Polisi wakiwa kazini benki ya CRDB

Polisi wakiwa kazini benki ya CRDB

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,347
Kijana-1.JPG

Kijana-3.JPG

Kijana-2.JPG

Kijana-4.JPG


TAFRANI imetokea katika Benki ya CRDB, tawi la Azikiwe,baada ya kijana mmoja aliyehisiwa kuwa jambazi kurusha mawe kwenye vioo vya benki hiyo na kusababisha wateja kukimbia ovyo wakidhani wamevamiwa. Tukio hilo lilitokea jana mchana, ambapo kijana huyo anayedhaniwa kuwa akili yake imeathirika kwa kubuia dawa la kulevya 'Teja' kurusha mawe kuelekeza kwenye jengo hilo na kuvunja vioo.

Baadhi ya wateja walianza kutimua mbio kutoka nje huku wengine wakilala chini kuhofia maisha yao. Baada ya kuona hivyo, Polisi waliokuwa kwenye lindo la benki hiyo, walifyatua risasi juu wakidhani majambazi wamevamia benki hiyo. Lakini baada ya muda walimuona kijana huyo aliyekuwa katikati a Barabara ya Azikiwe karibu na kituo cha Daladala cha Posta Mpya, akiendelea kurusha mawe.

Polisi walimuendea na kufanikiwa kumdhibiti na kuanza kumpatia mkong'oto wa nguvu, huku wanachi wenye hasira wakitaka nao waruhusiwe kumwadhibu. Ndani ya benki hiyo hali ilikuwa shaghalabaghala, kwani mitungi ya maua na baadhi ya nyaraka zilitawanyika ovyo, huku wakioneakana baadhi ya wateja wakiwa wamezirai na wengine wakilia baada ya kupotelewa na nyaraka muhimu za benki vikiwemo kadi na fedha taslimu. Wakati tukio hilo ilitokea, pia hali haikuwa nzuri kwa wafanyakazi wa benki hiyo, kwani baadhi walisikika kuwa walipatwa na hofu kubwa kiasi cha baadhi yao kukimbilia kujificha vyooni na kuacha kaunta zao.
 
Investigation inatakiwa ifanyike!! huenda kukawa na kundi ya watu nyuma yake waliokuwa wanahusika zaidi na wengine huenda walikuwa ndani ya bank, kijana aliporusha jiwe wateja wakatafaruki na wenye dili kumaliza mission kiulainiiiiiiiiiiiiiiii.

Matatizo kama haya yanatakiwa taasisi huru kama NCIS (National Criminal Invistigation System). Lakini kwa nchi yetu, itachukua miaka mingi kufikia hiyo hatua!
 
Wagonjwa wa akili wanapaswa kuwa katika taasisi maalum za tiba na sio kuachwa wakizurura mitaani.
Wizara ya Afya kwa kweli inatakiwa kulipa kipau mbele jambo hili.
 
Investigation inatakiwa ifanyike!! huenda kukawa na kundi ya watu nyuma yake waliokuwa wanahusika zaidi na wengine huenda walikuwa ndani ya bank, kijana aliporusha jiwe wateja wakatafaruki na wenye dili kumaliza mission kiulainiiiiiiiiiiiiiiii.

Matatizo kama haya yanatakiwa taasisi huru kama NCIS (National Criminal Invistigation System). Lakini kwa nchi yetu, itachukua miaka mingi kufikia hiyo hatua!

Hili nalo neno, kuna kila aina ya ukweli kwa speculation yako, haingii akilini kuwa wakati watu wengine wanakimbia wengine wawe na ujasiri wa kuchukuwa pesa na nyaraka za wenzao, unless ni calculated move. Kama ni punguani kwanini aje kurusha mawe kwenye jengo hilo tu wakati yapo majengo ya aina hiyo (ya vioo) maeneo hayo, unless alikuwa anamrushia mtu aliyemuuzi aliyekuwa karibu na benki hiyo, otherwise uchunguzi wa kina ufanyike usikute ndo njia mpya ili tuanze kukombwa vitu kiulaini na wajanja kwa jina la upunguani.
 
Inawezekana huyu kijana hajafanya hivyo kwa bahati mbaya!

