hivi kweli yangekuwa magazeti mengine na yamemchafua kiongozi wa CCM na chama chake MCT ingeyaachia hayo magazeti? Hizi double standard zimetufanya tuondoe hata ile chembe ya imani tuliyokuwa nayo kwa serikali yetu na vyombo vyake.
   
 6. m

  malaka JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Yaani sasa hivi hata matonya angeweza kuwa Mhariri. Nchi limeoza kila sekta aisee.
   
 7. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kweli wahariri na magazeti yao wamejichafua sana. Hata makanjanja wasiokuwa na elimu ya kutosha katika uandishi wa habari huwa wanajitahidi ku-balance habari. Hawa wanaonekana kabisa wanafanya kazi ya UDAKU ili kuikuwadia CCM.
   
 8. TAMKO

  TAMKO JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Nasema kila siku hatuna Waandishi Wa habari Bali wachafuzi Wa habari.. Sijui lini Tanzania itatoka..
   
 9. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Habari za upotoshaji kabisa na uchochezi. Mbali ya MCT kwanini asiwapeleke mahakamani?
   
 10. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Awapeleke mahakamani! its a defamation.
   
 11. D

  Dan Geoff P Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 25
  Hivi kumbe hata mimi naweza tu kumiliki silaha,,,manake naona siku hizi kila mtu ana kitu cha moto.
   
 12. mpalu

  mpalu JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 2,493
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hakuna kufungiwa wala nn?
   
 13. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,847
  Trophy Points: 280
  hapa suala muhimu ni kuwaswaga mahakamani halafu unadai bonge la FIDIA....kwa nini watu hawajui kutumia OPPORTUNITIES ku make monye jamani??
   
 14. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #14
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Hivi mlitegemea Uhuru na Habarileo waandike kuwa
  aliyefanya vurugu ni kada wa CCM? Waandishi wa
  magazeti haya na wahariri wao wanatekeleza kile cha
  "mtumikie kafiri upate mradi wako"...
   
 15. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Uhuru na habari leo ni magazeti yanayonunuliwa na serikali na mashirika ya umma kwa lazima! yakisambazwa maofisini yanatupwa kwenye dust bin au wanapewa masecretary,mesenger.Ni ubadhirifu wa kodi yetu kununua magazeti ambayo hayasomwi kwa walengwa!
   
 16. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,862
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Magazeti yaandikayo ukweli yanafungiwa sasa haya ya uongo ndio yanaachwa? hivi hawa uhuru walishiriki yale maandamano ya waandishi wa habari kupinga kuuwawa kwa Mwangosi?
   
Loading...