Polisi mtwara wakimbia makazi

Polisi mtwara wakimbia makazi

Obesity

Senior Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
111
Reaction score
46
SHINIKIZO la wananchi mkoani Mtwara kutaka gesi isitoke mkoani humo, limesababisha polisi takriban 50 kuzikimbia familia zao baada ya kutishiwa maisha na wananchi.

Habari zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Maria Nzuki zimeeleza kuwa polisi hao ambao wengi wao ni wale wanaoishi mitaa mbalimbali mjini humo, wamehamia kambini kutokana na kutishiwa maisha na wananchi kwamba watawadhuru wao na familia zao.

Habari hizo zilieleza kuwa, vurugu zilizotokea Januari 25 na 26, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu wanne huku jengo la Mahakama ya Mwanzo na nyumba zikiwamo za wabunge kuchomwa moto na nyingine kuharibiwa vibaya, ni moja ya sababu zilizowatisha polisi hao.
"Wamerudi kambini kwa sababu ya kutishiwa ila ni baadhi ya askari, siyo wote," alisema kamanda huyo.

Juzi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema hasira za wananchi hao ni kudhani kuwa gesi hiyo itapelekwa wilayani Bagamoyo nyumbani kwa Rais Jakaya Kikwete.
Alisema pia mpasuko ndani ya CCM mkoani humo na harakati za kisiasa ni sababu nyingine zilizochochea mgogoro h

Hata hivyo, Kamanda Njuki alisema hana idadi kamili ya askari waliokimbia makazi yao huku akifafanua kuwa mambo yatatulia mkoani humo ikiwa Serikali itatekeleza ahadi zake.
"Serikali inatakiwa kutekeleza ahadi zake ilizozitoa kwa wananchi ili kuweka hali shwari, lakini pamoja na hayo sisi tutaendelea na ulinzi kuhakikisha kuwa kila kitu kinakwenda sawa na hali inakuwa shwari," alisema Njuki.

Alisema baadhi ya wananchi wamekuwa wakiwatisha polisi hao na kutokana na hali hiyo imeonekana ni vyema waende kambini.

Askari wengi waliokimbia nyumba zao ni wale ambao makazi yao yanafahamika na wananchi ambao wakati wa vurugu hizo, walikuwa miongoni mwa askari waliokuwa waki zituliza. Inaelezwa kwamba wapo polisi zaidi ya 40 ambao hawaonekani mtaani na hata katika nyumba wanazoishi.

"Hivi sasa hawapo, si unaona mji ulivyokuwa mweupe, watu wana hasira na wanataka gesi isitoke, kwa hiyo hata wakimwona polisi wanaweza kumfanya lolote," alisema mtoa habari ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini na kuongeza:

"Wananchi sasa wamekuwa kitu kimoja, wameweka siasa na tofauti zao nyingine kando kutaka gesi iwanufaishe, ila binafsi naomba jambo hili limalizike kwa amani."

Chanzo:gazeti la mwananchi
 
Nadhani huu mwanzo mzuri wa mapinduzi ya kifikra. Maana polisi wetu licha ya kukabiliwa na tuhuma za kuua watu wasio na hatia wamekuwa wakitumika kama nepi bila wao kujitambua. Wakati wao wakikimbia familia zao wale waliofaidika na gesi wako wanatanua na wake na waume zao wakati wao wanawindwa kama sio kutanuliwa na mahawara. Mkome kutumiwa kama vile hamna akili nyie polisi.
 
Plato aliwaweka polisi na jeshi ktk kundi gani? Tukumbushane. Wanasiasa (a very small group), utumia polisi/jeshi kujinufaisha. Wao uagiza 'kamata'! na kazi ya awajamaa nikukamata. ktk mfumo usio na haki, aliyekamatwa ufikishwa mikononi mwa jaji mteuliwa na mkuu wa kaya...Hapo haki ubaki ni historia kwa mkamatwa. Tanzania my beloved country!
 
Hii nayo ni moja ya habari za uchochezi na tuwe makini na habari kama hizi!
 
