Polisi kipindi maalum Channel ten

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Kuna kipindi maalum Channel ten hivi mkutano wa makamanda wa ngazi ya juu wa polisi wa mikoa wanakutana na waziri wa usalama na IGP

Ni mkutano mzuri na agenda zenye tija, kujadili ufanisi wa jeshi la polisi na mikakati ya kukabiliana na changamoto. Unafanyika CCP moshi

Kilichonitia hamaki ni umri wa washiriki. Wote wanaonekana Kama vile wana umri kati ya miaka 55 na kuendelea. Hawa ndio wanaotoa amri zote nchini dhidi ya wananchi wanaooandamana kudai haki zao.

Ngazi ya juu ya serikali nayo imejaa wazee. Ngazi ya juu ya chama tawala nayo ni wazee tena wastaafu, isipokuwa vijana watatu walioteuliwa jana.

Wanalalamika kwamba vijana wengi wako upinzani, wanapinga serikali, hawapendi chama tawala, hawapendi jeshi la polisi

Tafakari
 
Hilo ni jeshi la CCM tu, haliko kulinda usalama wa wananchi, likiagizwa na CCM likaue raia wanaondamana kwa mujibu wa haki zao za msingi lenyewe huwa linatekeleza bila kufikiri.
 
Back
Top Bottom