Polisi Mbeya yaonya walevi Krismasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi Mbeya yaonya walevi Krismasi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 23, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  POLISI mkoani Mbeya imeonya tabia ya baadhi ya madereva kuendesha vyombo vya usafiri huku wakiwa wamelewa siku za sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

  Onyo hilo lilitolewa jana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Advocate Nyombi aliyesema jeshi hilo halitasita kuwachukulia hatua za kisheria madereva wa namna hiyo.

  Kamanda Nyombi alisema kuendesha chombo cha moto huku ukiwa umelewa pombe, si hatari kwa dereva pekee, bali pia kunahatarisha maisha ya watumiaji wengine wa barabara, jambo lisiloweza kufumbiwa macho na jeshi hilo.

  “Wapo madereva ambao kwa makusudi, siku za sikukuu hulewa pombe na kisha kuendesha vyombo vya moto.

  Nataka kuwaonya kwa ye yote atakayebainika, itakuwa zamu yake kuona mkono wa sheria ni
  mfupi ama mrefu,” alisisitiza Kamanda Nyombi.

  Alitoa pia mwito kwa wakazi mkoani hapa kuimarisha ulinzi jirani kwa kila mmoja kuona ana jukumu la kulinda mali za jirani yake huku pia akisisitiza wananchi kutoacha nyumba zao pasipo walinzi.

  Alisema ni jambo la busara kwao kutoa taarifa katika kituo cha polisi chochote kilicho jirani nao hususani pale wanapoona kuna uvunjifu wa amani na jeshi hilo litahakikisha linafika eneo la tukio mara moja kwa kuwa limejipanga kuhakikisha watu wanasherehekea sikukuu hizo za mwisho wa mwaka kwa amani na utulivu.

  Kamanda Nyombi aliwaasa wazazi kutowaacha watoto kwenda matembezini pasipo mwangalizi wa karibu na kuwasihi mabinti kutozurura ovyo na kupita vichochoroni hususani nyakati za usiku, kwani ni hatari.
   
Loading...