"Polisi mtuhumiwa atoweka, akwepa tuhuma" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Polisi mtuhumiwa atoweka, akwepa tuhuma"

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MpigaKura, Dec 30, 2011.

 1. MpigaKura

  MpigaKura JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: Jan 25, 2007
  Messages: 385
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  POLISI KATIKA TUHUMA ZA UPOTEVU WA $50,000 ATOWEKA

  Tarehe 21 Disemba 2011, gazetini HabariLeo ilichapishwa habari kuwa kiasi cha fedha za Marekani 50,000 (Sh milioni 90) zilizopatikana kwa mmoja wa majambazi watatu waliohusika na uporaji kwa kutumia usafiri aina ya pikipiki maarufu jijini Arusha kwa jina la ‘toyo’ ama bodaboda kwa mikoa mingine nchini, zimeyeyuka mikononi mwa Polisi katika mazingira ya kutatanisha.

  Watuhumiwa hao wa ujambazi walimpora dereva wa gari la hoteli maarufu ya kitalii ya jijini Arusha ya Kibo Palace aliyetambuliwa kwa jina la Onesmo Joseph (28) na kupora dola za Marekani 200,000 (Sh milioni 340).

  Habari za uhakika kutoka ndani ya Polisi na kuthibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Akili Mpwapwa, zilieleza kuwa baada ya fedha hizo kuibwa na baadhi ya askari Polisi wenye kukiuka maadili ya kikazi, tayari askari Polisi wawili wanashikiliwa kwa tuhuma kuhusika katika wizi huo na wako rumande.

  Awali Kamanda Mpwapwa hakuwa tayari kutoa ushirikiano juu ya upoteaji wa fedha hizo kituoni hapo, lakini alipoambiwa kuwa gazeti hili lina taarifa juu ya “kukwapuliwa kwa fedha” hizo na pia gazeti lina majina ya askari hao, ndipo alipokiri kuwa suala hilo lipo na linashughulikiwa kijeshi.

  Mpwapwa alikiri kuwekwa ndani kwa askari hao na kuomba kuacha kutaja majina ya askari kwani uongozi wa Polisi unafanya upelelezi zaidi kwa kuwa kuna taarifa kuwapo askari wengine katika tukio hilo la kuiba fedha za ushahidi, “Kwa sasa hata kama unayo hayo majina usiyataje, acha kwani ukiwataja, wengine wanaweza
  kuharibu ushahidi na mimi na wenzangu tutakuwa na wakati mgumu wa kuwatia hatiani waliohusika kulichafua Jeshi la Polisi,” alisema Kaimu Kamanda.

  Habari za uhakika kutoka Polisi zilieleza kuwa dola 50,000, simu mbili, mfuko uliobeba dola hizo na vitu hivyo vyote, vilichukuliwa na polisi kama ushahidi wakati walipomtia mbaroni mtuhumiwa.

  Vyanzo vya habari vilisema askari hao walifikisha Polisi dola 900 tu na zingine hazijulikani askari hao walizipeleka wapi, simu mbili na mfuko uliobeba fedha hizo za kigeni.

  Habari zaidi zilisema askari hao ‘waliokwapua’ walimshirikisha kigogo waPolisi mkoani Arusha aliyeahidi kuwalinda hadi dakika ya mwisho.

  Dereva Joseph na mtunza fedha wake waliporwa fedha, mita chache kutoka hotelini wakiwa katika Barabara ya Old Moshi, baada ya kuvamiwa na toyo waliojifanya wamegongwa na gari hilo.

  Dereva alipoteremka aliwapa upenyo majambazi hao kupora fedha hizo kirahisi na kutokomea kwa bodaboda na wengine kwa gari.

  29/12/2011
  0 Comments

  LEO gazeti hilo linaripoti "POLISI ATOWEKA, AKWEPA TUHUMA"

  Askari Polisi anayedaiwa kuhusika na wizi wa dola za Marekani 50,000 za kidhibiti katika kituo kikuu cha Polisi jijini hapa, ametoroka na familia yake.

  Askari huyo (jina limehifadhiwa) anadaiwa kutoroka usiku wa manane wakati Tume maalumu ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Said Mwema, ikiwa inaendelea kuhoji polisi na raia juu ya upotevu wa fedha hizo.

  Awali askari huyo, aliwekwa rumande na mwenzake, lakini walipewa dhamana baada ya kuandika maelezo kwa viongozi hao wa juu wa Polisi mkoani hapa juu ya wizi huo.

  Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa, alipoulizwa alikiri kuwekwa ndani kwa askari hao, lakini alikataa kutaja majina yao kwa sababu za kichunguzi juu ya suala hilo.

  Mbali ya askari huyo kutoweka, askari kanzu mwingine mwenye cheo cha Konstebo (jina tunalo), alikamatwa juzi jioni na anashikiliwa katika kituo kikuu cha Polisi kwa madai ya kufahamu mtandao mkubwa wa wizi jijini hapa na kuhusika na wizi wa fedha hizo.

  Mpwapwa alipoulizwa jana kwa njia ya simu juu ya kutoweka kwa askari huyo na familia yake, na mwingine kukamatwa, alisema yeye yuko nje ya mji, labda inawezekana ikawa kweli au la, lakini kwa kuwa yuko nje ya ofisi hilo hatalizungumzia, ‘’Mimi niko Karatu kikazi labda huyo askari alitoroka wakati nikiwa huku na kama kuna mwingine, nikirudi kesho (leo) nitapata taarifa kwa ukaribu zaidi na kupata ukweli wake,’’ alisema Mpwapwa.

  Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, kukamatwa kwa askari kanzu huyo kulitokana na taarifa kutoka kwa raia wema kuwa askari huyo alihusika moja kwa moja na upotevu wa dola hizo.

  Habari zilisema kuwa konstebo huyo piaanadaiwa kumiliki magari ya kisasa jijini Arusha, zaidi ya 10 yakiwamo yaliyokodishwa na mengine kubeba abiria - teksi.

  Vyanzo vya habari vilisema kwamba baadhi ya askari kanzu ambao wanafanya kazi karibu na Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa wa Arusha (RCO) ambao walikuwa zamu siku ya upekuzi nyumbani kwa mtuhumiwa nao tayari wamehojiwa na Tume hiyo ya IGP.

  Fedha hizo za kigeni sawa na Sh milioni 90 zinazodaiwa kuwa sehemu ya dola za Marekani 200,000 zilizoporwa zilioneshwa mahali ziliko na mmoja wa watu watatu wanaosadikiwa kuhusika na ujambazi wa kutumia usafiri aina ya pikipiki maarufu jijini Arusha kwa jina la Toyo ama Bodaboda.

  Fedha hizo dola 50,000 ziliyeyukia mikononi mwa polisi katika mazingira ya kutatanisha.

  Watuhumiwa hao wa ujambazi walifanya uhalifu huo hivi karibuni kwa kumpora dereva wa gari la hoteli maarufu ya kitalii ya jijini hapa ya Kibo Palace, Onesmo Joseph (28), dola 200,000 sawa na zaidi ya Sh milioni 340.

  source: Polisi katika tuhuma za upotevu wa $50,000 atoweka - Wavuti

 2. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  polisi- jambazi-jambazi- polisi hii kali
  nani atatulinda sie wachovu?
  mtu analipwa sh mshahara kidogo afu apate zali kama hilo ataachaiaje wkt anajua familia yake inaishi kwa tabu watoto wake hawana ada atafanyaje? boresheni maslahi yao yafanane na wanajeshi wataacha tamaa.
   
Loading...