Polisi Mlandizi wabeza kasi ya utendaji wa Rais Magufuli

security guard

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
799
603


Kituo cha Polisi cha Mlandizi, wilayani Kibaha, Pwani.

Na Mwandishi Wetu

ASKARI wa Kikosi cha Polisi cha Usalama barabarani, Kituo cha Polisi Mlandizi

wamewasotesha kwa takribani masaa mawili na nusu wanahabari kupata risiti

ya malipo ya faini aliyotozwa dereva wao baada ya kudaiwa kufanya kosa la

kutaka kulipita gari lingine sehemu isiyoruhusiwa.

Sakata hilo lilianza wakati polisi alipolisimamisha gari hilo katika Kituo cha

Visiga, Mlandizi, wilayani Kibaha, Pwani ambapo alimuomba dereva leseni yake

na kumuamuru ateremke ili ajieleze akiwa nje ya gari na hatimaye kumlipisha

faini ya sh. 30,000 kwa kosa hilo.

Baada ya wanahabari waliokuwa kwenye gari hilo kumsubiri dereva kwa

takribani nusu saa, waliamua kuteremka kumfuata kujua kinachoendelea, kwani

walikuwa wana haraka ya kufika Dodoma muda waliopangiwa ili waungane na

msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenda Singida kwenye

maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM.

Lakini baada ya mmoja wao kuwauliza Trafiki sababu zinazosababisha

kutomwachia dereva, walijibu kwa kashfa na kejeli, wakihoji kwani nyie ni akina

nani? na dereva wenu asipolipa faini basi watakaa hapo kituoni hadi jioni.

Mmoja wa wanahabari hao alilipa faini ya sh. 30,000 na kuomba risiti.

Hapo ndo songombingo ilianza ambapo Trafiki wa kike alijibu kuwa hawana

risti bali kinachofanyika pale ni kuandikiwa tu taarifa ya kosa lao na kwenda

Kituo cha Polisi cha Mlandizi kilichopo takribani umbali wa Km 5, na wengine

waliokamatwa kwa makosa mbalimbali ya usalama barabarani waliamuliwa

kwenda kupata risiti katika kituo hicho.

Mabishano makubwa yalitokea hapo baina ya Trafiki na wanahabari waliokuwa

wanahoji ni kwa nini kitabu cha risiti wala mashine za kielekroniki havipo hapo

ili kurahisisha kazi. Askari wa kike na mmoja wa kiume walijibu kuwa

wasifundishwe kazi.

"Msitupotezee muda hapa, nendeni Mlandizi, mkapate hiyo risiti,"alisema trafiki

wa kike. Wakati anasema hivyo kumbe mhasibu wao alikuwepo palepale Visiga,

lakini bila kuwaambia ondokeni naye ili akawahudumie."

Pia, mmoja wa Trafiki aliuponda sana utaratibu wa wakosaji kulipia faini kwa

kutumia mashine za elekroniki akidai kwamba ni hasara kwa trafiki na madereva

ni bora mashine hizo ziishie Dar es Salaam zisipelekwe Mkoa wa Pwani.Trafiki

wengine walisikika wakisema kuwa hivi hawa jamaa wanaolazimisha kupewa

risiti ni akina nani, waache waende zao, wakafie mbali.

Maneno hayo yalionekana kuwaudhi wanahabari na kuamua kuondoka kwenda

Kituo cha Polisi Mlandizi, kufuatilia risiti, lakini walichokikuta huko ni maajabu,

hasa ya kuambiwa kuwa Mhasibu hayupo ofisini kwake amekwenda kununua

peni.

Baada ya wanahabari hao kusubiri kwa takribani saa moja, waliamua kwenda

kaunta kuulizia na kuomba kuzungumza na Mkuu wa Kituo ili awasaidie kupata

risiti wawahi kwenda Dodoma, lakini mmoja wa askari aliyekuwa zamu aliwajibu

kuwa Mkuu wa Kituo hajafika ofisini amepitia Kibaha Mjini kwenye mkutano.

