Polisi Igunga wanavyofanya madudu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi Igunga wanavyofanya madudu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nyandaojiloleli, Mar 29, 2012.

 1. n

  nyandaojiloleli JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]HAYA HAPA NI MALALAMIKO YA WANANCHI KWA IGP.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]IGP,[/FONT] [FONT=&quot]S.L.P 9141,[/FONT] [FONT=&quot]DAR ES SALAAM.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot] YAH: MALALAMIKO DHIDI YA POLISI IGUNGA[/FONT] [FONT=&quot] Ndugu mkuu wa jeshi la polisi Tanzania rejea mada tajwa hapo juu yahusika mno mimi mwenye jina na anuani hapo juu ni raia wa kijiji cha Imalanguzu kilichopo wilaya ya Igunga na ni mmoja wa familia ya Bi Kija Tungu.[/FONT] [FONT=&quot] Nimeadhimia kukuandikia haya malalamiko kuwa Polis Igunga wameshindwa kutenda haki katika tatizo la mgogoro wa Ardhi uliokuwa unahusisha familia ya Kija Tungu na familia ya Lutoba Masaka. Bi Kija ni mmiliki wa shamba hilo siku zote na Mzee Lutoba Masaka ambaye anataka kumupokonya eneo hilo.[/FONT] [FONT=&quot] Kesi ilianzia Baraza la mwenyekiti wa kitongoji na maamuzi yakatoka kuwa Bi Kija ndiye mmiliki halari wa eneo hilo. Baadaye kwa hatua nyingine Mzee Lutoba alifungua kesi Baraza la kijiji Baraza hilo lilifika kwenye eneo la mgogoro likatoa maamuzi kuwa Bi Kija ndiye mmiliki wa eneo hilo.[/FONT] [FONT=&quot] Kwa hatua nyingine mmoja wa familia ya mzee Lutoba aitwaye Mathias Lutoba alipeleka kesi hiyo kwenye baraza la kata ya Mwamashimba akafungua kesi cha ajabu hakuhudhulia kwenye kesi hiyo badara yake akaenda moja kwa moja kwa mwenyekiti wa baraza la Ardhi na nyumba la wilaya Tabora linaloendeshwa na Bwana Emmanueli Sululu. Baadaye Bi Kija pamoja na mashahidi wake waliitwa kwenye baraza hilo wakatoa ushahidi wao lakini ushahidi huo haukuandikwa kwenye mwenendo wa shauri hilo hivyo mwenyekiti huyo wa Baraza la ardhi wilaya akamkabidhi shamba hilo mzee Lutoba na mwanae Mathias. Kama haitoshi eneo lililokuwa kwenye mzozo ni Ekari 22 lakini mzee Lutoba na mwanae Mathias waliporudi wakatangaza kuchukua mashamba yote yaliyo karibu na eneo hilo hivyo akaingia kwenye shamba la mzee Nkalango Sungula na kuanza kulifyeka mzee Kalango alipoona hivyo aliamua kwenda kwenye eneo lake akiwa na silaha za jadi ili amsubili huko wamalizane kwa vile yeye hana uwezo wa kwenda mahakamani Bwana Mathias alipoona huyo mzee yuko tayari kwa kuuana akaacha akavamia shamba la Salli Shidi akaanza kulilima kwa kukatia kama ekari moja mwenye eneo akashituka na kwenda kulilima kwa kusaidiwa na wanakijiji wenzake kwa majembe ya kukokotwa na Ng’ombe wakalilima eneo lake lote. [/FONT] [FONT=&quot] Baada ya siku kadhaa kupita polisi wapatao wanne wenye silaha na Bwana mmoja waliyemtambulisha kuwa yeye ni Darali kwa jina la Ramadhani Magembe wakaingia kijijini hapo kwa lengo la kukamata Ng’ombe hamsini(50) kwa wajukuu wa Kija Tungu ambao ni Salli Shidi, Keya Shidi,Sollo Shidi na pawa Shidi. Walipokamata ng’ombe hizo wanakijiji walipiga yowe ili kuwasaidia wenzao wasionewe na polisi. Umati ulikuwa mkubwa hivyo polisi waliogopa wakarudi. Baada ya wiki tatu(3) wakafika tena kijijini Jogohya wakiwa maasikali kumi na wawili (12) wakiwa na mabomu ya machozi wakakuta ng’ombe hawapo wakamkata Bi Kija Tungu wakaanza kumtembeza hadi usiku wakitaka awaonyeshe walipo ng’ombe lakini hawakuzipata hivyo Bi Kija aliwekwa Rocup na kulala hapo kesho yake akafunguliwa kesi mahakamani kwa kosa la kuzuia polisi kufanya kazi. Ndipo nilipoenda kwenda kwa mkuu wa wilaya kumpelekea taarifa hizi na kukiri kuwa hana nakara ya hati hiyo ya kwenda kukamata mali huko, nikamuomba kufika kwenye eneo hilo ili kubaini ukweli DC Bi Fatma Kimario kama mwenyekiti wa kamati ya urinzi na usalama ya wilaya aliondoka yeye kama mkuu wa wilaya na kamati nzima ya ulinzi wakiwemo usalama wa taifa wilaya,Afisa TAKUKURU wilaya, DSO, OC.CID, Mwanasheria wa halmashauli ya wilaya,Afisa wa jeshi la wananchi afisa magereza toka Gereza la wilaya na wengine kutoka kamati ya ulinzi. Walikutana na wanakijiji na kuujua ukweli wote wakaahidi kudhibiti hali hiyo.[/FONT]
