Baada ya kutafakari mauaji ya mbwana kule igunga, mauaji ya mwenyekiti CDM Usa river, mauaji ya wale vijana wa Arumeru na kukatwakatwa mapanga wabunge wa CDM mwanza. Nimegundua kuwa kukaa kimya kwa Mbowe na Slaa ktk mambo mazito kama haya kutawagharimu nafasi zao za uongozi huko mbele. Sioni kama wako serious hawa viongozi wakuu wakati wanajua wanaweza kuandaa maandamano yatakayoweza kubadili sura ya mchezo. Nadhani wanatakiwa waoneshe kuwa wanajali maisha ya wafuasi wao na sio kwenda kufanya kama mojawapo ya ajenda ktk mikutano ya hadhara kama alivyoongelea slaa kule Geita kuhusu wabunge amesahau kabisa kama kuna wengine wameuwawa kutokana na uaminifu wao kwa chadema.