Polisi mtaacha lini Rushwa?

Samahani kidogo mjomba! Mimi binafsi yangu natilia shaka saaana mazungumzo yako kuwa polisi " alishirikiana na mlalamikaji wako kukubambikia kesi".
Halafu unasema walipogundua kuwa huna hatia. Ndipo wakang'ang'ania uwape hizo pesa iweje wagundue? Wakati wanakubambikia kesi
 
umesahau kuingia kule ni bure kutoka unalipia...
 
Hapo ndipo mnapokosea!

Kwani wewe hujui KUTOA rushwa ni kosa sawasawa na KUPOKEA rushwa? ??
 
Itaisha tu wakiwapandishia maslahi yao na kuwajali sio muda wote kazini.
 
TAKUKURU? Kuna mhasibu wao bilionea unafikiri ni za mshahara?
Yule mhasibu alikuwa akifisadi hela za miradi mbalimbali ya Taasisi akishirikiana na mabosi wake. Ninaamini wote walioko kwenye hiyo chain watawajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Kitendo cha muhasibu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kuamua kuwa fisadi hakumaanishi tusiripoti matukio ya rushwa Taasisini. Wanalipwa kwa kodi zetu hivyo ni lazima watufanyie kazi! - Nao kama wakituomba tena rushwa, tuwaripoti kwenye mamlaka nyingine hadi KIELEWEKE!!!!
 

Kesi yenyewe ni ya kimtandao kuna group nilijiunga la whatsapp ikawa kuna kazi za msanii fulani zililetwa na admin sasa wakanikamata mimi ambaye sikushiriki kwa lolote zaidi ya kuwepo kwenye hilo group na ushahidi nilikuwa nao kwenye simu yangu maana pia nilikuwa mvivu wa kuchat kutokana na ubize wa kazi zangu...

Lakini wamenisumbua ili tu niwape hela hadi nikawapa ili yaishe, kwa sababu wamedai watapeleka kesi BASATA ili nisimame na serikali..
 
Hiyo ni pesa kidogo tu ya kupigia viatu kiwi siyo rushwa hiyo
 
Wataacha rushwa mbaka wakilipwa mishahara inayo kidhi mahitaji, nishackia police wengi wakilalamikia mishahara.
 
Kwa maana hiyo tuseme jamii iache rushwa kupitia jeshi la polisi. Tusiilalamikie polisi peke yake. Jamii nzima IJITATHMINI
 
Kesi ya madai polisi? Hebu fafanua hapo, maana polisi haihusiki na kesi hizo navyojua.
 
Kusikiliza upande mmoja utaamini tu. Pamoja na hivyo, hebu elezea mazingira ya kukamatwa ili tuone kama kweli ulifanyiwa hujuma au wewe ndo ulifanya hujuma kuukwepa mkono wa dola
 
Umewaon polisi tu mbona wengin hamsemi ao takukuru ndo hao hao mbona hamsemi yule mhadibu wao
Ha ha ha mbuzi hule kulingana na urefu wa kamba yake. Hata kwenye tuhuma, hutuhumu yule unayekutana naye
 
Elezea mazingira tuyapime.
 
upo sahihi mtoa mada na hali hii inawafanya raia wengi wasiwe na imani na askari wengi ambao wanalichafua jeshi la polisi na kusababisha hata polisi waaminifu waonekane ni walewale
kumbe kuna polis waaminifu pia?
 
Hata mahakamani ndo hayohayo tu....Nimejionea mwenyewe this week"!
 
Polepole kasema hata mkulu wachenjua mchanga walitaka kumhonga bilioni 300 aipotezee ile ripoti ya mchanga. Na wala hajawachukulia hatua yoyote.
 
Luka 3:14
Neno: Bibilia Takatifu

14 Na baadhi ya askari wakamwuliza, “Na sisi je, tufanye nini?” Akawajibu: “Msichukue fedha za watu kwa kutumia nguvu; msiwashtaki watu kwa kuwasingizia makosa; bali mtosheke na mishahara yenu!”
 
Kiukweli nliwakomalia Sana hadi mwisho wa Siku wakamuachia
Wataacha utakapoendelea kukomaa bila kutoa rushwa na wengine wasipu toa rushwa polisi wataacha kupokea rushwa kwa kuwa hakuna wakuwapa rushwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…