Polisi wakiwa kazini benki ya CRDB

Yote mliyoyaongea yana MANTIKI. Lakini mmesahau kuongelea juu ya afya za hao askari kutokana na kwamba huyo VICTIM wamemtoa damu. Me nahoji usalama wao kama damu ya huo wanayempiga ina VVU. Ikizingatiwa kwamba kama ni teja kama inavyosemekana na wanavyo share mabomba ya sindano huko kwenye uteja wao,kuna usalama hapo kama incase hao maaskari wana aina yoyote ya mikwaruzo!!! This is a challenge,and next time they should think aftermath of what they do!!
 
Duu, umeona teke lile, hawa jamaa wanajua hata maana ya haki za binadamu?
 
Polisi waatakiwa kutumia nguvu kiasi (reasonable force) katika kum arrest mhalifu, jee hawajui ama ndio....
 
hili tatizo la vyombo vyetu vya usalama kutumia nguvu kupita kiasi sasa naamini ni uzembe wa serikali maana kama govt ingekuwa na nia haya mambo yasingekuwepo na kwa style hizi hizi watu wengi sana wamepoteza maisha mikononi mwa polisi
 
Sasa kwanini polisi anampiga mtu ambaye teyari yupo chini ya ulinzi?

Unajua mbuzi ni mbuzi ata ukimlaza kwenye kitanda atamwaga maji na kudondosha changarawe hapo. Hawa police wamezoea hivyo. Itatuchukua muda kuibadirisha hali hii ya uvunjaji sheria. Hivi wanajua kuwa watoa hukumu kabla ya mahakama?

Ata ukituhumiwa bora ukimbilie msituni kuliko kukutana na hawa jamaa maana huwa ni nani katangulia alafu anayefuatwa ni kupingwa virungu, mitama nk!

Kuna kibaka mmoja MZ stand alikimbilia choo cha kulipia na akawa anawamwagia watu wenye hasira kinyesi na hakuna aliyemfuata. Polisi wanatoa roho kabla ya hukumu alafu wanakuja na porojo ya akari jamii!
 
Kijana-1.JPG

Kijana-3.JPG

Kijana-2.JPG

Kijana-4.JPG


TAFRANI imetokea katika Benki ya CRDB, tawi la Azikiwe,baada ya kijana mmoja aliyehisiwa kuwa jambazi kurusha mawe kwenye vioo vya benki hiyo na kusababisha wateja kukimbia ovyo wakidhani wamevamiwa. Tukio hilo lilitokea jana mchana, ambapo kijana huyo anayedhaniwa kuwa akili yake imeathirika kwa kubuia dawa la kulevya 'Teja' kurusha mawe kuelekeza kwenye jengo hilo na kuvunja vioo.

Baadhi ya wateja walianza kutimua mbio kutoka nje huku wengine wakilala chini kuhofia maisha yao. Baada ya kuona hivyo, Polisi waliokuwa kwenye lindo la benki hiyo, walifyatua risasi juu wakidhani majambazi wamevamia benki hiyo. Lakini baada ya muda walimuona kijana huyo aliyekuwa katikati a Barabara ya Azikiwe karibu na kituo cha Daladala cha Posta Mpya, akiendelea kurusha mawe.

Polisi walimuendea na kufanikiwa kumdhibiti na kuanza kumpatia mkong'oto wa nguvu, huku wanachi wenye hasira wakitaka nao waruhusiwe kumwadhibu. Ndani ya benki hiyo hali ilikuwa shaghalabaghala, kwani mitungi ya maua na baadhi ya nyaraka zilitawanyika ovyo, huku wakioneakana baadhi ya wateja wakiwa wamezirai na wengine wakilia baada ya kupotelewa na nyaraka muhimu za benki vikiwemo kadi na fedha taslimu. Wakati tukio hilo ilitokea, pia hali haikuwa nzuri kwa wafanyakazi wa benki hiyo, kwani baadhi walisikika kuwa walipatwa na hofu kubwa kiasi cha baadhi yao kukimbilia kujificha vyooni na kuacha kaunta zao.


Kama kuna mwanasheria atusaidie kuwafungulia mashitaka hawa jamaa tutachangia gharam maana tukiwakenulia watazidi kuharibu na kusababisha mauaji na uremavu kwa wanachi hasa wale ambao hawajathibitika kuwa na hatia. Sasa kama hapa ni Dar huku nyumbani Rubya Muleba wanachi siwanachinjwa? Ebu angalia walivyotoa macho!
 
