Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Jeshi la Polisi lingependa kutoa ufafanuzi kuhusiana na Waandishi wa Habari wawili waliokamatwa na kushikiliwa kwa mahojiano na kukamilisha ukusanyaji wa vielelezo ambavyo vilikuwa vimesha kusanywa toka walipoanza kufuatilia kutokana na tuhuma zinazowakabili.
Waandishi hao ni Baraka Lucas anayefanya kazi na Jambo TV na Ezekiel Nicco Mollel anayefanya kazi na Manara TV.
Sababu za kukamatwa mbali na kufanya kazi na Vyombo vinavyojulikana na vilivyosajiliwa wanatuhumiwa kuendesha Online Tv zao binafsi ambazo hazijasajiliwa kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 4 (1) za Kanuni za Maudhui Mtandaoni za Mwaka 2020 kama zilivyofanyiwa marekebisho 2022. Kanuni hizo zimetolewa chini ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta.
Soma Pia: Waandishi wa habari wa Jambo TV na Manara TV washikiliwa Arusha
Uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili unakamilishwa ili hatua zingine za kisheria zifuatwe kwa wakati.