Polisi kupewa posho ya shs 5000/= Igunga, watasimamia haki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi kupewa posho ya shs 5000/= Igunga, watasimamia haki?

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Dullo, Sep 30, 2011.

 1. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2011
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimesoma katika gazeti la Mtanzania la leo linasema kuwa Polisi walioko Igunga wanalipwa posho ya shs. 5,000/= kwa siku na imethibitishwa na mkuu wao Isaya Mgulu eti naye amesema anapata hiyo hiyo, hii inawezekana kweli mtu kulipwa 5000/= halafu akasimamia haki katika uchaguzi?

  Hii naona imekaa vibaya na inachochea rushwa kwa polisi siku ya uchaguzi na kuondoa usawa, jamani hivi kweli mtu akalale nje kwa pesa hiyo halafu asijihusishe na uharifu?

  Nawasilisha kwa wanaJF!!
   
 2. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kilo moja ya nyama, duh,nao wamekubali!Watanzania mavuvuzela kweli.Kwa mtindo huu kwa kweli, wana haki ya kusindikiza malori ya sukari kwenda Kenya.
   
 3. N

  NYAKIMWE Member

  #3
  Sep 30, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Duh!!! hiyo kali yaani hata posho ya mwanafunzi wa elimu ya juu anawazidi,kweli hii country inafurahisha sana!!! kwa nini tusifanye reform kama wenzetu pale Kenya ambapo nafasi ya IGP na wasaidizi wake wanne wana apply hizo nafasi,sio kupeana kama njugu!!!
   
 4. b

  ben genious Senior Member

  #4
  Sep 30, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nyie hawa watu si wa kutetea maana hawana maana, kwanza ndio wa kwanza kuwageuka watetea haki wkitumiwa na haohao wanaowalalamikia, acha wakione cha moto ili akili iwakae sawa
   
Loading...