Juzi tu raia walimwua askari polisi mmoja huko Tabora na sauti za kikubwa zikasikika na walifika eneo la tukio bila kuchelewa na kutoa kauli kali sana. Kabla ya hapo mashamba ya wawekezaji (Wakoloni wa kisasa) yalichomwa moto kule Mbulu na serikali ilituma mawaziri sita kwenda kushughulikia suala hilo, si haba juzi tu mkoloni akamchoma moto raia pale pembezoni mwa ikulu (kigamboni) Kova akasikika na kauli zilizoishia hewani na mtawala mmoja wa zamani pia akasikika akisema kuwa adhabu pekee iliyomfaa bepari yule ni kufukuzwa nchini ndani ya masaa ishirini na nne.
Isitoshe raia sita wameuawa huko Nyamongo viongozi hawaonyeshi kuwajibika juu ya hili. Rais anapanda ndege na kuelekea windhoke kujadili ya wengine.
Kagasheki anaongelea ofisini, nahodha hasikiki kabisa. Na isitoshe Kagasheki anatoa majibu ya kubuni kama vile kawekewa nta pale ofisini kwake asibanduke.
IGP Mwema hasikiki, ok kusema kuwa mashamba ya wawekezaji na wawekezaji wana thamani kuliko watanzania wanaofanywa watumwa nchini kwao? Polisi wa tanzania wanalinda raia na mali zao au wakoloni na mali zao?
CCM hili ni gamba na halitavulika kwa maneno mpaka mchemshwe jikoni na maji ya moto.