  [FONT=&quot] Siku kadhaa zikapita Mathias Lutoba akaingia kwenye shamba la Salli Shidi na kuanza kufyeka mazao mwenye shamba hilo akaenda kwa mwenyekiti wa kijiji aitwaye Yohana Ngehu akashindwa kutoa msaada kwa vile naye anaendelea na kesi ya kuzuia polisi kufanya kazi na yuko nje kwa dhamana baada ya kukaa sana mahabusu. Hivyo walinipigia simu kwa maana walitaka kumpiga mathias nikawasihi wasimpige wanisubili kweli nilipofika nikashuhudia ndipo nikamchukua mwenyekiti wa kijiji hadi polsi kwa OC.CID tukatoa maelezo yetu lakini bado mathias hajachukuliwa hatua yoyote na polisi baadaye alirudia tena kwa kwenda na familia yake yote ya watu saba (7) wakaingia kwenye shamba la Salli Shidi na kufyeka mazao kijana alipokosa msaada alidhimia kuwafuata humo shambani alipofika ugomvi ukaanza mathias alikuwa na jembe na mpini akamrushia akampiga mkono na Salli alikuwa na fimbo ikakatika bahati nzuri bwana mathias akaanguka ndipo aliponyang’anywa mpini na jembe na akamshambulia hadi kumjeruhi na kumuacha kesho yake mathias akaenda polisi kama kawaida yake akatoa taarifa baadaye mimi nikaenda na huyo Salli hadi polisi hawakufungua kesi yoyote zaidi ya kutoa PF3 tu matokeo yake polisi walianza kukamata watu wengine ambao hawakuhusika katika ugomvi huo na kuwapeleka mahakamani hadi leo baada ya kumuhoji OCS akanijibu alitumia uungwana tu kutokumkamata Salli Shidi siku hiyo.[/FONT]
  [FONT=&quot] Mpaka sasa katika kijiji cha Jogohya ameuawa mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Mbalu Giguna baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kari alipokuwa akivunja mahindi kwenye shamba la Salli. Tukio hilo lilitokea tarehe 12/03/2012 mama huyo alipohojiwa kwanini anavuna mahindi kwenye shamba ambalo si lake alidai kaambiwa na mwanae mathias na wakimpiga wataiona polisi. Hivyo wananchi wakapandwa na hasira wakampiga mpaka akafa. Baada ya tukio hilo wanakijiji walikimbia familia zao kwa kuogopa kukamatwa na polisi. Baada ya hapo bwana Mathias akaunda kikosi cha kulipiza kisasi kikiongozwa nay eye mwenyewe na familia yake na shemeji yake bwana James Fale wa Igunga nakuanza kupiga wanawake ambao waume zao walikuwa wamekimbia na kuvunja nyumba ya Bi Kija Tungu na kukatakata vitanda vyote na magodoro na kwa Salli wakafanya hivyo hivyo wakaenda kwenye familia nyingine wakamkamata mototo na kumweka kwenye mti wakitishia kumuua kama hatamuonyesha baba yao alikoenda. Hadi sasa Mathias Lutoba na James Fale na wenzao walimkamata mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Mwanankinda mke wa mzee Madakila ambaye alikimbia walimchukua usiku awaonyeshe aliko na mpaka sasa hajulikani alipo na kwamba yu hai ama wamemuua na polisi hawataki kuchukua hatua yoyote na hali ya Jogohya bado ni mbaya sana kwa maana watoto wengi sana hawaend shule kwa ajiri yakuhofia maisha yao na wazazi wao wakiwa wamekimbia na familia ya Mathias inatumia mazao yao. Tunaomba ofisi yako ichukue hatua za zarura ili kuondo hali hii tete iliyojikeza katika kijiji hiki cha Jogohya.[/FONT]
  [FONT=&quot] Wako mwanakijiji [/FONT] [FONT=&quot] …………………………………[/FONT] [FONT=&quot] Antony Kayange [/FONT]
   
 2. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,753
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  Inatia uvivu kusoma Mkuu,panga kwa aya basi.
   
Loading...