Mie sikumoja pale Salender bridge muda wa saa moja na nusu usiku nilipita nikiwa gari la mwisho na taa zimekuwa nyekundu, polisi akiwa katikati ya barabara, tena amelewa. Akanisimamisha kwa nini napita na taa nyekundu, nikamjibu bwana, wewe unafanya nini hapa katikati kwenye taa kama huongozi na taa zinafanya kazi? Mie nilidhani tunaongozwa na wewe sio taa. Tukabishana, mwishowe akaniambia haya hebu niachie kitu kidogo uondoke!