Polisi: Ukaidi wa CHADEMA ndio chanzo cha kifo cha Aquilina

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Haya maajabu ya Jeshi la Polisi hivi yataisha lini? Hivi chanzo cha maandamano ya CHADEMA ilikuwa ni nini? Hivi mkurugenzi na NEC wanaachwa ili iweje?

Nimesikia kamanda akisisitiza vyama vya siasa kufuata sheria. Sheria iliyopo inaruhusu vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu kufanya mikutano na maandamano ya kisiasa. Nadhani wahusika mmesikia.
 
siku tutakapoacha kuwapa nafasi za kujiunga jeshi la polisi vijana waliopata ZERO kidato cha NNE ndio huu ujinga utaisha!
 
Nimesikia kamanda akisisitiza vyama vya siasa kufuata sheria. Sheria iliyopo inaruhusu vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu kufanya mikutano na maandamano ya kisiasa. Nadhani wahusika mmesikia.
Maandamano gani saa mbili usiku?
 
Siyo lazima wagonjwa wote wa akili kupimwa hospitalini ili wagundulike ni wagonjwa wa akili. Wengine wanathibitika kwa kusikiliza tu yale wanachoongea.
 
Endeleeni na hayo mnayofanya, damu ya wasio na hatia iliyomwagika chini itawafuata popote mwendapo. Kwa kuwa Mungu yupo atahukumu kwa haki, hayumbishwi na vyeo, vyama, umaarufu, fedha na kiburi ya watawala wa nchi hii
 
Haya maajabu ya Jeshi la Polisi hivi yataisha lini? Hivi chanzo cha maandamano ya CHADEMA ilikuwa ni nini? Hivi mkurugenzi na NEC wanaachwa ili iweje?

Jeshi la polisi la Tanzania mwanzoni lilionekana kama linatia aibu hivi, lakini sasa ni dhahiri linatia huruma sana ! Linaweza kutumikishwa hata na mjumbe wa nyumba 10 wa ccm na likatii !
 
Hivi polisi wetu wapo kulinda raia au utawala? Maana hata wakifanya makosa polisi wanajifanya vipofu. Lazima wamtafute wa kumsingizia
 
Siku hizi ina maana polisi Hawana mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kutawanya waandamanaji? Wameona ni bora watumie risasi za moto kutawanya maandamano.

Ni Sawa chadema hawakuwa na Kibali cha kuandamana hawakuwa sahihi, sasa wao kutumia risasi za moto kutawanya maandamano yasiyokuwa na kibali na waandamaj hawakuwa na mawe wala siraha yeyote ile kwa maadili yao ni ruksa??

Chadema hawakuwa sahihi, ila polisi wao pia ndyo hawakuwa sahihi kwa 100% wametuulia kijana wetu aliyekuwa na ndoto nyingi za kuzitimiza
 
Back
Top Bottom