Polisi Temeke wakamata 'Panya Road' 18

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
PANYA.jpg

Kwa ufupi
Kamanda wa polisi wa Temeke, Gilles Muroto amesema leo kuwa vijana hao, wanaohusishwa na kundi la Panya Road linalofanya unyang'anyi maeneo ya jiji la Dar es Salaam, walikamatwa jana nyakati tofauti baada ya polisi kuendesha msako wa kuzuia na kupambana na wahalifu.

By Bakari Kiango,Mwananchi bkiango@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi linawashikilia vijana zaidi ya 18 wenye umri kati ya miaka 14 na 20 kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uhalifu katika maeneo ya Wilaya ya Temeke.

Kamanda wa polisi wa Temeke, Gilles Muroto amesema leo kuwa vijana hao, wanaohusishwa na kundi la Panya Road linalofanya unyang'anyi maeneo ya jiji la Dar es Salaam, walikamatwa jana nyakati tofauti baada ya polisi kuendesha msako wa kuzuia na kupambana na wahalifu.

Alisema vijana hao wanatoka maeneo ya Buza Kanisani, Chanika, Yombo Kirakala, Buza Changulu, Yombo Makangawe na moja anayeishi maeneo ya Mwananyamala lakini alikamatwa Temeke.

"Kama Kamanda Simon Sirro alivyosema kuwa ni lazima wahalifu wadhibitiwe katika mko huu. Temeke hatuwez kumwangusha, tunatekeleza agizo lake," alisema Kamanda Muroto.

Alisema vijana hao wanajihusisha na vitendo vya uporaji wa mali mbalimbali kuanzia mitaani, pia kujeruhi watu hali inayosababisha wakazi wa eneo husika kuishi kwa hofu.

Alisema upelelezi ukikamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria.

Wakati huohuo, Kamanda Muroto amesema polisi inashikilia mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 38, mkazi wa Buza baada ya kumkuta na puli 120 za dawa za kulevya aina ya bangi.

Chanzo.Polisi Temeke wakamata 'Panya Road' 18
 
Huko yombo wanakaba hata mchana kweeupeee, ni mji wa zamani ila hauendelea Kuna uwenyeji Sana yombo.
 
Wanaume wa dar wanaporwa na vitoto vya miaka 16

Mkuu kuna sehemu inaitwa yombo njia panda ya mwinyi, pita saa moja tu au kumi na mbili asubuhi alafu ukutane na wenye kazi yao. Ukipambana nao na ukiwashinda leta mrejesho humu. Mimi ni mkazi wa maeneo hayo. Yombo ni chafu sana, tena chafu zaidi ni ya mwanzoni kabla hujafika njia panda ya kitunda.
 
Kuna miaka walikula sana kibiriti hali ikatulia kidogo sasa wameanza tena
 
Mkuu kuna sehemu inaitwa yombo njia panda ya mwinyi, pita saa moja tu au kumi na mbili asubuhi alafu ukutane na wenye kazi yao. Ukipambana nao na ukiwashinda leta mrejesho humu. Mimi ni mkazi wa maeneo hayo. Yombo ni chafu sana, tena chafu zaidi ni ya mwanzoni kabla hujafika njia panda ya kitunda.
True story. Hiyo njia ya kwa mwinyi hadi kilakala ni hatari. Hata hapo relini mpaka taa nyekundu hakufai.
 
Iweje panya kuwadi maarifa bin adam bana?huo ni uzembe sisi huku hawathubutu tunapiga moto
 
taharifa ya kukamatwa tunapewa hakuna mrejesho tena maana wengi si ndio hao wanarudi mtaani mnawakamata kila mara kuna waliofungwa kwa kesi za panya road..
 
Back
Top Bottom