Polisi wakamatwa na meno ya ndovu

Polisi wakamatwa na meno ya ndovu

Lukolo

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
5,143
Reaction score
3,209
Kisarawe. Watu tisa, wawili kati yao wakiwa polisi wa Kituo cha Oysterbay, Dar es Salaam wamekamatwa wilayani Kisarawe, mkoani Pwani kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha meno 70 ya tembo (kilo 305) kinyume na sheria.

Meno hayo kwa hesabu za kawaida ni sawa na tembo 35, wameuawa na kwamba thamani yake ni zaidi ya Sh850 milioni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei, alisema watuhumiwa hao walikamatwa Kisarawe usiku wa kuamkia jana na askari wa wanyamapori waliokuwa kwenye operesheni.

Matei alisema watuhumiwa walikamatwa kwenye kizuizi cha Kauzeni, Kata ya Vikumburu, Tarafa ya Chole na kwamba, walikuwa wakisafirisha meno hayo kwa kutumia gari aina ya Toyota Surf kwenda Dar es Salaam.

"Ni kweli wamekamatwa watu tisa, wawili wakiwa ni Polisi wa Oysterbay, nimepata hiyo taarifa na nimeshamtuma Ofisa Upelelezi Mkoa (RCO) kuwaleta Kibaha," alisema Matei.

Kamanda Matei alitaja watuhumiwa kuwa ni mkazi wa Tandika Yombo, mkazi wa Kinondoni Studio, mkazi wa Tandika hewa, mkazi wa Mbagala Charambe na mkazi wa Chanika. Pia, polisi wawili wanaodaiwa wa Kituo cha Oysterbay.

Wakati polisi hao wakikamatwa, Idara ya Magereza imetangaza kuwafukuza askari wanne wanaodaiwa kukamatwa wakiwa wamepakia meno ya tembo Julai 23, mwaka huu.

My TAKE: Jeshi la polisi la sasa limekosa uhalali wa kuwa chombo cha ulinzi na usalama wa watu na mali zao. Ni wakati mzuri sasa wa kulivunja na kuliunda upya.

 
Hii dili imebuma na hao wameangushiwa jumba
Kuna zaidi ya hilo, mil 850? Eti dili la koplo? Thubutu!
 
PoliCCM bana!
Policcm na Nyara zetu; Policcm na kichwa cha mtu; Policcm na bangi; policcm na kitu cha ncha kali; Policcm na mabomu; Policcm na utekaji wa raia; Poiliccm na mauaji ya raia!!
 
duuh, deal imeliki. hiyo hela ni ya ukweli. wangefanikisha kufikisha mzigo naamin hata kazi wangeitosa
 
Nikisema kinana nyie mnamalizia....haya twende.....KINANAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA!!!!
 
Kuna jamaa alisema humu jamvini kuwa siku hizi polisi ndio wezi sasa sisi raia tutaiba wapi?
 
Dili la Kinana hilo aliye wakamata atahamishwa kazi nakupelekwa Sumbawanga
 
We are doing too much for our country to handle
Nchi inatia aibu....hivi ni nini ambacho we are doing right and in a right way? hebu mtu aniambie nipunguzie hasira
 
Tena??aisee nimeamini kweli ccm they dont deserve to be in power again,mara huku kinana kule ma pusher...bado tu mwema hajajiudhuru?
 
Hahahaa! Teh,teh. POLISI WAKAMATWA NA MENO YA NDOVU. Dah ni baadhi ya vitu adimu vinavyopatikana jf pekee.
 
  • Thanks
Reactions: K'T
PoliCCM bana!
Policcm na Nyara zetu; Policcm na kichwa cha mtu; Policcm na bangi; policcm na kitu cha ncha kali; Policcm na mabomu; Policcm na utekaji wa raia; Poiliccm na mauaji ya raia!!
Naona ile timu ya buku7 imekua adimu sana
kwenye huu uzi jamani Hamiiii
 
Back
Top Bottom