Polisi kinara tena wa rushwa nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi kinara tena wa rushwa nchini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, May 30, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba


  Jeshi la Polisi hapa nchini limetajwa kuwa taasisi ya serikali inayoongoza kwa kupokea rushwa huku Tanzania ikishika nafasi ya tatu kwa vitendo hivyo katika nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), mwaka 2011.

  Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya haki za binadamu iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kwa mwaka 2011.

  Ripoti hiyo ilizinduliwa jana jijini Dar es Salam na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba.

  Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Polisi wanaoongoza kwa rushwa kwa asilimia 36.2, wakifuatiwa Mahakama asilimia 32.4, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), asilimia 15.1, Hospitali asilimia 8.6, na Wizara ya Ardhi imepewa asilimia 5.3.

  Katika ripoti hiyo Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni za (Brela), ndiyo taasisi iliyoonekana kutojihusisha na vitendo vya rushwa ambapo imeshindwa kupewa asilimia yoyote.

  Ripoti hiyo ilisema kwamba Tanzania kwa mwaka 2011 ilishika nafasi ya tatu kwa vitendo vya rushwa kwa asilimia 31.6, Uganda asilimia 33.9. Kenya asilimia 28.8, Rwanda asilimia 5.1 huku Burundi ikiongoza kwa kuwa na asilimia 37.9.

  Aidha, ripoti hiyo imeeleza kwamba mwaka 2011 jeshi la Polisi liliua raia 25 kwa risasi, huku watu 673 wakiua na wananchi wenye hasira katika matukio mbalimbali.

  Mkoa wa Dar es Salaam umetajwa kuwa unaongoza kwa mauaji yanayotokana na watu wenye hasira ambapo ripoti inaonyesha kwamba mwaka 2011 watu 150 waliuwa.

  Baadhi ya mikoa na idadi ya watu waliouawa kwenye mabano ni Mbeya (43), Mwanza (84), Shinyanga (80), Kilimanjaro (59), Tabora (58), Kagera (33), Mara (20), Tanga (16) na Morogoro (15).

  Ripoti hiyo ilibainisha kwamba mwaka 2011 wanananchi waliwaua polisi watano katika mikoa mbalimbali hapa nchini kuanzia Januari hadi Desemba.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Profesa Lipumba alisema LHRC imekuwa ikiibua vitu vingi ambavyo vinachangia kuibua, kuielimisha, kulinda na kutetea haki za binadamu hapa nchini.

  Profesa Lipumba aliwakumbusha viongozi wa nchi kuwa waadilifu na kuachana na vitendo vya ubadhirifu wa fedha za wananchi zinazotokana na kodi.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa LHRC, Dk. Hellen Kijo- Bisimba alisema vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu hapa nchini vinaongezeka.

  Alitaja baadhi ya vitendo hivyo kuwa ni pamoja na kuendelea kuwepo kwa adhabu ya kifo, unyanyasaji wa majumbani, mauji yanayofanywa na wananchi pamoja na ajali za barabarani.
  CHANZO: NIPASHE

   
 2. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,755
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  We are at it again.
   
 3. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  nafasi ya tatu? tuko kati, haitishi sana. polisi lazima watajwe kuwa wala rushwa kwa kuwa rushwa yao inawahusisha watu wengi halafu maskaini, wanaotoa huku wakilia na ni walalamishi tena rushwa hizo ni kuanzia 500/-, 1,000/-, 2,000/-. rushwa ya laki huwa ni nadra sana, labda katika ajali ambapo wahusika ni wenye nazo. Haki ya binadam wasiwe imprical kwa kuhesabu matukio, wawe rational kwa kufuatilia kiasi cha pesa kilichohusika katika idara mbalimbali. utakuta POLISI inakuwa ya mwisho. wapo wala rushwa, sio polisi wanao ganga njaa kutokana na maisha magum waliyonayo.
   
Loading...