GE2025 Polisi: Paul Chuwa (Kiduku) tunamshikilia kwa tuhuma za makosa ya Kimtandao

GE2025 Polisi: Paul Chuwa (Kiduku) tunamshikilia kwa tuhuma za makosa ya Kimtandao

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,436
Reaction score
5,234
Haya Polisi wanachekesha sana! Yani mpaka watu wapige kelele wao ndio wanatoa kusema wamemchukuwa wao

Na hayo makosa ya kimtandao mbona kama yamekuwa mengi au kisa wanaikosoa serikali?
================

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limetoa taarifa ya kumkamata mtuhumiwa mmoja kwa tuhuma za makosa ya Kimtandao.

‎Taarifa hiyo ya leo Septemba 25, 2025 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, imesema mtuhumiwa huyo anafahamika kwa jina la Paul Chuwa, maarufu zaidi kama "Kiduku" ambaye ni mkazi wa Kijichi Temeke, ambapo taarifa hiyo imesema uchunguzi unakamilishwa na mtuhumiwa atafikishwa kwenye mamlaka zingine za kisheria.

‎"Jeshi la Polisi halitasita kumuhoji na kumkamata mtu yoyote anayejihusisha na tuhuma za kihalifu" imeeleza barua hiyo ya polisi.

Soma Pia: Kiduku Ofisa Ngiri mtumiaji wa mtandao X zamani twitter achukuliwa na watu wasiojulikana

‎Hata hivyo, taarifa hiyo ya Jeshi la Polisi imebainisha kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Septemba 24, 2025, majira ya saa 07:00 mchana, lakini haijaweka wazi aina ya makosa ya kimtandao ambayo yamefanywa na mtuhumiwa huyo.

Screenshot 2025-09-25 185729.png
 
Makosa ya kimtandao jau sana, maana hataa waandaji wa hayo mashataka wanakuwaga shalow sana.. Ni kunyooshana tu 😅
 
Back
Top Bottom