Polisi na wizi wa Tochi barabarani

Polisi na wizi wa Tochi barabarani

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,775
Reaction score
46,063
Pana wizi wa wazi unaotokea barabarani ambao kama hautapigiwa kelele katu wanaonufaika nao hawata kaa kuusemea.

1. Camera wanazotumia kupima mwendo kwa jina lao tochi zinapima relative speed wala si actual speed ya gari.

Katika hili suala la mwendo kasi zinazosajili with their error margin, huwa inategemea sana pia camera naoyo ilikuwa katika mwendo gani. Hii ni katika hali zote hata kama ni katika kui position kuelekea katika lengo. Kutegemea relative speed hizi camera hizi zinaweza toa matokeo tofauti kabisa na hali halisi.

2. Tabia ya kupiga picha kuonyesha mwendo kasi pasipo na kuonyesha vibao husika vyenye kuonyesha kiwango cha mwendo unaoruhusiwa kwa mjiu wa sheria mfano wa 50km/h. Hakika ni wizi mwingine usio mithilika.

Katika hili pana uwezekano mkubwa picha kupigwa nje ya maeneo yasiyokuwa restricted na speed hizi. Bahati iliyo mbaya Polisi wetu hawa kuwaamini kwenye face value ni bora ya ngamia kupita katika tundu la sindano.

3. Tabia ya kupiga picha hizi za mwendo kasi na kudai kuwa vibao maeneo husika havipo ila ni makazi ya watu ni kasoro nyingine ambayo ni ya kushangaza.

Katika hili ni jambo la kushangaza kwani dereva anaendesha kwa kufuata sheria zinaelekezwa na vibao. Kama vibao hakuna dereva atajua vipi restriction inaanzia wapi mpaka wapi with precision?

Ilikuwa muhimu kuwe na uwazi na haki katika haya.

By the way kwa utaratiu huu kwa ulipaji wa machine mtu ana appeal vipi kama anaona kuwa kuna ukiukaji wa haki katika utozaji faini wa namna hii?

Kwa nini polisi hawaweki hotline kama ilivyo kwa mashirika ya simu ili kuondoa utata kwa wakati kunapotekea ukikwaji wa sheria wa wazi kama hivi?
 
Kwa hili suala polisi wanakosea sana.kwanza wanavizia magari. Kujificha porini. Kuvaa kiraia ili wasionekane. Gari inapigwa tochi nyuma halafu picha inatumwa kwa wassup hamna hata kibao isitoshe huwezi kujiridhisha kama ni kweli ume overspeed.hizi tochi zimekua ni biashara.
 
Sasa hivi kama una safari ya mbali bora usafiri usiku hakuna namna.
 
Ni jambo la kushangaza kuwapa tochi hao
Kwanini wasiweke speed camera tu
Haya mambo hayahitaji watu tena

Wakiweka camera tu bila watu:

1. hizo camera zitapima actual speeds wala si relative speed.
2. Hakika zitapima speed katika marked restricted areas.
3. Hakika zitapma speed katika restricted areas wala si katika fictitious areas kama anavyofanya sasa.

Indeed sense ya haki itakuwapo wala issue za hotline ku resolve uonevu wa matochi tochi haya hautakuwapo.

Ni ukweli usiopingika kuwa haki ni tunda la amani. Kusigina haki huku hakutaendelea unabated milele.
 
Katika hili suala la mwendo kasi zinazosajili with their error margin, huwa inategemea sana pia camera naoyo ilikuwa katika mwendo gani. Hii ni katika hali zote hata kama ni katika kui position kuelekea katika lengo. Kutegemea relative speed hizi camera hizi zinaweza toa matokeo tofauti kabisa na hali halisi.
Mkuu naomba specification za hizo camera na kampuni iliyotengeneza camera hizo...ila nijiweke kwenye mazingira mazuri ya kuchangia hoja yako.
 
Kwa hili suala polisi wanakosea sana.kwanza wanavizia magari. Kujificha porini. Kuvaa kiraia ili wasionekane. Gari inapigwa tochi nyuma halafu picha inatumwa kwa wassup hamna hata kibao isitoshe huwezi kujiridhisha kama ni kweli ume overspeed.hizi tochi zimekua ni biashara.
tunaibiwa sana aisee, kuna siku barabara ya moro dar, walinisumbua sana, hakuna kibao huku naambia nime overspeed
 
Wakiweka camera tu bila watu:

1. hizo camera zitapima actual speeds wala si relative speed.
2. Hakika zitapima speed katika marked restricted areas.
3. Hakika zitapma speed katika restricted areas wala si katika fictitious areas kama anavyofanya sasa.

Indeed sense ya haki itakuwapo wala issue za hotline ku resolve uonevu wa matochi tochi haya hautakuwapo.

Ni ukweli usiopingika kuwa haki ni tunda la amani. Kusigina haki huku hakutaendelea unabated milele.
Umeandika ukweli usiopingika ila nashangaa kwa nini wanalazima mfumo huu ambao ni kuibiana dhahiri kabisa.

System yote ni mbaya upande wa barabara hata sign post hazipo sehemu nyingi hivyo kusababisha uonezi kwa madereva.
Ajali nyingi zinatokea kwa ubovu wa system
Kweli tunataka barabara ziwe safe lakini hii sio njia sahihi
Nimekuelewa vizuri sana
 
Mkuu naomba specification za hizo camera na kampuni iliyotengeneza camera hizo...ila nijiweke kwenye mazingira mazuri ya kuchangia hoja yako.

Mkuu haihitaji specs za camera kufahamu kuwa wanaiba. Principle ya ufanyaji kazi wa camera hizi upo katika very elementary physics.

Waweza ona kwenye link hii kuwa kinachopimwa ni relative speed kutegemea nini kinatembea yaani gari, camera au vyote:



Kumbuka kama camera haiko 100% stationary (absolute zero speed) tunaibiwa sana na tumeibiwa sana kwani wanachopima ni relative speed baina ya hivyo viwili target na camera nini unapata yategemeana na speed ya camera pia (hii ikiwa hata kwenye positioning pia). Pana haja ya kuwafikikisha hawa jamaa kwenye mahakama huru. Hawa wanapaswa kurejesha pesa zote walizokwiba kwa mpangilio uliopo sasa hivi vinginevyo chagizo zao za kutaka kuombewa maana hakuna mbingu zitakazowasikiliza.
 
Last edited:
Back
Top Bottom