Nina hasira mimi sanaaaaaa. Ngoja niondoke kwenye post hii. Nakumbuka mauaji ya Arusha.....
 
Picha mnato peke yake hainikidhi kunipa uwanja mpana wa kuliongelea tukio hili:Video ingenifanya niwe huru zaidi juu ya kulichanganua kwa mapana suala hili japo Picha hii imenifanya nitoe maoni haya
1.kwanza nashukuru kwa media kuweza kufichua hili na ningependa waongeze juhudi zaidi kufichua Police Brutality na excess use of force ya police.Wadau wa Human rights,wanasheria,watunga sheria,na mahakama hii ni changamoto ambayo inakuwa kwa kasi na haijapewa mtazamo unaostahili kwa nafasi zetu na nyakati zetu tulipe angalizo suala hili.

2.Kwako kamanda Mwema kwanza heshima mbele,vijana wako hawana mvuto kwa jamii na ndio chanzo kikuu cha kushindwa kwa mtazamo wako mzuri wa Polisi jamii (community policing) ambao ungeongeza ufanisi wa jeshi lako. Kunyang'anya haki za raia, unyama kwa raia, use of excessive force dhidi ya raia na kutosimamia misingi ya kazi na haki kamwe polisi jamii haitafanikiwa.
Nimefuatilia juu ya ufahamu wa sera la utumiaji nguvu (Law enforcement use of force policy) na kugundua kuwa ni mojawapo ya topic ndogo inayofundishwa CCP ktk somo la Police General duties,nashauri hapa ufanye mabadiliko makubwa kwani kwa dunia ilipo sasa hli ni somo linalojitegemea sana na ndio muhimili wa utendaji kazi wa vijana wakiwa mtaani.Mkuu badili silabi ya mafunzo iende na wakati vijana wafanye mafunzo mara kwa mara hasa hili la use of force ambalo ndio anguko lao kuu kwani vijana wengi wanaongozwa na common sense zao ktk kufanya maamuzi (wkt common sense is not common thing) na hivyo wanajikuta kufanya na maamuzi kinyume na sheria,katiba na misingi ya haki za binadam.

Only good training and proper police practice ndio siri ya kutawaandaa vijana kufanya kazi sahihi.

Boresha maslahi yao na promote their walfare,Polisi ni chanzo kizuri cha pato la taifa pia na hivyo wakisimamiwa vema wanaweza kuinua pato la taifa,kuboresha mazingira yao ya kazi na maslahi yao bila kuiumiza hazina.kwa hili ukiamua utaweza kwani huitaji extra resource sababu tayari unazo mkuu.Baada ya hapo sasa ulete polisi jamii uone kama itashindwa.

kwa wadau ninachokiongea juu ya use of force police nina maana hii
[h=1]Police Use of Force[/h] Police enforce social order through the legitimized use of force. Use of force describes the "amount of effort required by police to compel compliance by an unwilling subject" [1]. The levels, or continuum, of force police use include basic verbal and physical restraint, less-lethal force and lethal force.

The amount of force police use should be the minimum amount needed to eliminate the threat presented, thereby minimizing the risk and severity of any injury that may occur.

Police should also:


  • Ensure that those injured receive medical aid.
  • Ensure that the family of any injured person is notified.
Officers receive guidance from their individual agencies, but no universal set of rules governs when officers should use force and how much.
The level of force an officer uses will vary based on the situation. Because of this variation, guidelines for the use of force are based on many factors, including:


  • The police officer (department's) experience
  • Available law enforcement technologies and training.
  • The complex relationships that may exist between the police and citizens in a given jurisdiction.

3.Kwa mfumo uliopo sasa huyu kijana kupata haki yake ya kisheria juu ya police brutality na excess use of force against him ni ngumu sana sababu waliompiga ni polisi,Pf 3 atapewa na polisi,ataenda kufungua mashitaka polisi,uchunguzi utafanywa na polisi,kibaya zaidi ni kuwa hata mwendesha mashitaka nae ni polisi.
 
polisi wetu vilaza wa sheria na haki za binadamu. Siwapendi kama nini sijui!
 
Back
Top Bottom