Alipoombwa awasaidie kumpata mhasibu, askari huyo alitoka nje hadi ofisi ya

Mhasibu alipomkosa akaamua kumpigia simu na kuwajibu kuwa ametoka mara

moja kwenda kununua peni. Jambo hilo liliwashangaza sana wanahabari na

kuanza kuhoji kwamba iweje kitendo cha kununua peni kitumie muda wote huo

na kusababisha watu wakiwemo wao kukosa huduma tena asubuhi majira ya

saa 3?

Mmoja wa wananchi aliyekwenda kituoni kupata huduma ya risiti, alisikika

akilalamika kuwa tabia hiyo ya kuchelewesha kutoa huduma ipo sana kituoni

hapo na kwamba wanaoonekana kabisa hawaendani na kasi ya kufanya kazi

anayoitaka Rais Dk John Magufuli ya 'Hapa Kazi Tu'.

Mle ndani ya Kituo cha Polisi walisikika wakiulizana kwamba hivi haw watu

wanaowasumbua na kutaka kuzungumza na mkuu wa kituo ni akina nani hawa,

eti wanataka risiti, ebu tumpigie simu mhasibu aje atuondolee balaa hapa.

Baada ya muda askari mwenye E 3275 alitoka nje na kuwaambia wanahabari

kuwa mhasibu amepigiwa simu atakuja muda si mrefu mhudumiwe muondoke,

lakini mmoja wa wanahabari hao anayemiliki blogu ya Full Shangwe, John

Bukuku, alihoji kuwa hivi ni kwanini polisi wa kituo hicho hawaendani na kasi

ya Rais Dk. Magufuli? alijibu kuwa kwani kuna nini?

Baada ya muda Mhasibu aliwasili kwa Bodaboda, na alipofika aliwakebehi

wanahabari kwamba anawashangaa kwa yeye kumuacha kule Visiga

alikokuwa nao na kuwahi kituoni, ndipo wanahabari nao wakashangaa kumuona

tena kituoni hapo wakati wlipofika kituoni waliambiwa ameenda kununua peni.

Dereva alimwambia haya twende ukachukue risiti yako muondoke na

watu wako. Dereva aliingia na kupatiwa risiti kutoka kwenye kitabu kipya

ambacho kwa mujibu wa dereva kilionekana dhahiri kuwa ni kipya.

Lakini kwa masaa yote waliyokaa wanahabari kituoni hapo (takribani masaa

mawili), hawakuwaona madereva wa magari waliokamatwa pamoja na gari lao

na kuandikiwa makosa na faini pale Visiga, hawakufika Kituo cha Polisi

kupatiwa risiti, kitendo ambacho kinaashiria fedha wanazolipishwa madereva

kwa kutenda makosa hazitolewi risiti, hivyo mapato ya serikali kupotelea

mifukoni mwa baadhi ya askari wa kikosi cha usalama barabarani.

Baada ya wanahabari hao kupata risiti majira ya saa 4:15 waliamua kuondoka

kituoni hapo kuanza safari ya kwenda Dodoma kuwahi msafara wa Katibu Mkuu

wa CCM, Komredi Abdulrahman Kinana uliokuwa unawasubiri kwenda Singida.

Mwisho
 
Safi #PT ... fine ya elfu 30 unalia lia huku...kabla huja hoji utendaji kazi wa polisi wa kituoni hapo nadhani ulipaswa kuhoji utendaji kazi wa dereva wenu ...ni kuovertake tuu mnatuulia watoto wetu wakivuka barabara....asante nimepata udaku mwingine.
 
Sijui kama nitakuja niwapende waandishi Wa habari makajanja Wa Tanzania......sasa hill suala MBNA wala hata alikuhitaji majungu yote hayo waliyoyapika....Nafikiri hao waandishi nao hawakuwa wastaarabu....
 
