NjalangiJr
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 251
- 88
Salamu wana jamvi,
Nilipata ajali gari kama miezi miwili ilioyopita maeneo ya Msasani. Baada ya gari niliokua nikiendesha kugongana uso kwa uso na gari nyingine, lakini baada ya ajali dereva wa gari nyingine alikimbia na kuacha gari pale barabarani hadi polisi wa usalama barabarani walipofika.
Polisi walipofika na kupima ikaonekana jamaa anamakosa ndio maana akakimbia ikabidi gari zivutwe hadi polisi Oysterbay. Sababu ile gari nyingine ilikua ya kampuni polisi waliniambia nisiwe na hofu sababu wenye gari yao lazima waje mimi niandike maelezo niondoke na kesho yake nirudi kituoni asubuhi ili tufanye taratibu zinazotakiwa pamoja na kuwasilisha documents za gari na bima pamoja na leseni yangu na nikafanya hivyo.
Kilichonishangaza nafika asubuhi naambiwa Jalada limepotea halionekani,nikashinda Oysterbay polisi tokea asubuhi saa2 hadi jioni saa9 kuna afande akaniaelekeza niende kwa mkubwa wao (OCS) nimueleze tatizo,baada ya kumueleza tatizo ikabidi aamuru lifunguliwe jalada upya na mchoro uchorwe tena, ikawa hivyo.
Cha kushangaza polisi wakawa hawafanyi juhudi kumpata mmiliki wa gari ili tujue hatma yangu kama nalipwa au vipi,ikabidi nifanye taratibu binafsi kumtafuta mmiliki wa kampun ya gari na kujifanya mimi ni polisi wa Oysterbay ili kumtisha aje polisi Oysterbay na hapo ilishapita wiki2 inaenda wiki3.
Ndio mmiliki anakuja polisi baada ya kumtisha, nilipo hakikisha kafika polisi sababu alinipigia simu kama yupo Oysterbay anataka kuniona ikabidi nimuunganishe kwa afande ambae ana faili la kesi yangu, huku yeye akiamini mimi ni askari na namkabidhi kwa askar mwenzangu. Nilifanya hivyo baada ya kuona sipati ushirikiano kutoka polisi ili tumpate mtuhumiwa.
Kinachonishangaza jamani tokea nimkutanishe yule mmiliki na afande hakuna kinachojiri nikipiga simu kumuuliza askari kuhusu maendeleo naambiwa faili limeenda kwa mwanasheria wa serikali halijarudi na likirudi litaenda mahakamani kesi iendeshwe iishe ndio uende kudai bima ili gari yako itengenezwe. Na mimi Bima ya gari yangu ni ndogo na yule alienigonga ni kubwa.
Naombeni ushauri wanajamvi.