Polisi kama ndio hivi hamna intelejensia

Polisi kama ndio hivi hamna intelejensia

pansophy

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2011
Posts
502
Reaction score
320
Kwa kweli inasikitisha kuona raia hawana amani na Jeshi la Polisi nchini.

IGP na viongozi wengi wamekuwa wakiomba umma kutoa ushirikiano kwa Polisi ili kuweza kukomesha vitendo vya kihalifu. Lakini hali inakuwa tofauti pale raia wema wanapojitolea kutoa taarifa kwa Polisi tena hii imetokea kwa Mkuu wa Kituo na mkuu wake wa upelelezi.

Taarifa zilipokelewa na vipolisi hivi (nasema vipolisi kwani hawana hadhi kuwa polisi) na mtuhimiwa alikamatwa, katika hali ya kushangaza vipolisi hivi vikamtaja raia aliyetoa taarifa zilizopelekea mtuhumiwa kukamatwa.

Tena kwa kujitapa kabisa wakasema "Kwani ni sisi, Mzee XXY (Jina nalihifadhi) ndio alituambia kuhusu wewe na mambo unayoyafanya, uwe makini na vizee kama hivi".

Sasa najiuliza kama huyu mzee aliyejitolea kutoa taarifa halafu anaanikwa na kuhatarisha maisha yake hiyo intelejensia ya polisi iko wapi?Weledi wa hawa Polisi uko wapi?

Kwa hali hii polisi sahauni kupata ushirikiano kutoka kwetu
 
Kwa kweli inasikitisha kuona raia hawana amani na jeshi la polisi nchini. IGP na viongozi wengi wamekuwa wakiomba umma kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuweza kukomesha vitendo vya kihalifu. Lakini hali inakuwa tofauti pale raia wema wanapojitolea kutoa taarifa kwa polisi tena hii imetokea kwa Mkuu wa Kituo na mkuu wake wa upelelezi. Taarifa zilipokelewa na vipolisi hivi (nasema vipolisi kwani hawana hadhi kuwa polisi) na mtuhimiwa alikamatwa, katika hali ya kushangaza vipolisi hivi vikamtaja raia aliyetoa taarifa zilizopelekea mtuhumiwa kukamatwa.

Tena kwa kujitapa kabisa wakasema "Kwani ni sisi, Mzee XXY (Jina nalihifadhi) ndio alituambia kuhusu wewe na mambo unayoyafanya, uwe makini na vizee kama hivi". Sasa najiuliza kama huyu mzee aliyejitolea kutoa taarifa halafu anaanikwa na kuhatarisha maisha yake hiyo intelejensia ya polisi iko wapi?Weledi wa hawa Polisi uko wapi?

Kwa hali hii polisi sahauni kupata ushirikiano kutoka kwetu
طيب

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aiseeee pole sana mkuu labda pesa imenunua haki
 
Kama vilimtaja basi vina kiherehere,nashauli vitandikwe makwenzi.
 
Kwa Africa usije ukajiroga kuwaambia Polisi Fulani ni mwizi au ndio anaowasumbua kaa ukijua wanakuja kumwambia kuwa tumeambiwa na Fulani.
 
Kwa kweli inasikitisha kuona raia hawana amani na Jeshi la Polisi nchini.

IGP na viongozi wengi wamekuwa wakiomba umma kutoa ushirikiano kwa Polisi ili kuweza kukomesha vitendo vya kihalifu. Lakini hali inakuwa tofauti pale raia wema wanapojitolea kutoa taarifa kwa Polisi tena hii imetokea kwa Mkuu wa Kituo na mkuu wake wa upelelezi.

Taarifa zilipokelewa na vipolisi hivi (nasema vipolisi kwani hawana hadhi kuwa polisi) na mtuhimiwa alikamatwa, katika hali ya kushangaza vipolisi hivi vikamtaja raia aliyetoa taarifa zilizopelekea mtuhumiwa kukamatwa.

Tena kwa kujitapa kabisa wakasema "Kwani ni sisi, Mzee XXY (Jina nalihifadhi) ndio alituambia kuhusu wewe na mambo unayoyafanya, uwe makini na vizee kama hivi".

Sasa najiuliza kama huyu mzee aliyejitolea kutoa taarifa halafu anaanikwa na kuhatarisha maisha yake hiyo intelejensia ya polisi iko wapi?Weledi wa hawa Polisi uko wapi?

Kwa hali hii polisi sahauni kupata ushirikiano kutoka kwetu
Tafadhali sana peleka taarifa hizi ngazi za juu ili uchunguzi ufanyike hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya wahusika manake hili ni kosa baya sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii imetokea wapi na lini..??
Kama unataka kweli Mzee huyo apate sahiki ya kulindwa na Polisi hao walio vujisha taarifa hizo wawajibishwe.... ebu tuelekeze wapi tukio hili linetokea
Mabwepande polisce post, siku tatu nyuma
 
Kwa Africa usije ukajiroga kuwaambia Polisi Fulani ni mwizi au ndio anaowasumbua kaa ukijua wanakuja kumwambia kuwa tumeambiwa na Fulani.
Niliwahi cheka sehemu 1 inaitwa mpanda hotel iko katavi kule hata mtoto wa darasa la kwanza hawezi mwambia flani yuko wapi? kama akiulizwa.

siku moja anatafutwa jamaa watoto wakaambia askari hawamfahamu huyo bwana dk 2 dogo anaenda kumstua jamaa kwamba anatafutwa.

polisi wana matendo ya hovyo yanayofanya jamii isiwape ushirikiano
 
Toa taarifa za kiintelejensia kwa Polisi kwa njia ya barua na kuipost na usiandike jina lako.
 
Back
Top Bottom