Polisi waanza kutekeleza adhabu "kali" kwa madereva wanaovamia barabara za mwendo kasi

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
Jeshi la Polisi limeanza kutekeleza mtindo mpya wa kuwaadhibu madereva wote wanaotumia barabara ya mabasi ya mwendo kasi na kuvunja sheria za Barabarani.
Mtindo huo wa adhabu unajumuisha kumkamata dereva,kumuandikia makosa na kulipa faini na pia kumpoga picha na kuzisambaza mitandaoni ili wahusika waone "uchungu" wa kosa na wengine wajifunze kupitia adhabu hizo

Hii imekuwapo hata kabla ya Rais JPM kutoa pendekezo la askari wa usalama barabarani kukamata magari yanayovunja sheria ya njia za mwendo kasi,kuyapeleka polisi na kufungua magurudumu.

Kikubwa kilichojitokeza ni kuwa wengi wa wavunjaji wa sheria hizo ni "wasomi" na watumishi wa mashirika ya umma na binafsi ambao ilitegemewa ndio wenye uelewa mkubwa na hivyo kuheshimu sheria za barabarani

image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
 
Nashauri kuwepo na mfanano (uniformity) katika hizo karatasi au mabango ya makosa ili wakosaji wote watendewe sawa. Mfano wakati kuna karatasi za baadhi ya wakosaji zina hadi imani yake kidini, kazi yake na pia kabila lake zingine hazina hivyo vipengele. Kuepuka hilo karatasi zenye mfanano zichapishwe kisha ibaki tu kwa wasimamizi wa usalama barabarani kujaza maelezo ya mkosaji.
 
Jeshi la Polisi limeanza kutekeleza mtindo mpya wa kuwaadhibu madereva wote wanaotumia barabara ya mabasi ya mwendo kasi na kuvunja sheria za Barabarani.
Mtindo huo wa adhabu unajumuisha kumkamata dereva,kumuandikia makosa na kulipa faini na pia kumpoga picha na kuzisambaza mitandaoni ili wahusika waone "uchungu" wa kosa na wengine wajifunze kupitia adhabu hizo

Hii imekuwapo hata kabla ya Rais JPM kutoa pendekezo la askari wa usalama barabarani kukamata magari yanayovunja sheria ya njia za mwendo kasi,kuyapeleka polisi na kufungua magurudumu.

Kikubwa kilichojitokeza ni kuwa wengi wa wavunjaji wa sheria hizo ni "wasomi" na watumishi wa mashirika ya umma na binafsi ambao ilitegemewa ndio wenye uelewa mkubwa na hivyo kuheshimu sheria za barabaraniView attachment 353176View attachment 353177View attachment 353178View attachment 353179View attachment 353180View attachment 353181View attachment 353182View attachment 353183View attachment 353184
 
Back
Top Bottom