Hii hahari imekaa kiudaku udaku, haina tofauti na habari za magazeti ya udaku na blog za udaku, kwa uandishi huu ni ngumu kuamini habari hii.
 
Tusidharahu kazi za wenzetu kisa eti unamwahi kinana mnaenda spidi kubwa na kulipita gari sehemu isiyoruhusiwa alafu mnaleta jeuri tatizo la magamba kijifanya nchi yao hii nchi ni kufuata sheria tu hongereni maafande kwa kuwachelewesha
 
Kwako mleta uzi....
Je, una uhakika na kosa ambalo lilidaiwa kutendewa na dereva aliekua akiwaendesha?
If ndio, je mlipewa ushahidi wa kuwaonyesha na kuhakiki kosa la dereva wenu?
If hapana, je kwanini mlikubali kulipa faini kwa kosa ambalo hamkulijua au hamkua na uhakika kama dereva wenu amelitenda?
 
Tusidharahu kazi za wenzetu kisa eti unamwahi kinana mnaenda spidi kubwa na kulipita gari sehemu isiyoruhusiwa alafu mnaleta jeuri tatizo la magamba kijifanya nchi yao hii nchi ni kufuata sheria tu hongereni maafande kwa kuwachelewesha


Yaani kudai risiti ni jeuri??!!! Mbona watanzania tunaelewa kidogo sana. Sijaona sehemu panapoonesha wanahabari wamedharau kazi ya wenzao. Acha inferiorities hizo. Mwingine anasema anawachukia waandishi wa habari, kwani wao wamesema wanampenda. Halafu mwandishi mshahara wake unatokana na habari, hasipoandika habari hawezi kula.
 
Binafsi, hawa askari wa mlandizi walinikamata kwa kosa walilo nituhumu kwamba ni wrong overtake.
Kwanza niliwakatalia kwamba hakuna alama au kibao kinacho muonyesha dereva kuto overtake katika eneo walilonieleza. Na baada da mabishano marefu walinijibu kwa kebehi kwamba kama naona ninaonewa wanipe namba ya askari Mangu ili nimeueleze kwamba ninaonewa.
Agghhhh......
Nilijikuta napatwa na jazba zaidi pale askari wa kike around (43-48) akinijibu kwamba usipo lipa faini utajichelewesha wewe mwenyewe, na wakati huo alikua tayari ameishikilia driving licence yangu.
Hapo ilinibidi nikue mpole na nikaamua kulipa hiyo faini.
Hapo mziki mwingine ukakuja.... pale nilipo waomba risiti ya kile nilicho lipia, walinijibu niende kituo cha mlandizi nikachukue hiyo risiti.
Then niliona isekue tabu, nakachomoka hadi mlandizi, kufika naambiwa mtoa risiti hayupo na wakanitaka nikae kumsubiri.
Mmmhhhh......
Hapo kiukweli niliona kuna mazingira ya kutilia mashaka kwa mimi kupata hiyo risiti mara baada ya kumsubiri mtoa risiti kwa zaidi ya dakika 40 pasipo kutokea.
Then, niliamua kusepa tu aiseeee....
 
Lol pale mlandizi kuna trafiki moja jeusiiiiii kazi yake kila gari anayoiona machoni mwake anasimamaisha,hizi gari zinazosafirishwa nje ya nchi ndio zinakoma kwa jinsi wanavyokamuliwa hela na mtoto wa kiongozi flani mstaafu wa jeshi la polis
 
Kuna uzi ulishaletwa hapa kuhusisna na jeuri ya askari wa Mlandizi. Inaonekana hawa watu ni Sugu. Mimi walininituhumu kwa kosa la kuovertake kwenye mstari na nilikuwa sijafanya hivyo. Baada ya mabishano makali sana na vitisho juu ndo wakaniachia. Sina uhakika kama huu ujasiri wanautoa wapi.
 
Dah sikujua kama hii habari ni ya kishambenga sana hivi huu ni ushiranga na ushankunaku mkubwa khaaa
 
Back
Top Bottom