Mfumo wa Kipolisi unarahisisha wao kutumika thubutu JWTZ!

Nidhamu za kipolisi hata diwani wa CCM ni kama bosi wao.
 
Hii nayo ni moja ya habari za uchochezi na tuwe makini na habari kama hizi!
Hata kamanda wa polisi amethibitisha, wewe unasema ni uchochezi... Tupe basi habari yako ya uhakika!!
 
Hii nayo ni moja ya habari za uchochezi na tuwe makini na habari kama hizi!

Wale waliokuwa wakiishi Mwembechai zilipotokea vurugu walikuwa wanavalia uniform kwenye daladala. Hii ni kweli na sio uchochezi. Katika akili ya kawaida lazima wakimbie kwani bunduki wanaacha kituoni.
 
Ndo wajifunze kuishi na watu, wewe umpige mtu virungu mchana kumbe umepanga kwenye nyumba yake na usiku unaenda kulala, aisee hata kama ni mimi nakutimua. Sasa mnaishi mtaa mmoja then unambutua halafu badaye iweje?
 
Nadhani huu mwanzo mzuri wa mapinduzi ya kifikra. Maana polisi wetu licha ya kukabiliwa na tuhuma za kuua watu wasio na hatia wamekuwa wakitumika kama nepi bila wao kujitambua. Wakati wao wakikimbia familia zao wale waliofaidika na gesi wako wanatanua na wake na waume zao wakati wao wanawindwa kama sio kutanuliwa na mahawara. Mkome kutumiwa kama vile hamna akili nyie polisi.

Hiyo lugha uliyoitumia ya kutumika kama nepi sidhani kama ni sahihi. Kadiri unavyoweza jitahidi kitumia lugha zisizoudhi wengine mawazo yako yanaweza kupuuzwa kwa sababu ya upuuzi wa lugha yako
 
Hii nayo ni moja ya habari za uchochezi na tuwe makini na habari kama hizi!
Kwahiyo Waziri Mkuu na Kamanda wa Polisi ni wachochezi?Mkuu kama huna cha kuchangia ni bora uwe msomaji tu,kuliko kuchangia UHARO hapa.Stupid...!
 
Kweli nyani haoni kundule kama wewe. Wewe umeona neno upuuuzi ni zuri kuliko nepi? Hayo unayoniambia kamwambie mama yako uone atakujibuje kama siyo kukuachia laana. Kwa vile mimi ni baba yako nakudharau na kukusamehe.
Hiyo lugha uliyoitumia ya kutumika kama nepi sidhani kama ni sahihi. Kadiri unavyoweza jitahidi kitumia lugha zisizoudhi wengine mawazo yako yanaweza kupuuzwa kwa sababu ya upuuzi wa lugha yako
 
Hiyo lugha iliyoitumia ya kutumika kama nepi sidhani kama ni sahihi. Kadiri unavyoweza jitahidi kitumia lugha zisizoudhi wengine mawazo yako yanaweza kupuuzwa kwa sababu ya upuuzi wa lugha yako
Anaonyesha ni gani anavyokerwa na ufanyaji kazi wa kipuuzi wa hao(Kama ID NAME yako inavyojieleza).
 
Kwahiyo Waziri Mkuu na Kamanda wa Polisi ni wachochezi?Mkuu kama huna cha kuchangia ni bora uwe msomaji tu,kuliko kuchangia UHARO hapa.Stupid...!

Mkuu huwezi kujibu bila kutukana?hebu jiheshimu bana
 
Kweli nyani haoni kundule kama wewe. Wewe umeona neno upuuuzi ni zuri kuliko nepi? Hayo unayoniambia kamwambie mama yako uone atakujibuje kama siyo kukuachia laana. Kwa vile mimi ni baba yako nakudharau na kukusamehe.

Hii style ya kutembea na bangi mfukoni ndo tabu yenyewe kutwa kuzinusa hata mkishauriwa hamtaki haya father of all baki na mdomo wako
 
tunakoelekea hakuna dalili njema ya mahusiano wanananchi na vyombo vya dola hususani jeshi la police
 
Back
Top Bottom