Polisi na serikali raia na Mungu wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi na serikali raia na Mungu wao

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by potash, May 20, 2011.

 1. p

  potash Member

  #1
  May 20, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Juzi tu raia walimwua askari polisi mmoja huko Tabora na sauti za kikubwa zikasikika na walifika eneo la tukio bila kuchelewa na kutoa kauli kali sana. Kabla ya hapo mashamba ya wawekezaji (Wakoloni wa kisasa) yalichomwa moto kule Mbulu na serikali ilituma mawaziri sita kwenda kushughulikia suala hilo, si haba juzi tu mkoloni akamchoma moto raia pale pembezoni mwa ikulu (kigamboni) Kova akasikika na kauli zilizoishia hewani na mtawala mmoja wa zamani pia akasikika akisema kuwa adhabu pekee iliyomfaa bepari yule ni kufukuzwa nchini ndani ya masaa ishirini na nne.

  Isitoshe raia sita wameuawa huko Nyamongo viongozi hawaonyeshi kuwajibika juu ya hili. Rais anapanda ndege na kuelekea windhoke kujadili ya wengine.

  Kagasheki anaongelea ofisini, nahodha hasikiki kabisa. Na isitoshe Kagasheki anatoa majibu ya kubuni kama vile kawekewa nta pale ofisini kwake asibanduke.

  IGP Mwema hasikiki, ok kusema kuwa mashamba ya wawekezaji na wawekezaji wana thamani kuliko watanzania wanaofanywa watumwa nchini kwao? Polisi wa tanzania wanalinda raia na mali zao au wakoloni na mali zao?

  CCM hili ni gamba na halitavulika kwa maneno mpaka mchemshwe jikoni na maji ya moto.
   
 2. kibakwe

  kibakwe Senior Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wanataka kumaliza wapiganaji pamoja na raia wanaodai haki zao ambazo zipo mikononi mwa wenye MAGAMBA MAGUMU
   
Loading...