Mie ni mmoja watumiaji barabara ya Kilwa! Kikubwa kinachokera kwa sie wafanyakazi na watumiaji wa barabara hiyo tunakwerwa na hatua za ufungaji barabara kwa asubuhi bila kutupatia muda rasmi niwakati gani barabara inafungwa kwa wanaotoka mjini! Kero Kubwa ni nyakati za joini barabara inafungwa muda Wowote na hakuna muda Maalum! ombi langu kwa Kamanda Mpinga, weka ratiba tujue barabara ya Kilwa asubuhi inafungwa saa ngapi kwa wanaotoka mjini na kariakoo na vivyo hivyo barabara hiyo nyakati za joini itafungwa kuanzia saa ngapi na kwa muda gani kupisha Magari yanayotoka mjini.