kipara kipya
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 17,336
- 21,431
Nawapongeza sana kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kupambana na uhalifu hapa mkoani kwetu,ila tatizo lipo pale kwenye chaka la majambazi mbona kila mkikamata tu eneo la tukio ni mapango ya amboni,utasikia walikua na mapanga,shortgun,na pikipiki mbili hamjui kila mkitaja eneo mnaweza kutisha watalii wanaoenda eneo hilo kwa kujua kumbe tunakwenda kwenye nyumba ya majambazi tafuteni chimbo jengine la kujinasbu nalo.
Jeshi la Polisi mkoani tanga limefanikiwa kukamata bunduki tatu aina ya shotgun Bastola moja,risasi 51 pamoja na mavazi ya jeshi la wananchi ambazo zimetumika katika vitendo vya uhalifu kwa kupora fedha na mali mbalimbali kisha kuua mmoja kati ya wafanyabiashara wilayani Kilindi.
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga Kamishna Msaidizi wa Polisi Leonard Paul amesema katika operesheni hiyo iliyofanyika katika kijiji cha Kimamba kilichopo kata ya Negero wilayani Kilindi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna mtu aliyejulikana kwa jina la Tabu Chabai anakiwanda cha kutengeneza silaha ndipo walipokwenda kumpekua na kukuta silaha hizo.
Kamanda Paul amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa zitakazo wezesha kukamatwa kwa wahalifu ili kuwapunguzia adha raia wema na pamoja na maisha.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Tanga wameelezea hatua hiyo kuwa imeanza kuwapa imani na jeshi hilo hasa baada ya matukio mfululizo ya ujambazi yaliyotokea katika wilaya za Kilindi na Tanga na kusababisha watu sita kuuawa katika wilaya hizo kwa kupigwa risasi.