Inawekana kuna watu wamemtuma ili waone watu wanavyo-react au police wanavyorespond incase mashambulizi yakianzia nje.

Nashauri police wamhoji vizuri huyo kijana.

I don't think aliamua tu kufanya hivyo.
 
Picha za cctv zitatuambia mengi, tusijeambiwa video camera zilipata hitirafu, bongo zaidi ya uijuavyo..................................
 
Watu wamechoka na maisha haya kila waonekanapo wanaonekana kama hawana akili timamu huku ni kuchanganyikiwa na maisha anahitaji cancelling huyu!
 
mbona hujaweka picha ya vioo vilivyo vunjwa?hiyo ya police kuweka watu chini ya ulinzi ni kitu cha kawaida.
 
wakija vijana wa kaz(majambazi) kuchukua hela zao benki hawa maaskari wala huwa hatusikii kama walikuwa karibu na eneo la tukio! kwanza askari hana ruhusa ya kumpiga mtuhumiwa ambaye tayari yuko chin ya ulinzi kwa sababu endapo atamuua atapata wapi habari za mtandao mzima?! wanadhani ni sifa kumbe hawana lolote! wanashindwa kudhibiti majambazi ambao kila siku wanapiga matukio ya ukweli wanakuja kumalizia nguvu zao zote kwa haka kateja!
 
Kijana-1.JPG



Huyu polisi kwa nini anampiga teke wakati wamekwisha mdhibiti? Hii ni abuse. Vile vile inaonekana hawana hata bangili hawa warudi tena wakafanye mafunzo.
 
kwa nini askari amempiga huyu kijana? Hawa askari wetu inabidi wapewe darasa. huyu mkuu wa polisi (jina nimesahau) Atembee aone polisi wa wenzetu wanavyofanya kazi
 
Sioni sababu kabisaaaaaaaa kwa polisi hao kumpiga mtuhumiwa mbaye tayari wamesha mdhibiti. Huo ni uvunjifu wa sheria unaofanywa na Jeshi la Polisi.

Naomba hatua zichukuliwe dhidi ya polisi hao kwa kitenda walichokifanya.
 
Ha ha! Watz kweli waoga! Hapo kama iraq au afghanstan watu wanaendelea na business zao.
 
Shit.... Uonevu mtupu. Polisi elimu ndogo, ufundi sifuri, maadili ziro rushwa na ghadhabu kibao. Tumewazoea ndivyo walivyofundishwa na vilaza wao. Tena askari wa hivyo atapendwa sana na bosi wao. Huyu kijana amechoka na serikali mbovu maisha magumu na wawekezaji wabovu kama hao mara atm hazina mtandao.... Wakati imeandikwa 24hrs. Kaka watwange mawe tu wala sishangai.


Atm 24 hrs is it true???????, mara mtandao, mara haina hela, mara umeme sasa kwanini msipigwe mawe shit.....
 
je wakati polisi wanaanza kumkamata mtuhumiwa alifanya vurugu ... na kama walimdhibiti kulikuwa na ulazima wa kumpiga au kuendelea kumpiga??? je alikuwa na siraha yoyote???
 
Sasa kwanini polisi anampiga mtu ambaye teyari yupo chini ya ulinzi?

"You've the right to remain silent, Anything you say or do can be and will be held against you in a court of law, You have the right to speak to an attorney, If you cannot afford an attorney, one will be appointed for you. Do you understand these rights as they have been read to you?"


Sasa hapo sijui hicho kipengele was applicable? au ilikuwa ni kupige kwanza ndio nikusomee kipengele hicho

My Take:

Hicho kipengele kwa huku kwetu hutumika hivi

"You've the right to remain silent, Anything you say or do can be and will probably be held against you in a court of law, You have no right to speak to an attorney, Your not allowed to afford an attorney but of course the government will be appoint one for you. Do you understand these rights as they have been read to you?"
 
huyo askari anavyompiga teke namna hiyo utadhani si binadamu halafu hana hata silaha huyo jamaa. ndio maana sishangai ninaposikia mtu kafa kabla hata ya kufikishwa mahakamani au kuhojiwa vya kutosha kiasi kwamba tunapoteza taarifa ambazo zingeweza kusaidia.
 
Back
Top Bottom